Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CAF yakataa malalamiko ya Tunisia dhidi ya muda wa mechi

MUDA CAF Benchi la Ufundi la Tunisia wakimlalamikia mwamuzi

Fri, 14 Jan 2022 Chanzo: BBC

Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limetupilia mbali malalamiko yaliyowasilishwa na Shirikisho la Soka la Tunisia (FTF) kuhusu mchezo wao na Mali kumalizika mapema, sekunde 13 kabla ya muda wa mechi kuisha.

Katika taarifa iliyotolewa, CAF ilisema kamati ya maandalizi ya Kombe la Mataifa ya Afrika ilikutana siku ya Alhamisi na kukataa malalamiko hayo lakini haikutoa maelezo zaidi.

CAF pia ilithibitisha matokeo ya mchezo wa Jumatano kama ushindi wa 1-0 dhidi ya Mali, bao ambalo mwamuzi wa Zambia Janny Sikazwe, alisema alipigwa na jua, alipuliza mapema.

Tayari alikuwa amepiga filimbi ya kumaliza muda wa mechi baada ya dakika 85, na kugundua makosa yake hivyo kuendelea na mechi.

Mapema siku ya Alhamisi, afisa wa FTF Hussein Jenaieh alilisisitiza kuwa: "Tutafanya chochote kinachohitajika ili kutetea haki za timu ya taifa. Sisi sio watoto."

Afisa wa habari wa FTF Kais Reguez alikataa kuelezea kwa undani alipoulizwa kuhusu chanzo cha malalamiko ya Tunisia, ambayo alithibitisha.

Mwamuzi wa mchezo huo, Sikazwe, inasemekana alilazimika kwenda hospitali kupata nafuu baada ya mchezo kumalizika, na ndiyo maana afisa wa nne alipewa jukumu la kutaka kuanza tena mchezo kwa dakika 20 baada ya kushindwa.

Wakati Mali walijitokeza, Tunisia hawakutokea, kwani baadhi ya wachezaji wao walikuwa wakipooza miili yao kwa barafu .

"Mwamuzi alipigwa na jua, jambo ambalo liliathiri maamuzi yake katika mchezo," afisa mwamuzi wa CAF Essam Abdul Fattah aliambia vyombo vya habari vya Misri.

"Baada ya mchezo, alihitaji kwenda hospitali kwa sababu hali ya hewa ilikuwa ya joto".

Baada ya sare ya 0-0 ambayo haikutarajiwa dhidi ya Sierra Leone, mabingwa watetezi Algeria walilaumu kuonesha kwao kutokana na joto nchini Cameroon.

Tunisia, mabingwa wa 2004, waliingia dimbani wakijua kwamba timu changa na mahiri ya Mali huenda ikawa washindani wao wakuu kundini.

Wakiwa dakika za mwisho , zikiwa zimesalia dakika tano tu za kumaliza mchezo, walipigwa na butwaa wakati mwamuzi Sikazwe alipopuliza kipyenga.

Mzambia huyo baadaye aliangalia muda wake na kuendelea na mchezo, huku akimtoa mchezaji wa Mali kwa kadi nyekundu, kisha akalipua na saa kuonyesha dakika 89 na sekunde 47.

Katika hali isiyo ya kawaida, mkutano wa waandishi wa habari wa 'baada ya mechi' wa kocha huyo wa Mali ulikatizwa huku ikitangazwa kwamba mchezo huo ungetakiwa kuanza upya kwa dakika tisini, jambo ambalo halikufanyika.

"Walituomba turudi uwanjani, hatukujua - hatukujua kilichokuwa kikiendelea," mlinzi wa Tunisia Bilel Ifa aliwaambia waandishi wa habari.

"Tunatumai mechi itarudiwa. Mwamuzi hakujua kilichokuwa kikiendelea tangu mwanzo wa mchezo."

Kocha msaidizi wa Tunisia alikasirishwa na tukio hilo na uwezekano wa uharibifu wake wa sifa kwa mchezo wa Afrika.

"Kwa bahati mbaya, hatuwezi kuona mambo kama haya katika kiwango hiki cha juu barani Afrika - Soka la Afrika haliwezi kusonga mbele hivi," kocha msaidizi wa Tunisia Jalel Kadri aliwaambia wanahabari.

"Mwamuzi "alitikiswa" leo. Alisita hata kumtazama Video Assistant Referee (VAR), hakujua hata jinsi ya kufika kwenye VAR."

Jinsi malumbano yalivyoibuka

Mwamuzi kutoka Zambia, Sikazwe alirejelea mechi mbili za hatua ya makundi katika Kombe la Dunia la 2018 nchini Urusi na kuchukua jukumu la fainali ya Kombe la Mataifa ya 2017.

Ripoti yake ya kupigwa na jua ingeelezea mengi ya sintofahamu yaliyofuata kutoka dakika ya 85 na kuendelea.

"Hatukuelewa chochote katika dakika ya 85 - tulikuwa katika mshtuko," aliongeza.

"Tulizungumza na afisa wa nne ambaye alisema kulikuwa na kutoelewana kati yake na mwamuzi mkuu ambaye huenda hakumwelewa.

Tulianza tena mechi ili apige filimbi tena dakika ya 89."

"Tulielekea kwa afisa wa nne ambaye alikubali kwamba mchezo bado haujaisha," afisa wa FTF Jenaiah aliwaambia wanahabari.

"Tulilalamika ilikuwa ni mara ya pili mwamuzi kusimamisha mchezo kabla ya wakati wake.

"Ofisa wa nne alisema kwanza mechi itaendelea, lakini alipokuwa akielekea kwa mwamuzi mkuu, mwamuzi huyo alisema 'Hapana, nilipiga filimbi, mchezo umekwisha."

Chanzo: BBC
Related Articles: