Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fadlu apangua wanne, Simba ikiivaa Coastal

Grfstcdtrdc Fadlu apangua wanne, Simba ikiivaa Coastal

Sun, 11 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha wa Simba, Fadlu Davids amepangua wachezaji wanne katika kikosi kilichoanza katika mchezo uliopita wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga wakati ikivaana na Coastal Union kusaka ushindi wa tatu wa michuano hiyo ya kuzinduliwa msimu mpya wa 2024-2025.

Msauzi huyo amegusa maeneo mawili tu ambayo ni ukuta na kiungo kwa kuwaweka nje, Shomary Kapombe, Chamou Karaboue, Mzamiru Yassin na Edwin Balua, akitoa nafasi kwa Kelvin Kijili, Abdulrazak Hamza na Augustine Okajepha na Saleh Karabaka aliowaanzisha.

Licha ya kuwa na uwezo wa kucheza kama beki wa pembeni, Hamza aliyetokea Supersport United ya Afrika kusini atatumika kama beki wa kati akicheza sambamba na Che Malone.

Kijili ambaye alingia kipindi cha pili katika dabi dhidi ya Yanga, ataendelea kutumika upande wa beki ya kulia huku kushoto akisalia nahodha wa kikosi hicho, Mohammed Hussein 'Tshabalala'.

Viungo wa kati ni Okajepha na Debora Fernandes ambao walicheza pamoja kipindi cha pili katika dabi, mawinga ni Karabaka na Joshua Mutale huku Jean Charles Ahoua na Steven Mukwala wakiongoza mshambulizi ya wekundu hao wa Msimbazi.

Kikosi Kamili; Moussa Camara, Kevin Kijili, Mohammed Hussein, Abdulrazak Hamza, Augustine Okajepha, Saleh Karabaka, Debora Fernandes, Steven Mukwala, Jean Charles Ahoua na Joshua Mutale.

Coastal Union; Chuma Ramadhani, Jackson Shija, Mukrim Issa, Abdallah Denis, Semfuko Daudi, Denis Modzaka, Ramadhan Iddy, John Makwata, Lucas Kikoti na Hernest Malonga.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: