Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Equatorial Guinea Watimba 16 Bora Afcon 2021

 122920105 Mediaitem122920104 Equatorial Guinea wakishangilia goli lao la ushindi

Fri, 21 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Equatorial Guinea imefuzu kucheza hatua ya 16 bora ya mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2021 baada ya kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Sierra Leone mchezo uliopigwa Januari 20.

Bao pekee kwenye mechi hiyo ambalo lilileta utofauti wa timu hizo ni la Pablo Ganet kunako dakika ya 38 ya mchezo ikiwa ni dakika takribani saba kabla ya mapumziko.

Mwenye bahati habahatishi, katika hali isiyokuwa ya kawaida, Sierra Leone walikuwa wanahitaji ushindi au sare pekee kufuzu lakini hata fursa ya penati iliyopatikana na Kupigwa na mshambuliaji mkongwe Kei Kamara iliokolewa na mlinda mlango Jesus Owono.

Kufuatia matokeo hayo Equatorial Guinea wamemaliza nafasi ya pili nyuma ya vinara Ivory Coast katika Kundi E.

Equatorial Guinea watacheza na atakayemaliza nafasi ya kwanza katika Kundi F, anaweza kuwa Gambia, Mali au Tunisia Jumatano Januari 26.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: