Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#AFCON2021: Nigeria Watupwa Nje, Tunisia Yatinga Robo Fainali

Nigeria Tunisia.jpeg #AFCON2021: Nigeria Watupwa Nje, Tunisia Yatinga Robo Fainali

Sun, 23 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Licha ya kuwa bora kwenye hatua ya makundi na kumaliza wakiongoza kundi lao kwa pointi 9 bila kupoteza mchezo, Timu ya Taifa ya Nigeria imeambulia kichapo cha bao 1-0 kutoka wa Tunisia na kuondoshwa katika michuano ya Afcon2021.

Bao pekee la Tunisia limefungwa na Youssef Msakni dakika ya 47 na kuwapeleka robo fainali ya michuano hiyo huku Alex Iwobi wa Nigeria akilamba kadi nyekundu dakika chache tu baada ya kuingia akitokea benchi.

Tunisia katika hatua ya robo fainali watakutana na Burkina Faso ambaye amemtungua Gabon kwa penati 7-6 baada ya kutoka sare ya bao 1-1 katika dakika 120. #AFCON2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: