Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fadlu alia mabao machache kwa washambuliaji wake

Fadlu Davids Misriii Fadlu alia mabao machache kwa washambuliaji wake

Tue, 30 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids amedai lengo la kucheza mechi za kirafiki za ndani ni kuficha kikosi chake kwa lengo kutaka kuona muunganiko wa timu yake na suala la ufundi kwa kila mchezaji kupata nafasi ya kucheza katika maandalizi ya kambi ya wiki mbili, nchini Misri.

Amesema ilikuwa ni mechi za kiunfundi na mbinu hali na kutaka kuda mzuri wa kuandaa timu yake bila presha yoyote hali iliyopelekea timu yake kucheza mechi bila ya mashabiki wao kuona kikosi chao cha msimu huu.

Simba imekamilisha wiki mbili za maandalizi ya msimu wa 2024/25 wa mashindano na kucheza michezo mituatu ya kirafiki na jana walikamilisha program yao ya mechi ya kirafiki dhidi ya Al Adalah ya nchini Saudi Arabia kwa ushindi wa mabao 2-1 yaliofungwa na Joshua Mutale na Steven Mukwala.

Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu amesema amepata muda mzuri wa kuandaa timu kwa kupata mechi za kirafiki kwa ajili ya kupata ubora wa kikosi na muunganiko wa mchezaji mmoja mmoja kupata nafasi ya kucheza.

“Zilikuwa wiki tatu nzuri za maandalizi tumecheza mechi tatu za kirafiki, hazikuwa kwa ajili ya kutafuta ushindi ni kuwapa nafasi ya kila mchezaji kucheza na kuona niliyowapa mazoezi wamefanyia kazi.

Katika mechi zimenipa mwanga wa kuona ubora na madhaifu ya kikosi, sina mashaka kwa sababu nimeona sehemu ya ulinzi iko vizuri, kiungo na washambuliaji kwa kufuata kile nilichowapa kwenye mazoezi,” amesema Kocha huyo wa Simba.

Amesema katika michezo ya kirafiki waliyocheza ameona mabadiliko na bado kuna mapungufu madogo anahitaji kufanyia kazi ikiwemo safu ya ushambuliaji kwa kuwa wanatengeneza nafasi nyingi.

“Eneo la ushambuliaji tumekuwa tukitengeneza nafasi nyingi lakini zinazotumika vizuri ni chache, nahitaji kuzidi kuliimarisha eneo hilo, lakini pia wachezaji wawe na moyo wa ushindi, kiujumla timu ipo vizuri ” amesem Fadlu.

Amesema anachokipenda ni kujituma kwa wachezaji kila unaempa nafasi anaonyesha kazi nzuri. wakati wa mashabiki kwenda kwa wingi Jumamosi kwenye Simba Day ‘Ubaya Ubwela ‘ kuona timu yao mpya ya msimu ujao na jinsi walivyojiandaa.

Kikosi cha Simba kinarejea kesho nchini wakitokea Misri walipoweka kambi na tayari kwa ajili ya mchezo dhidi ya APR FC ya Rwanda katika kilele cha Simba Day utakaochezwa, Agosti 3, 2024, uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: