Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Cameroon yamaliza kinara Kundi A

Cameroon Vs Verde Cameroon

Tue, 18 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya taifa ya Cameroon ambao ni wenyeji wa mashindano ya Kombe la Mataifa Bingwa Afrika AFCON 2021 imekamilisha mechi zake za hatua ya makundi Kundi A kwa kukaa kileleni mwa Kundi hilo kufuatia kupata sare ya 1-1 na Cape Verde katika mchezo uliopigwa Jumatatu Januari 17.

Mshambuliaji wa timu hiyo na nahodha Vicent Aboubakar alifunga goli la uongozi kipindi cha kwanza kunako dakika ya 39 ya mchezo kabla ya goli hilo kusawazishwa kipindi cha pili na vijana wa Cape Verde kupitia kwa Garry Rodrigues.

Kukaa kileleni kwa wenyeji hao kuna maanisha kuwa kwenye hatua ya 16 bora kuna uwezekano wa kupangwa na timu moja wapo inayoshika nafasi ya pili kwenye Kundi C, D au E katika mchezo utakaopigwa dimba la Yaounde Jumatatu Januari 24.

Kwa upande wa Cape Verde watasubiri bahati yao kuona kama wanaweza kusonga mbele hatua ya 16 bora kupitia mlango wa best loser baada ya kumaliza nafasi ya tatu wakiwa na alama nne wakitofautiana goli za kufunga na kufungwa na Burkina Faso.

Ethiopia imefungashiwa virago kurudi kwao baada ya kuvuna alama moja katika mechi tatu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: