Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Covid-19 yaitafuna Comoro ikijiandaa kuwavaa Cameroon hatua ya 16 Bora

 122945197 Whatsubject Golikipa namba 1, Salim Ben Boina ni majeruhi huku wawili wa Ziada wote wakikitwa na Covid -19

Sun, 23 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wauaji wa Mataifa tawala katika Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2021 Comoros wamepata pigo kwenye eneo la golikipa baada ya walinda mlango wawili fiti kupata dalili za maambukizi ya virusi vya Covid-19 huku mlinda mlango wa kwanza akiwa ni majeruhi.

Comoros wanapata pigo hilo katika wakati ambao wamekamilisha mchakato mgumu wa kufuzu hatua ya 16 bora na watacheza na washindi wa AFCON mara tano Cameroon siku ya Jumatatu Januari 24.

Takribani wachezaji saba, ukijumulisha magolikipa wawili wa akiba (Moyadh Ousseini na Ali Ahamada) wamebainika kuwa na dalili za virusi vya Corona pamoja na kocha wao Amir Abdou.

“Tutajaribu kila linalowezekana kuhakikisha tunapata jibu la kufanya katika hili”, alisema El Hadad Himidi Meneja wa timu hiyo.

Kwa mujibu wa taratibu za Shirikisho la Kandanda barani Afrika CAF. lilisema kuwa mechi itaendelea kuchezwa kama kawaida hata kama hakuna kipa anayetambulika wazi.

“Timu italazimika kucheza mechi yake ili mradi kuwe na wachezaji 11 ambao katika vipimo vya mwisho watakuwa hasi katika maambukizi”.

Comoros walifuzu kucheza 16 bora baada ya kuifunga Ghana bao 3-2 kwenye mechi ya mwisho hatua ya makundi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: