Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AFCON 2023- Kocha Misri aendelea kushambuliwa

Kocha Wa Misri AFCON AFCON 2023- Kocha Misri aendelea kushambuliwa

Thu, 1 Feb 2024 Chanzo: Dar24

Maoni yameendelea kutolewa nchini Misri, baada ya Timu ya Taifa ya nchi hiyo kutokewa mapema katika Fainali za Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2023’ zinazoendelea nchini Ivory Coast.

Viongozi wa Shirikisho la Soka nchini Misri ‘EFA’ pamoja na Kocha Mkuu wa ‘The Pharaohs’ Rui Vitoria, wanaendelea kukosolewa vikali, huku wakitajwa kama sababu kuu ya Taifa hilo kushindfwa kufurukuta katika Fainali za ‘AFCON 2023’.

Kiungo wa zamani wa Klabu Bingwa nchini Misri Al Ahly Ahmed Abou-Moslem amekosoa maamuzi ya Shirikisho la Soka nchini humo ‘EFA’ ya kumuajiri Rui Vitoria kama Kocha Mkuu wa ‘The Pharaohs’.

Timu ya Taifa ya Misri ilitupwa nje ya Fainali za ‘AFCON 2023’ Jumapili (JAnuari 28), kwa kufungwa na DR Congo kwa changamoto ya Mikwaju ya Penati, katika hatua ya 16 bora.

‘The Pharaohs’ walikuwa na kampeni mbaya zaidi katika Fainali za ‘AFCON 2023’ baada ya kuambulia sare tatu mfululizo za 2-2 katika hatua ya makundi dhidi ya Msumbiji, Ghana, na Cape Verde.

Matokeo hayo yamedhihirisha Misri imeshindwa kuchomoza na ushindi katika Fainali za ‘AFCON 2023’, hali inayodaiwa kuwa imetokana na uwezo mdogo wa Kocha Rui Vitoria.

“Kilichofanywa na Vitoria kilikuwa tusi kwa soka la Misri,” Ahmed Abou-Moslem amesema.

“Hakuna mfumo nchini Misri, hakuna muundo, hakuna mipango ya muda mrefu, na hakuna mawasiliano kati ya timu za vijana.

“Hakuna viwango linapokuja suala la Chama cha Soka cha Misri kuchagua makocha, na hakuna maono. Mkataba wa Vitoria na timu ya taifa ya Misri ni janga na uhalifu, na yeyote aliyefanya makubaliano hayo lazima awajibike.”

“Carlos Queiroz (kocha mkuu wa zamani) alikuwa akipata Euro 100,000 akiwa na Misri, na alipotuacha na kuchukua jukumu la kuinoa Iran, alikuwa akipata 30,000. Kwa hivyo, pesa hizi zilienda wapi?”

“Kulipaswa kuwa na kipengele kinachoruhusu EFA kusitisha mkataba wa Vitoria endapo atashindwa kushinda AFCON. Mradi wa ‘Vitoria’ uko wapi? Hatujaona sura mpya kwenye timu, tofauti na Queiroz, ambaye aliunganisha wachezaji kama Omar Kamal, Mohamed Abdelmonem na wengine,” ameongeza.

Chanzo: Dar24
Related Articles: