Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mvua yachelewesha Makarani wa Sensa Dar

Mvua Makarani Mvua yachelewesha Makarani wa Sensa Dar

Tue, 23 Aug 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Mvua iliyoanza kunyesha asubuhi ya leo Jumanne, Agosti 23, 2022 imechangia kuchelewa kwa makarani wa sensa katika baadhi ya mitaa jimbo la Mbagala.  

Kama ambavyo ilitangazwa, sensa itaanza asubuhi ya Agosti 23, 2022  wakazi wa kata ya Toangoma waliokuwa wamejiandaa kuhesabiwa wamejikuta wakisubiri kwa muda kabla ya kuanza kutembelewa na makarani.

Ester Mangachi amesema aliamka mapema akisubiri karani apite ila hadi saa 2:40 asubuhi bado hajahesabiwa.

“Nilikuwa nataka wanikute mwenyewe ila naona mvua imeleta changamoto kidogo, sasa mie wacha nikatafute riziki kwanza, watawakuta wengine maana taarifa zote nimeacha,” amesema Ester.

Akizungumzia hali hiyo, msimamizi wa makarani, mtaa wa Mzinga B, Onesmo Bundi amesema changamoto ya kuchelewa iliyojitokeza imetokana na mvua.

“Tumeona leo kumekucha na mvua ndio maana kuna sehemu makarani wamechelewa kufika ila kazi inaendelea na tunapata ushirikiano mzuri kutoka kwa wakuu

“Nimeshazungumza na makarani wangu kubeba miamvuli maana hatujui hali itakuwaje kwa kutwa nzima, hatutaki sisi kuwa kikwazo lazima kazi ifanyike,” amesema Bundi.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz
Related Articles: