Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baggio avamiwa akiangalia Italia vs Hispania Euro 2024

A4b0bcc35c1b618987c83581dd712a70.jpeg Gwiji wa Italia, Roberto Baggio

Fri, 21 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Gwiji wa Italia, Roberto Baggio amelazimika kuwahishwa hospitalini baada ya kuumizwa vibaya na wezi waliovamia nyumbani kwake wakati akitazama mechi ya Euro 2024 iliyokutanisha Italia na Hispania usiku wa juzi Alhamisi.

Kwa mujibu wa Corriere del Veneto, kundi la watu watano wenye silaha lilivamia nyumbani kwa supastaa huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Italia saa nne usiku. Baggio alijaribu kupigana na mmoja wa wezi hao, lakini wakati akiwa kwenye mapambano hayo, alipigwa na kitako cha bunduki kichwani.

Baggio alibaki na majeraha makubwa kichwani kabla ya kiungo huyo na familia yake kufungiwa ndani. Wezi hao waliondoka nyumbani hapo wakiwa wameiba saa za thamani kubwa, vidani vya thamani na pesa.

Baggio baada ya kuwa na uhakika kwamba wezi hao wameondoka, alivunja mlango na kupiga simu polisi. Na baada ya polisi kufika kwenye eneo hilo, Baggio alipelekwa hospitalini, ambako alikwenda kushonwa nyuzi kadhaa kichwani. Familia yake ilisema kwamba staa huyo alipata mshtuko.

Baggio ametumikia maisha yake yote ya soka akiwa Italia, ambako alicheza kwenye klabu tatu zenye mafanikio makubwa kwenye nchi hiyo Juventus, AC Milan na Inter Milan. Alijiunga na Juventus 1990, alishinda Serie A na Coppa Italia katika msimu wake wa mwisho.

Baada ya miaka mitano Turin, alijiunga na AC Milan, ambako alishinda tena Scudetto. Wakati akiwa Juve, alishinda Ballon d’Or baada ya kuisaidia timu hiyo kushinda Kombe la UEFA, alipofunga mara mbili kwenye mechi ya kwanza ya fainali dhidi ya Borussia Dortmund.

Mafanikio yake kwenye ngazi ya klabu hakuweza kufanya hivyo kwenye soka la kimataifa, licha ya kwamba alikuwa Mtaliano wa kwanza kufunga kwenye fainali tatu tofauti za Kombe la Dunia. Baggio aliongoza Azzurri kucheza fainali kwenye Kombe la Dunia 1994, ambapo Italia ilipoteza kwa mikwaju ya penalti mbele ya Brazil. Brazil ilishinda kwa penalti 3-2 baada ya kupigwa mikwaju tisa, huku Baggio alikosa penalti.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: