Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Angola kuishangaza Afrika AFCON 2023

Kocha Mkuu Wa Angola, Pedro Goncalves.png Kocha Mkuu wa Angola, Pedro Goncalves

Wed, 17 Jan 2024 Chanzo: Dar24

Kocha Mkuu wa Angola, Pedro Goncalves amefurahishwa na kikosi chake kuwa na hali ya kupambana katika kipindi cha pili na kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya washindi wa mwaka 2019, Algeria katika mchezo wa Kundi D wa Kombe la Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2023’.

Algeria ilidhihirisha ubabe wake dakika 18 tangu kuanza kwa mchezo wakati Baghdad Bounedjah alipoiwezesha timu hiyo kuwa mbele, lakini Angola hawakutetereka na walibaki katika njia na kufanikiwa kupata Penati.

“Tulianza mchezo taratibu lakini tulifanikiwa kupata baadhi ya nafasi na kurudi mchezoni katika kipindi cha pili ambacho timu yetu ilifanya vizuri,” alisema Goncalves.

“Kazi bado haijafanyika. Timu ilionesha iko vizuri na tutaendelea kuijenga timu katika mechi zijazo.”

Goncalves alikuwa akielezea kuhusu timu yake kutaka kuweka historia, na kushuhudia ikitinga Robo Fainali.

“Acha tufanye kile ambacho bado hatujawahi kukifanya kabla, hilo ndilo lengo letu kubwa. Tunajua kama tukishinda mara mbili, tutafuzu,” alisema.

Tutaona utendaji na uwezo wetu utatufikisha wapi, lakini naamini tunaweza kufuzu kutoka kwenye Kundi na kujaribu kushinda hatua ya mtoano”.

Mchezo ujao Angola itacheza dhidi ya Mauritania Jumamosi (Januari 20).

Naye kocha wa Algeria, Djamel Belmadi alisema baada ya mchezo huo kuwa kikosi chake kilishindwa kuusoma mchezo na kupata matokeo.

“Haya sio matokeo tuliyoyatarajia. Tulitarajia kuondoka na pointi tatu,” alisema kocha huyo.

Chanzo: Dar24
Related Articles: