Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bundi aendelea kutanda viunga vya Liverpool, walazimishwa sare Anfield

Liveerpool .jpeg Liverpool wamekuwa na matokeo mabovu tangu kuanza kwa msimu

Sun, 2 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Majogoo wa Jiji, tmu ya Liverpool wamelazimishwa sare ya 3-3 na Brighton & Hove Albion katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Anfield.

Mabao ya Liverpool yamefungwa na Roberto Firmino mawili dakika ya 33 na 54 na Adam Webster aliyejifunga dakika ya 63, wakati ya Brighton yote yamefungwa na Leandro Trossard dakika ya nne, 17 na 83.

Kwa matokeo hayo, Liverpool inafikisha pointi 10 katika nafasi ya tisa, wakati Brighton imetimiza pointi 14 nafasi ya nne baada ya wote kucheza mechi saba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: