Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fahamu mifumo ya kocha mpya Simba

Fadluraghman 15.jpeg Kocha Fadlu Davids.

Mon, 1 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Sioni sababu ya kwanini asiwe mali nzuri sokoni katika dirisha hili la uhamisho (anasakwa na Simba), Kocha Fadlu Davids ambaye amekuwa na sifa nzuri katika coaching yake kwa timu alizowahi kuzifundisha akiwa Head Coach, Assistant Manager.

Tuangalie sifa zake za ufundishaji 1: POSSESSION BASED – Huyu anapenda sana kucheza one touch football ambapo wachezaji huchukua nafasi na kuunda faida ya namba uwanjani kwenye nyakati mbili muhimu attacking and defending, na pattern huonekana kwa pembetatu au almasi kwa lugha nyepesi anapenda kucheza pira biriani (position play).

2: A GOOD LEADER (COACH) – Huyu ni Kocha ambaye ambaye anajua kucoach wachezaji vizuri na pia ni kiongozi bora sana kwa wachezaji wake ndani na nje ya uwanja ,unaweza kuwa Kocha mzuri kiufundi lakini usiwe kiongozi bora ila Fadlu Davids anakupa faida ya vitu hivyo viwili kwa pamoja.

Fadlu Davids (43) anaweza kuorganize timu kwa ustadi mzuri sana, na competent sana why? Amefanya kazi zake katika vilabu vya Maritzburg United, B. Fontein Celtic, Chippa United, Loko Moscow, Orlando Pirates, Raja Casablanca amezicoach hivi vilabu kuna timu zingine.

akiwa (Head Coach, Assistant Manager) Kitu ambacho huwa anapenda sana kwa Kocha Fadlu Davids ni kuwa na wachezaji ambao wapo possession based ili kushindania mipambano yake kwa ustadi wa hali ya juu, na formation yake pendwa ni 4-2-3-1.

4-2-3-1 pia havutiwi na wachezaji ambao wapo vertical style maana yake katika falsafa zake hawatokuwa wafanisi KWA MAANA HIYO SIONI SABABU KWANINI ASHINDWE KUFUNDISHA TIMU: KUIMARISHA AU KUBORESHA TIMU, NI KOCHA MWENYE CHARISMA BORA SANA.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: