Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyekosa penalti Morocco aomba radhi

Hakimi Sorry Aliyekosa penalti Morocco aomba radhi

Wed, 31 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Beki wa kulia wa timu ya taifa ya Morocco anayekipiga PSG, Ashraf Hakimi amewaomba radhi mashabiki wa timu hiyo baada ya timu hiyo kutolewa kwenye fainali za Afcon 2023, hatua ya 16 Bora.

Hakimi aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram, anawaomba radhi mashabiki wa soka wa Morocco kwa kushindwa kuifanya timu yao kufuzu robo fainali ya michuano hiyo, "Naomba radhi kwa kukosa pelnati, nilichukua majukumu ya kusaidi timu lakini bahati mbaya sikuweza, hayakuwa makusudi yangu, niwashukuru mashabiki wote hasa waliosafiri hadi Ivory Coast, Mungu akipenda tutarudi na nguvu zaidi."

Aidha Hakimi amewatakia kheri timu ya Afrika Kusini (Bafana Bafana) katika fainali hizo, licha ya kuwa ndio timu iliyowatoa wao.

Morocco ilishindwa kufuzu baada ya kufungwa mabao 2-0 na Afrika Kusini yaliyowekwa kimiani na Evidence Makgopa dakika ya 57 na Teboho Mokoena akipiga msumari wa mwisho dakika 90+5 huku ikishuhudiwa nyota wa Manchester United, Sofyan Amrabat akionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 94+4.

Morocco iliyoonyesha kiwango bora kuanzia hatua ya makundi, ikiwa kundi moja pamoja na Tanzania, Congo na Zambia, iliduwazwa kwa bao hilo huku Hakimi akikosa penalti hiyo iliyowagharimu kukosa nafasi ya kufuzu.

Kwa ushindi huo, Afrika Kusini itakutana na Cape Verde kwenye robo fainali ya fainali hizo zinazoendelea kushika kasi Ivory Coast.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: