Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fountain Gate yajitetea kwa Kagoma

Kagoma Saido Fountain Gate yajitetea kwa Kagoma

Fri, 9 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Fountain Gate FC umekanusha juu ya kumuwekea pingamizi aliyekuwa kiungo wao, Yusuph Kagoma aliyesajiliwa na Simba kwa makataba wa miaka mitatu.

Kagoma hajaonekana katika mchezo wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii, dabi dhidi ya Yanga na kutokea sintofahamu kuwa waajiri wake wa zamani wameweka pingamizi asiichezee Simba hadi watakapofuata taratibu.

Akizungumza nasi, Ofisa habari wa Fountain Gate FC, Issa Mbuzi amesema hawana shida na kiungo huyo kwa kuwa Simba wamefuata sheria zote za usajili kwa mchezaji mwenye mkataba.

“Hakuna pingamizi lolote ambalo tumeliweka kwa Kagoma asiitumikie Simba. Wana sababu zao na kiungo huyo amepewa baraka zote kujiunga na klabu hiyo,” amesema Mbuzi.

Imeelezwa kuwa kiungo huyo hakuwa sehemu ya kikosi kwa sababu alikuwa majeraha na ameanza kurejea taratibu kufanya mazoezi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: