Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Anaetajwa mrithi wa Kajula, awakana Simba SC

CEO Simbaaaaa 111 François Regis Uwayezu

Tue, 16 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

François Regis Uwayezu aliyekuwa Makamu Rais wa timu ya APRF FC ya Rwanda, amekanusha taarifa za kumalizana na Simba SC kuchukua mikoba ya Imani Kajula ambaye anaondoka katika nafasi ya Mtendaji Mkuu ndani ya klabu hiyo.

Régis ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la soka nchini Rwanda (FERWAFA), amekanusha kufanya mawasiliano na Simba SC kwa ajili ya kuhudumu katika nafasi hiyo iliyo.

Bodi ya Wakurugenzi ya klabu ya Simba ilikubali ombi la Afisa Mtendaji wake mkuu wa klabu hiyo Imani Kajula la kuomba kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa mwezi wa ujao pindi mkataba wake utakapotamatika.

Kajula aliingia Simba mnamo Januari 2023 na kusaini kandarasi ya miezi 6 uliyokuwa na kipengele cha kuongeza muda,akirithi mikoba ya Barbara Gonzalez aliyeondoka ndani ya Simba SC kipindi hicho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: