Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

FC Barcelona yathibitisha kumrudisha Messi

Messi Barca Argentina Numeros 285606.jpeg FC Barcelona yathibitisha kumrudisha Messi

Tue, 24 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi wa michezo wa FC Barcelona, Deco amefichua kuwa klabu hiyo inakusudia kuandaa mchezo wa kumuaga Lionel Messi.

Messi ndiye mwanasoka bora zaidi kuwahi kuichezea FC Barcelona, na kuwa mfungaji bora wa muda wote wa klabu hiyo akiwa na mabao 672 katika mashindano yote na mfungaji bora wa muda wote akicheza mechi 778 katika mashindano yote katika miaka yake 17 ndani ya kikosi cha kwanza.

Klabu hiyo ililazimika kumruhusu mchezaji huyo kuondoka mwaka 2021 kutokana na matatizo ya kifedha, huku Messi akitumia misimu miwili katika Klabu ya Paris Saint Germain.

Baada ya kumalizika kwa mkataba wake wa miaka miwili katika klabu hiyo ya Ligue 1, Barca walijaribu kumsajili tena Messi, lakini hawakuweza kutokana na matatizo ya kifedha.

Kwa hiyo, Messi alihamia Inter Miami ya Ligi Kuu ya soka Marekani (MLS), ambapo amemaliza kampeni yake ya kwanza akifunga mabao 11 katika mashindano yote.

Bila kufuzu kwa hatua ya mtoano, uvumi umeenea kuhusu uwezekano wa kurejea Barani Ulaya kwa mkopo wakati wa msimu wa baridi.

Mshambuliaji huyo maarufu tangu wakati huo amefutilia mbali uvumi huo, hata hivyo akizungumza na Lance, Mkurugenzi wa Michezo wa Barcelona, Deco amefichua kwamba mashabiki wanaweza kutarajia kumuona Messi akirejea katika rangi ya klabu hivi karibuni.

“Nadhani kutakuwa na mchezo wa kumuaga, lakini labda katika uwanja mpya ukiwa tayari. Daima atakuwa sanamu kubwa katika historia ya klabu. Klabu ilikuwa na sanamu kubwa, kama Cruyff, lakini labda ndiye mkuu kuliko wote.

“Hakika atacheza mechi ya kuagwa lakini itakuwa lini, FC Barcelona, hatujui. Atacheza, na tunatumaini atacheza kwa miaka zaidi, kwa sababu watu wanaopenda soka, wale wanaopenda, watafurahi kumuona akiwa na furaha.”

FC Barcelona wanatarajia kurudi kwenye uwanja wao wa Camp Nou Novemba 2024 baada ya kukamilika kwa ukarabati wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: