Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahmed Ally: Mashabiki tuwe wavumilivu

Simba Ahmed Mashabiki Ahmed Ally: Mashabiki tuwe wavumilivu

Wed, 14 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally ametaka Wanasimba kuwa wavumilivu na kumuamini kocha wa kikosi hicho Fadlu Davids.

Ahmed ameandika katika ukurasa wake wa Instagram kuw Simba SC imefanya usajili mzuri kuliko misimu mitatu iliyopita, hivyo Wanasimba wanatakiwa kuwa watulivu.

“Tumesajili timu bora ndani ya msimu huu. Lakini ni ngumu kuliona hili kwa sababu mashabiki wa Simba tunatazama mpira kwa presha.

“Presha ya kukosa Mataji misimu mitatu inatunyima uhuru wa kuangalia mpira kwa jicho la utulivu ndio maana ligi haijaanza lakini tumeanza kuona baadhi ya wachezaji hawafai kwa sasa Wanasimba tunahitaji ushindi tu na tunahitaji kila mtu afunge hii yote ni presha ya mataji,” ameandika Ahmed.

Ahmed aliendelea kuandika kuwa; “Ombi langu kwenu wana Familia ya Simba, Tuwe na subira na wavumilivu, tumpe uhuru Mwalimu na tuwape nafasi wachezaji wetu kuonesha uwezo wao,” aliongeza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: