Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Balaa la mpira wa Euro 2024

Fdzfdxgfx Balaa la mpira wa Euro 2024

Fri, 21 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kama kuna kitu kinachovutia zaidi kwenye fainali za Euro 2024 zinazoendelea huko Ujerumani ni aina ya mabao yanayofungwa.

Mashuti yanayotinga nyavuni kupitia kwenye kona za magoli - si kazi rahisi kwa makipa kudaka.

Kuna mabao ya kutosha yanayofungwa kwa mashuti ya kutoka nje ya boksi na kinachoelezwa ni kinachofanya hilo kutokea ni aina ya mpira unaotumika kwenye fainali hizo. Mpira huo umetengenezwa na Adidas.

Morten Hjulmand wa Denmark alifunga kwa shuti la mbali kusawazisha kwenye sare ya 1-1 dhidi ya England na kuhesabu bao la 13 lililofungwa nje ya boksi kwenye fainali hizo za Euro 2024 baada ya mechi 18.

Hiyo ilikuwa kabla ya mechi za usiku wa jana Ijumaa na miongoni mwa michezo ya kibabe kabisa iliyopaswa kufanyika usiku huo wa jana ni baina ya Ufaransa na Uholanzi.

Katika hatua ya makundi ya fainali zilizopita za Euro, ni mabao 12 tu ndiyo yaliyokuwa yamefungwa kwenye umbali wa zaidi ya mita 18.

Sasa kwenye fainali hizi za Euro 2024 za huko Ujerumani, mabao yaliyofungwa huku ikiwa mechi bado kibao za hatua ya makundi, yamepiku mabao ya Euro 2008 na Euro 2012 kwa idadi ya mabao ya mashuti ya mbali.

Kabla ya bao la Hjulmand, wastani wa asilimia 32.4 ya mashuti ya mbali yaliyopigwa kwenye fainali hizo za Euro 2024 yalitinga nyavuni.

Na sababu kubwa inayoelezwa kusababisha hilo ni mpira unaotumika kwenye fainali hizo.

Mpira wa Euro 2024 unaitwa Fussballliebe. Unaelezwa kufanana kabisa na mpira wa Jabulani uliotumika kwenye fainali za Kombe la Dunia 2010, ambao ulikuwa ukiwatesa makipa kutokana na mwendo wake wa kuyumbayumba unapokuwa hewani kwenye upepo.

Lakini, hata kwa fainali za Afrika Kusini, wastani wa mabao ya mbali yalikuwa asilimia 18.6.

Na kwa Adidas kuamua kuupa mpira wa Euro 2024 jina la Fussballiebe ilikuwa na maada kubwa kwa namna ya mabao yanayofungwa, kuanzia shuti la Arda Guler kwenye mechi dhidi ya Georgia au lile la Xherdan Shaqiri alilowafunga Scotland.

Mpira wa Euro 2024 unapenya upepo kuliko kawaida na jambo hilo linawafanya makipa kuwa kwenye wakati mgumu kwelikweli. Kwenye kila tabaka limetengenezwa kwa malighafi zinazotokana na nyuzi za mahindi, miwa, mabaki ya mbao pamoja na mpira. Kuna teknolojia ya hali ya juu imewekwa kwenye mpira huo ili kuupa mwendo mzuri katika kukinzana na upepo.

Straika wa Serbia, Dusan Vlahovic aliuita mpira huo ni wa ajabu, lakini anafurahia kwa sababu ni kama unamsikiliza vile.

Nahodha wa England, straika Harry Kane aliongeza: "Nimeupenda huu mpira. Una kasi sana. Unapopiga shuti, unakuitika.

“Ni kitu kilichonipa uzoefu tofauti kabisa na mipira iliyopo kwenye Bundesliga, mipira ya Adidas inatumika Ulaya na kule nilikotoka, Ligi Kuu England mpira unaotumika ni wa Nike.

"Kwa upande wangu, nadhani mipira hii ni mizuri zaidi kwa washambuliaji na wafungaji kuliko makipa, hivyo siwezi kulalamika."

Adidas ilibainisha mpira huo umetengenezwa kwa ufundi na kuzingatia ushauri kutoka kwa wachezaji.

Ngoja tuone, ni mabao mangapi yatafungwa kwa mashuti ya mbali hadi fainali za Euro 2024 zitakapofika tamati huko Ujerumani.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: