Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ibrahim Bacca; Askari kamili aliyejitosa kumtetea mwananchi Novatus

Bacca 8028460 Ibrahim Hamad Bacca

Sat, 9 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tanzania imefanikiwa kufuzu fainali za AFCON 2023 usiku wa juzi baada ya kitoa sare ya bila kufungana na Timu ya Taifa ya Algeria katika Dimba la May 19, nchini humo.

Matokeo hayo yalizifanya Algeria kufikisha alama 16 akiwa kinara wa kundi na Tanzania alama 8 katika nafasi ya pili, alama hizi hazingeweza kufikiwa na timu yoyote kwenye kundi hilo, hivyo Uganda na Niger wakaaga mashindano dakika za lala salama.

Hapa nakupitisha kwenye tukio moja dakika za mwisho kabisa za mchezo wa Tanzania na Algeria, kuna tukio lilitokea uwanjani ambapo mchezaji wa Stars, Novatus Dismas alichezewa vibaya wakati mpira unakwenda kutoka.

Novatus Dismas alisukumwa bila sababu na mchezaji wa Algeria, beki kitasa Ibrahim Hamad Bacca akaamua kuvua jezi na kuvaa gwanda kumtetea raia wa Jamhuri aliyeonewa, alianzisha varangati zito mbele ya Waarabu, huyo ndio Askari aliyesababisha mechi isimame kupisha jambo la kikatiba.

Bendera imepiganiwa ndani na nje ya uwanja kwa wivu mkubwa saana, unyonge umeisha na Mwalimu Nyerere aliwahi kusema anataka kizazi jeuri kisichoogopa, Annaba ni mbali ila Askari alitetea bendera.

Ikumbukwe kuwa, kabla ya kugeukia soka, Bacca alikuwa askari wa kikosi cha kuzuia magendo Zanzibar (KMKM) kwa Tanzania Bara ni kama TAKUKURU, hata Yanga walimtoa kwenye timu KMKM wakati wa michuano ya Kombe la Mapinduzi mwaka 2021/22 na sasa anaipeperusha Bendera ya Yanga, Bendera ya Zanzibar na Bendera ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania karika tasnia ya Soka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: