Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#BREAKING: Simba wampa "Thank You" Pa Omar Jobe

Video Archive
Tue, 16 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Klabu ya Simba umefikia makubaliano ya kuvunja mkataba na mshambuliaji Pa Omar Jobe (25) baada ya kuitumikia kipindi kifupi cha miezi sita.

Jobe ambaye ni raia wa Gambi alijiunga na Simba wakati wa dirisha dogo la usajili, Januari 15, 2024 akitokea katika timu ya Zhenis inayoshiriki Ligi Kuu nchini Kazakhstan akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake.

Jobe amefanikiwa kuifungia Simba mabao matatu tu kwenye mashindano yote ikiwa ni bao moja Ligi Kuu ya NBC dhidi ya tabora United, bao moja Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Jwaneng galaxy na bao moja kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho la CRDB dhidi ya Tembo FC.

Jobe na BabaCar ndio nyota wawili wa Simba SC wa kimataifa ambao hawakutumiwa tiketi ya kuwasili Nchini tayari ya kujiandaa na msimu mpya wa mashindano.

Umeipokeaje "Thank you" ya Jobe?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: