Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CAF yamfutia adhabu Kocha Morocco

Walid Regragui Kocha Wa Timu Ya Taifa Ya Morocco Kocha wa Morocco, Walid Regragui

Sat, 27 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) limemfutia adhabu zote kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Morocco, Walid Regragui mara baada ya kuonekana hana hatia.

Regragui alifungiwa michezo minne pamoja na adhabu ya pili ya kufungiwa miezi 12 kutojihusisha na soka ndani na nje ya bara la Afrika.

Adhabu zote zimefutwa na sasa yupo huru kuendelea na shughuli zake ndani ya timu ya taifa ya Morocco.

Regragui atakuwa kwenye benchi la ufundi wakati Morocco itakapoikabili Afrika Kusini kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora siku ya Jumanne Januari 30, 2024.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: