Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Musoma: Intaneti yachelewesha zoezi la Sensa

Internetvjk Pic Musoma: Intaneti yachelewesha zoezi la Sensa

Thu, 25 Aug 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Kutokana na ukosefu wa mtandao wa intaneti katika baadhi ya maeneo kwenye halmashauri ya wilaya ya Musoma vijijini mkoani Mara makarani wa sensa wanalazimika kuchukua taarifa za watu na makazi kisha kuzijaza baadaye wanapokuwa katika eneo lenye mtandao.

Hayo yamesemwa mjini hapa jana Agosti 24, 2022 na mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dk Halfan Haule alipokuwa akizungumza na gazeti hili ofisini kwake juu ya maendeleo ya sense ya watu na makazi katika wilaya yake.

"Kuna baadhi ya maeneo hasa kule vijijini ambapo hakuna mtandao kabisa kwahiyo makarani wanachukua taarifa na kuzitunza wakifika kwenye mtandao wanazituma moja kwa moja NBS," amesema.

Amesema kuwa kutokana na changamoto ya mtandao huo katika baadhi ya maeneo, makarani hao walifundishwa namna ya kufanya wanapokutana na changamoto hiyo hivyo ukosefu huo wa mtandao haujaathiri shughuli hiyo iliyoanza jana nchini kote.

Mkuu huyo wa wilaya pia amewaondoa hofu wakazi wa wilaya hiyo ambao hadi sasa hawajahesabiwa kuwa lazima watahesabiwa kabla ya siku saba za sesna kuisha.

Advertisement Dk Haule ameyasema hayo baada ya baadhi ya wakazi wa awilaya hiyo ambao hawajahesabiwa kulalamika kuachwa bila kuhesabiwa jana.

"Watu wanalalamika wanasema wameachwa bila kuhesabiwa naomba niwaondoe hofu kila mtanzania atahesabiwa, kama karani hakufika kwako jana basi atafika leo au kesho au hata keshokutwa, tuvute subira lazima watanzania wote watahesabiwa tuna siku saba za kuhesabu" amesema

Amesema kuwa amekuwa akipokea simu za malalamiko ambapo watu wamekuwa wakidhani wameachwa bila kuhesabiwa hali ambayo hata hivyo amesema kuwa inaonyesha kuwa muitikio wa wananchi ni mkubwa.

Kuhusu maendeleo ya shughuli hiyo,mkuu huyo wa wilaya amesema kuwa kazi inaendelea vizuri na kwa kasi huku akisema kuwa katika maeneo maalum kama vile kwenye  kambi za wavuvi na maeneo ya machimbo ya madini makarani wamegawanywa kulingana na wingi wa watu katika eneo husika.

"Mfano katika kisiwa cha Rukuba pale tumepeleka makarani saba hivyo tunaamini kazi ya kuhesabu watu pale haitachukua muda mrefu, itafanyika kwa haraka na ufanisi," amesema.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz
Related Articles: