Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Barca ya Xavi vs Guardiola

Xavi Pep Guardiola Barcelona Xavi vs Guardiola

Sat, 1 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika msimu wake wa kwanza mzima ndani ya Barcelona, Xavi Hernandez huenda akafuata nyayo za Pep Guardiola kwa kuiletea timu hiyo taji la La Liga.

Xavi ni zao la La Masia, alijifunza mengi kupitia kwa Guardiola ndani ya miaka minne akicheza chini ya kocha huyo.

Xavi aliwahi kunukuliwa akisema: “Malengo yangu yanaweza kuwa sawa na yake (Guardiola).

“Guardiola alikuwa anataka kuona unaweza kumiliki mpira na kuwa na pilikapilika katika eneo la ushambuliaji na kuona namna ya kuwa bora kwenye eneo la ushambuliaji.

“Nimejifunza vingi kutoka kwa Guardiola aina ya soka alilofundisha, mbinu zake hata uhusiano wake na wachezaji kwa ujumla, tumekuwa tukizungumza mara kadhaa.

“Niwe mkweli, kwangu namuona yeye ndiye kocha bora duniani kwa sasa kama kuna ujuzi nitajifunza kupitia yeye basi kitakuwa kitu kikubwa kwangu.”

Hayo ni maneno ya Xavi kipindi akiwa Al Sadd mwaka 2020 wakati akianza kuinoa timu hiyo ya Uarabuni kabla ya kutua Barcelona Novemba 2021.

Kwa sasa Barcelona imesaliwa na mechi 12 za msimu wa 2022-23 na wao ndiyo vinara wakiwachaa Real Madrid kwa pointi 12.

Wakiwa hapo, Xavi ameendelea kutisha kwani ndani ya msimu mmoja amefanikiwa kuibuka na ushindi mara tatu ndani ya El Clasico, huko nyuma aliyewahi kufanya hivyo ni Guardiola.

Pamoja na hayo yote, Barcelona msimu huu wamezingua ndani ya michuano ya Ulaya pekee kwani waliondolewa Ligi ya Mabingwa Ulaya, walipoangukia Europa League wakafeli tena.

Kwa upande wa La Liga, wameonekana kuwa imara kama ambavyo walikuwa msimu wa 2008-09 chini ya Guardiola wakiwa wamecheza mechi kama hizi za sasa.

Katika msimu wa 2008-09, Guardiola alikuwa akiongoza kwa pointi sita dhidi ya Madrid, wakati huo wastani wa mabao kwa mechi upande wa Barcelona ilikuwa ni matatu, lakini kwa Xavi imekuwa tofauti kidogo, wameruhusu mabao tisa katika mechi 26 za La Liga.

Hizi hapa takwimu za Barcelona katika La Liga msimu huu 2022-23 ukifananisha na ile ya 2008-09 wakiwa katika hatua kama hii.

2022-23 MECHI: 26 POINTI: 68 USHINDI: 22 SARE: 2 KUPOTEZA: 2 MABAO: 49 MABAO KWA MECHI 1.88 MABAO YA KUFUNGWA: 9 MABAOKWA KUFUNGWA KWA MECHI: 0.34 POINTI KWA MECHI 2.61 WASTANI WA USHINDI: 84.6% WASTANI WA KUPOTEZA: 7.6%

2008-09 MECHI: 26 PointI: 63 USHINDI: 20 SARE: 3 KUPOTEZA: 3 MABAO YA KUFUNGWA: 76 BAO KWA MECHI: 2.92 MABAO YA KUFUNGWA: 24 MABAO YA KUFUNGWA KWA MECHI: 0.92 POINTI KWA MECHI: 2.42 WASTANI WA USHINDI: 76.9% WASTANI WA KUPOTEZA: 11.5%

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: