Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ateba aandaliwa kuwamaliza Fountain Gate FC

Lionel Ateba Kimeeleweka Simba SC,  Kuwavaa Singida Big Stars.png Ateba aandaliwa kuwamaliza Fountain Gate FC

Tue, 20 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji mpya wa Simba, Leonel Ateba sasa ruska kuitumikia klabu hiyo katika michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kukamilika vibali vya kazi pamoja na ITC yake kuwasili.

Nyota huyo huenda akawa sehemu ya kikosi cha Simba katika mchezo ujao dhidi ya Fountain Gate FC utakaochezwa Jumapili, Agosti 25, 2024, uwanja wa KMC, uliopo Mwenge, Dar es Salaam.

Usajili wa Ateba ni baada kocha mkuu wa Simba Fadlu Davids kuutaka uongozi wa timu hiyo kuongeza mshambuliaji na kuchukuwa nafasi ya Freddy Michael ambaye tayari amepewa THANK YOU.

Meneja wa idara ya habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema wamekamilisha taratibu zote za vibali vya mshambuliaji wao Ateba na sasa rasmi kucheza mechi.

Amesema mechi ya Tabora United alishindwa kucheza baada ya vibali vyake kutokamilika ikiwemo ITC kutoka klabu USM Alger.

“Tumekamilisha taratibu zote za vibali, Ateba sasa ruksa kucheza ligi, hata tukipangiwa mechi leo mshambuliaji huyo yupo tayari kucheza, ni mipango ya kocha Fadlu tu kumtumia,” amesema Ahmed.

Ameongeza kuwa timu hiyo inaendelea na maandalizi, pamoja na kushinda dhidi ya Tabora United, wanahitaji kuwapa muda zaidi wachezaji wao waendelee kutafuta ubora wao

“Tumesajili Wachezaji bora sana wamefanya makubwa walikotoka, katika hao Wapo walioanzia juu moja kwa moja na wengine wameanzia chini, iko hivyo duniani kote hasa Mchezaji anapotoka timu ndogo kwenda kubwa au kutoka ligi ndogo kwenda kubwa au anapoenda kwenye timu yenye presha kubwa kama yetu.

Ni jukumu letu kuwavumilia, kuwatia moyo, kusimama nao nyakati zote ili warejeshe kujiamini na kuupata ubora wao,aina ya Wachezaji tuliokua nao nusu yao wakiupata ubora wao basi Mwaka huu utakua Msimu mzuri kwetu,” amesema Ahmed.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: