Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CEO Simba: Hatutampangia kikosi Benchikha

Benchikha Kajula CEO Simba: Hatutampangia kikosi Benchikha

Tue, 28 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba, Imani Kajula amesema kuwa uongozi wa klabu hiyo hautamuingilia Kocha Mkuu mpya wa timu hiyo, Abdelhak Benchikha kwenye majukumu yake, badala yake wamempa uhuru wa kuamua lolote kwenye kikosi hicho.

Kajula amese hayo leo Jumanne, Novemba 28, 2023 wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano wa kumtambulisha rasmi Kocha Benchikha kuanza kuitumikia klabu hiyo.

“Leo tunatamatisha shauku iliyokuwepo kwa siku kadhaa. Haikuwa jambo rahisi maana lengo letu kama klabu tulitaka mwalimu ambaye atatupeleka mbali. Kumpata mwalimu mzuri ni mchakato mkubwa sana.

“Mwalimu Benchikha atakuwepo kwa mkataba wa misimu miwili. Bodi ya Simba, menejimenti ya Simba imempa mwalimu uhuru wa kufanya kazi. Sisi ni moja ya klabu bora Afrika hatuwezi kufanya kazi kwa kumuingilia kwenye majukumu yake, upande wa ufundi yeye ndiyo bosi na ndiye atafanya maamuzi yote.

“Walimu ambao kocha Benchikha amekuja nao ndio aliochukua nao ubingwa wa Shirikisho Afrika na Super Cup. Kocha Farid amefanya kazi na Benchikha kwa miaka 30 pamoja na kocha Kamal amefanya nae kazi kwa karibu,” amesema Kajula.

Benchikha amesajiliwa na Simba baada ya kuachana na USM ALger akiwa ameshinda Ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika kwa kumtoa Yanga pamoja na ubingwa wa Super league kwa kumfunga Al Ahly.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: