Kocha mkuu wa Real Madrid, Carlo Ancelotti ana imani kuwa Real Madrid wana uwezo wa kupindua kichapo cha 1-0 cha mchezo wa mkondo wa kwanza wa nusu fainali ya Copa del Rey dhidi ya timu ya Barcelona siku ya Alhamisi.
Barca walipata ushindi wa bao 1-0 Santiago Bernabeu hapo na kuchukua faida ya uongozi katika mchezo wa marudiano wa mwezi ujao huko Camp Nou. Bao hilo la ushindi lilipatikana dakika ya 26 kwa bao la kujifunga la mlinzi Eder Militao.
Ancelotti hakufurahishwa na uchezaji wa Barca na anasalia na imani kwamba Madrid itatinga fainali, licha ya Los Blancos kushindwa kupata hata shuti moja lililolenga lango kwa mara ya tatu pekee katika muongo mmoja.
Kocha huyo aliwaambia waandishi wa habari kuwa; “Timu ilicheza vizuri, na Barcelona walicheza kama hawakutaka kucheza. Hatujawa wazuri. Kushindwa kunauma, lakini tukifanya vivyo hivyo katika mkondo wa pili, tuna nafasi ya kusonga mbele.”
Carlo aliongeza kuwa wameshindwa lakini hatukustahili kupoteza na akakazia kuwa ndani ya dakika 90 wanaweza kuifunga bao Barcelona, licha ya kuchanganyikiwa kwa sauti yake, kocha huyo Mhispania bila shaka alifurahishwa na jinsi Madrid walivyoweza kudhibiti sehemu kubwa ya mchezo, na kuwalazimisha Barca kucheza zaidi kwenye eneo lao lao.
Barcelona wana faida, lakini wana imani yote kuweza kugeuza matokeo hayo. “Mechi ya mkondo wa pili itachezwa huko Camp Nou mnamo Aprili 5.