Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#AFCON2023: Ulaya itahamia Afrika, fursa kwa wazawa

Rais Samia Atoa Mil. 500 Taifa Stars Kufuzu AFCON.jpeg #AFCON2023: Ulaya itahamia Afrika, fursa kwa wazawa

Thu, 5 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtangazaji wa EATV na EA Radio, Albogast Myaluko amesema kuwa Bara la Afrika litajaa wataalam wa soka kutoka Barani Ulaya wakati wa michuano ya AFCOn inayotarajiwa kufanyika nchini Januari, 2024 nchini Ivory Coast.

Tanzania ni miongoni mwa mataifa 24 yaliyofuzu michuano hiyo, hivyo endapo wachezaji wazawa wa Tanzania wataitumia fursa hiyo vizuri inaweza kuwa ni daraja kwao kwenda kucheza Ulaya na kutimiza ndoto zao.

"AFCON ni mashindano ambayo yanahusisha wachezaji wanaotoka kwenye ligi kubwa barani ulaya, maana yake macho mengi yanakuwepo kwenye hii michuano.

"Ma-scout wakubwa duniani achana na wanaowakilisha klabu, wale ambao wenye academy tu ulaya wanataka kuja kuchukua vipaji wakafanye biashara baada ya miaka mitatu nao watakuja hapa, maana yake nini?

"Maana yake utaingiza fedha za kigeni za kutosha, lakini pia utatengeneza mahusiano mazuri baada ya michuano kunaweza kukawa na uwekezaji enedelevu kutokana na kile kimeonekana kwenye mashindano," amesema Albogast.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: