Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Asitafutwe mchawi Taifa Stars kwa unyonge Morocco

Kikao Cha Taifa Stars Asitafutwe mchawi Taifa Stars kwa unyonge Morocco

Fri, 19 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taifa Stars haijaanza vyema fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) zinazoendelea mwaka huu huko Ivory Coast baada ya kupoteza mechi ya kwanza dhidi ya Morocco kwa mabao 3-0, matokeo yaliyoifanya ianze kwa kushika mkia kwenye kundi F.

Hicho ni kipigo cha pili mfululizo ambacho Taifa Stars imekipata kutoka kwa Morocco katika mechi mbili ambazo timu hizo zimekutana ndani ya muda usiozidi miezi miwili kwani kabla ya hapo timu hizo zilikutana katika mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia, Novemba 21 mwaka jana ambao Tanzania ilifungwa mabao 2-0.

Kabla ya mechi ya juzi Jumatano, baadhi ya Watanzania walikuwa na matumaini kwamba huenda safari hii Taifa Stars ingeondoka na pointi dhidi ya Morocco iwe kwa kupata ushindi au kutoka sare au hata ikipoteza iwe sio kwa idadi kubwa ya mabao lakini mambo yamekuwa tofauti.

Baada ya matokeo hayo kumeanza kuibuka lawama ambazo zinaelekezwa kwa baadhi ya watu kwamba ndio wamechangia Taifa Stars ianze kwa kupoteza.

Kuna ambao wameamua kumshutumu kocha wa Taifa Stars, Adel Amrouche kuwa kikosi alichokipanga na mbinu zake ziliipa urahisi Morocco hadi ikaweza kupata ushindi huo na kuna wanaolaumu baadhi ya wachezaji kuwa hawakucheza vizuri.

Pia kuna wanaoelekeza lawama kwa refa wa mchezo kuwa aliinyonga Taifa Stars mara kwa mara na kuipendelea Morocco katika mchezo huo hasa wakitumia tukio la Novatus Miroshi kuonyeshwa kadi nyekundu katika kipindi cha pili cha mchezo.

Hata hivyo, kiukweli hatupaswi kumuangushia mtu yeyote lawama kutokana na matokeo hayo kwani tunarudi palepale kwenye uhalisia kuwa Morocco wametuacha mbali kisoka na sisi tulikuwa na nafasi finyu ya kupata ushindi au hata pointi dhidi yao.

Ubora wa wachezaji wa Morocco ulitulazimisha tufanye makosa ambayo waliyatumia kutuadhibu kwa mabao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: