Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Barcelona yamtambulisha Dani Olmo

Daniel Olmo Carvajal (1) Daniel Olmo Carvajal

Fri, 9 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Barcelona ya Hispania imekamilisha usajili wa kiungo mchezeshaji wa RB Leipzig, Daniel Olmo Carvajal mwenye umri wa miaka 26.

Dau la Euro milioni 55 limetosha kumng’oa kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania kutoka Leipzig na kutua Barcelona, klabu ambayo alianzia soka akiwa mdogo.

Olmo anakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Hansi Flick na anajiunga akiwa ametoka kwenye kiwango bora kutoka kwenye michuano ya Euro 2024.

Olmo alikuwa ni mfungaji bora katika michuano ya Euro 2024 iliyofanyika nchini Ujerumani. Anaondoka Leipzig akiwa amecheza michezo 107, kufunga mabao 17 na kutoa pasi za mabao 24.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: