Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alaba ana kazi spesho Austria Euro 2024

Alaba Austria Alaba ana kazi spesho Austria Euro 2024

Fri, 21 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Staa, David Alaba yupo kwenye fainali za Euro 2024 akiwa na kikosi cha taifa lake la Austria, lakini huwezi kumwona ndani ya nyasi za viwanja hivyo vya Ujerumani akionyesha mavitu yake.

Staa huyo wa Real Madrid ndiye nahodha wa Austria na mchezaji bora wa timu hiyo, lakini hachezi fainali hizo za Ujerumani.

Hata hivyo, Alaba bado yupo kwenye kikosi hicho akijaribu kuwapa nguvu wachezaji wenzake katika kupambana kupenya kutoka katika kundi gumu kabisa la fainali za Euro 2024, ambapo wamepangwa pamoja na Ufaransa, Uholanzi na Poland.

Kinachoelezwa ni kwamba Alaba yupo kwenye kikosi cha Austria kwa kazi maalumu. Alaba hachezi kwenye Euro 2024 kwa sababu ni majeruhi.

Hajacheza mechi tangu Desemba 17 mwaka jana baada ya kuumia mguu katika mechi ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Villarreal, ambapo ni miezi saba hiyo iliyopita. Katika mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Alaba alikuwa kwenye benchi la Real Madrid, lakini hakuwa kwenye orodha ya wachezaji ambao wangecheza mechi hiyo dhidi ya Borussia Dortmund.

Kiraka huyo mwenye umri wa miaka 31 bado hayupo fiti kuitumikia Austria, lakini kocha Ralf Rangnick amechagua kumjumuisha kwenye timu yake na kumpa kazi maalumu.

Akizungumzia hilo, kocha Rangnick alisema: “Ni kitu kinachohuzunisha kwamba hayupo nasi kama mchezaji. Kwa wiki kadhaa sasa nimekuwa nikifanya kazi kwa karibu na David kwa ajili ya kubadilishana ujuzi. Yupo kwenye timu hii akifanya kazi nyingine nje ya uwanjani kama mchezaji.”

Austria ilicheza mechi yake ya kwanza ya Euro 2024 dhidi ya Ufaransa na kupoteza mchezo huo kwa bao la kujifunga na usiku wa jana Ijumaa, ilikuwa na kazi ya kukabiliana na Poland ilipokuwa ikisaka pointi zake tatu za kwanza kwenye fainali hizo.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: