Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gambia na maajabu yao AFCON, Yatinga robo fainali kwa kuichapa Guinea

Skysports Gambia Afcon 5651461 Wachezaji wa Gambia wakimpongeza mfungaji wa goli la ushindi, Musa Barrow

Mon, 24 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakicheza kwa mara ya kwanza michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2021, Gambia wameendelea kuandika rekodi baada ya kufuzu kucheza hatua ya robo fainali kwa kuifunga Guinea bao 1-0 mchezo uliopigwa Leo Jumatatu.

Bao pekee la ushindi limefungwa na mshambuliaji wa Bologna inayoshiriki Ligi Kuu nchini Italia Seria A Musa Barrow akimalizia kazi nzuri ya Aly Keita kunako dakika ya 71 ya mchezo.

Pamoja na ushindi huo, Gambia walimaliza mchezo wakiwa pungufu kufuatia Yusupha Njie kuonyeshwa kadi nyekundu dakika tatu kabla ya mbungi hilo kumalizika.

Gambia ambao wanashika nafasi ya 150 kwenye viwango vya Fifa watacheza na mshindi baina ya Comoros au Cameroon katika hatua ya robo fainali ya Afcon 2021 ambapo tayari ubingwa uko rehani baada ya Algeria kutupwa nje hatua ya makundi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: