Timu ya Taifa ya Cameroon jana iliibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Burundi katika mchezo wa mwisho wa kufuzu AFCON 2023 na kukwea kileleni mwa kundi C alama 7 baada ya mechi 4.
CAMEROON 3-0 BURUNDI
⚽ Bryan Mbeumo 46'
⚽ Christopher Wooh 59'
⚽️ Vincent Aboubakar 90'
MSIMAMO KUNDI C
Cameroon alama 7
Namibia alama 5
Burundi alama 4
Cameroon na Namibia wamekamilisha timu 24 zilizofuzu AFCON 2023.
TIMU 24 ZILIZOFUZU AFCON 2023:-
Tanzania
Ivory Coast
Morocco
Algeria
South Africa
Senegal
Burkina Faso
Tunisia
Egypt
Zambia
Equatorial Guinea
Nigeria
Guinea-Bissau
Mali
Cape Verde
Guinea
Angola
Ghana
Mozambique
DR Congo
Mauritania
Gambia
Cameroon
Namibia.
Michuano ya AFCON 2023 inatarajiwa kuanza kutimua vumbi nchini Ivory Coast Januari 2024.
Kundi C lilisaliwa na timu tatu tu baada ya Kenya kuondolewa kutokana Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) kufungiwa na FIFA baada ya Serikali ya Kenya kuingilia masuala ya soka Nchini humo.