Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gambia Yaichapa Tunisia Afcon 2021

Gambia Wachezaji wa Gambia wakifurajia ushindi

Fri, 21 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya taifa ya Tunisia licha ya kuwa timu yenye kupewa kipaumbele cha kutwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2021 lakini kwenye hatua ya makundi wameanza wakiwa chini kwa ubora ambapo mchezo wa mwisho wamekubali kipigo cha goli 1-0 kutoka kwa Gambia.

Ikiwa timu yenye viwango vya Fifa vya chini katika Kundi F, Gambia imemaliza hatua ya makundi ya michuano hiyo bila hata kupoteza mchezo ambapo wamevuna alama saba, ushindi mara mbili na sare moja.

Tunisia walikuwa kwenye nafasi ya kupata ushindi ungwe ya kwanza lakini mlinda mlango Baboucarr Gaye aliokoa mchomo wa Seifeddine Jaziri, likiwa ni tuta la tatu kukosa katika mechi tatu zilizopita.

Makosa ya kukosa penati yakatumiwa vyema na Musa Barrow kwa shuti kali la hatua kama 25 hivi na Ablie Jallow shuti lake kugonga mwamba.

Matokeo hayo yanaifanya Tunisia kumaliza nafasi ya tatu kwenye Kundi F wakati Gambia wakishika nafasi ya pili na watacheza na Guinea hatua ya 16 bora.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: