Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi mpya tena, Sabaya afikishwa Moshi

Sabaya Mko.jpeg Sabaya kesi mpya tena Moshi

Wed, 1 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa Mkuu Wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya Alfajiri ya leo Jumatano, Juni Mosi, 2022, amefikishwa Moshi mkoani Kilimanjaro akitokea Arusha kwa ajili ya kufunguliwa kesi nyingine mpya.

Sabaya amesafirishwa akitokea Gereza Kuu la Kisongo jijini Arusha kwa kuwa yupo mahabusu kutokana na kukabiliwa na mashtaka mengine ya uhujumu uchumi yasiyokuwa na dhamana.

Ikumbukwe kuwa siku ya jana, Mei 31, 2022 Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha iliahirisha hukumu ya kesi ya Uhujumu uchumi inayomkabili Sabaya na wenzake sita hadi, Juni 10, 2022.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: