Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dabo awavaa Mastaa Azam FC, awapa onyo hili..!

Fei Toto 9 Goals Kiungo wa Yanga, Feisal Salum "Fei Toto"

Tue, 27 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Azam, Yousuph Dabo amekiri wachezaji wake hawafanyi vizuri kwenye michezo ya hivi karibuni akiwataka kubadilika, huku akiwatupia kijembe mashabiki wanaozipa nafasi Yanga na Simba kwenye mbio za ubingwa.

Azam haijawa na matokeo mazuri tofauti na ilivyoanza msimu, kwani kati ya michezo minne ya hivi karibuni, imeambulia sare tatu na kushinda mchezo mmoja ikibaki nafasi ya pili kwa pointi 37 baada ya michezo 17.

Katika michezo hiyo ya Ligi Kuu, imepata sare ya 1-1 dhidi ya Simba, ikashinda 2-1 kwa Geita Gold, suluhu mbele ya Tabora United na 1-1 dhidi ya Tanzania Prisons.

Katika mechi hizo matajiri hao wameruhusu mabao ya kufungwa matatu, wakifunga manne idadi ambayo ni ndogo kulinganisha na ubora na uwezo wa kikosi hicho ndani na nje ya uwanja.

Dabo alisema matokeo hayo hayakuwa katika hesabu zao, lakini wachezaji hawajaonyesha kiwango na sasa wanakwenda kujipanga tena kurekebisha makosa eneo la ushambuliaji na ulinzi.

Kuhusu vita ya ubingwa msimu huu, kocha huyo alisema wanaozipa nafasi timu za Yanga na Simba wasubiri muda kwani raundi ya pili ndio kwanza imeanza na lolote linaweza kutokea.

“Ni kweli kiwango hakijawa bora wachezaji wanakosa umakini kushindwa kutumia nafasi kufunga lakini wanaruhusu mabao, tunakwenda kulifanyia kazi ili mchezo ujao na Singida FG tufanye vizuri.

“Kuna ambao wameshaamua kuupeleka ubingwa wanakotaka, hawajui bado ligi haijaisha na ndio kwanza raundi ya pili imeanza, Azam hatujajitoa kwenye mbio hizo na tunaamini tutapambana,” alisema kocha huyo raia wa Senegal.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: