Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bao la Bellingham Euro 2024 lavunja rekodi kibao

Jude Bellingham Goal Euro.jpeg Jude Bellingham

Tue, 18 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kiungo wa England, Jude Bellingham amepiku rekodi za mastaa Cristiano Ronaldo na Michael Owen baada ya kuisaidia timu yake kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Serbia katika mchezo wao wa kwanza kwenye fainali za Euro 2024 huko Ujerumani, uliofanyika juzi Jumapili.

Bellingham ametua kwenye fainali hizo za Euro 2024 akitokea kwenye kiwango bora kabisa cha msimu wake wa kwanza Real Madrid, ambako alishinda La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na Spanish Super Cup. Staa huyo mwenye umri wa miaka 20, hakucheza mechi mbili za kujipima nguvu ambazo England ilicheza na Bosnia-Herzegovina na Iceland, lakini hiyo Jumapili alianzishwa na kocha Gareth Southgate na hivyo kufunga bao pekee kwenye mchezo huo, alipounganisha kwa kichwa krosi ya mpira wa kubabatiza uliopigwa na Bukayo Saka.

Ushindi huo uliifanya England kukusanya pointi zao tatu za kwanza kwenye Kundi C na hivyo kusubiri mechi nyingine kwenye harakati zao za kufukuzia ubingwa huo wa Ulaya. Hata hivyo, kwa Bellingham si tu amefunga bao la ushindi, bali ameliweka pia jina lake kwenye vitabu vya rekodi.

Akiwa na umri wa miaka 20 na siku 353, Bellingham amekuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kucheza kwenye michuano mitatu mikubwa, rekodi ambayo awali ilikuwa ikishikiliwa na staa wa England, Owen (miaka 22 na siku 170).

Bellingham amevunja pia rekodi ya staa wa Ureno, Ronaldo, ambaye alifikia rekodi alikuwa na umri wa miaka 23 na miaka 123.Bellingham ametimiza michuano mitatu mikubwa kwanza alicheza kwenye Euro 2020, ambapo alitokea benchi kwenye mechi tatu za England, kisha kiungo huyo wa zamani wa Borussia Dortmund alicheza kwenye fainali za Kombe la Dunia 2022 na sasa kwenye Euro 2024.

Baada ya kufunga dhidi ya Iran kwenye Kombe la Dunia 2022, bao la kichwa la Bellingham dhidi ya Serbia limemfanya sasa kuwa mchezaji wa kwanza wa kikosi cha Three Lions kufunga kwenye michuano hiyo mikubwa wakati akiwa anachezea klabu za nje ya England.

Staa huyo wa Los Blancos pia amepita kwenye nyayo za magwiji Bobby Charlton, Alan Shearer, Gary Lineker na Bryan Robson na kuwa mchezaji wa tano wa England kufunga bao la kwanza katika michuano mikubwa tofauti. Amefikisha mabao manne.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: