Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makarani 10, 000 wa sensa watawanyika mitaani Mwanza

Sensa Maswali 12 Makarani 10, 000 wa sensa watawanyika mitaani Mwanza

Mon, 22 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Sensa ya Watu na Makazi ikitarajiwa kufanyika kesho Agosti 23, Mkoa wa Mwanza umekamilisha maandalizi yote muhimu huku makarani wa sensa wkitumia siku ya jana na leo kuhakiki maeneo na mitaa watakayopita.

Akizungumza leo Jumatatu Agosti 22, Mratibu wa Sensa mkoa wa Mwanza, Goodlucky Lyimo amesema jumla ya makarani 10, 060 watakaofanya kazi hiyo tayari wamekabidhiwa vifaa na wanendelea na uhakiki katika maeneo yao ya kazi.

"Makarani wote wametawanyika kuhakiki maeneo yao ya kazi. Tunaomba ushirikiano kutoka kwa wananchi kukamilisha shughuli hii muhimu kwa maendeleo ya Taifa,” amesema Lyimo

Afisa Mtendaji wa Kata ya Luchelele jijini Mwanza, Fredrick Kitwala amesema mikutano ya kuhamasisha wananchi kushiriki imefanyika katika mitaa yote sita ya kata hiyo ya Nganza, Ihumilo, Luchelele Ziwani, Kasamiko, Shadi na Nyakalekwa, na kinachosubiriwa ni kukamilisha kazi hiyo muhimu.

"Hata leo tutakuwa na vikao vya kuhamasisha wananchi kuhusu umuhimu wa sensa kwa maendeleo ya Taifa,” amesema Kitwala

Mkazi wa Mtaa wa Kasamiko kata ya Luchelele jijini Mwanza, Fred Mabangala ameiambia Mwananchi kuwa tayari makarani wa sensa wamepita mtaa huo kutoa elimu na kupata taarifa ya awali za kaya mbalimbali.

Advertisement "Kuna watu wamepita hapa nyumbani kwangu wakiniuliza baadhi ya taarifa kuhusu familia yangu wakiwa na vifaa kama simu na vitabu. Mimi niko tayari kuhesabiwa," amesema Mabangala

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe, Joshua Manumbu amewahimiza kujitokeza kuhesabiwa katika Sensa ya Watu na Makazi kuwezesha Serikali kujua idadi na mahitaji yao kibajeti.

“Wilaya ya Ukerewe ina visiwa 38, kati ya hivyo, visiwa 34 ni vya makazi ambako kunahitajika huduma za kijamii; ni muhimu wakazi wake kushiriki sensa ili idadi na mahitaji yao yafahamike kwa Serikaki,” alisema Manumbu

Aliwasihi wananchi wa kisiwa hicho kutoa taarifa na takwimu sahihi ikiwemo idadi ya watu wenye elemavu wanaohitaji huduma maalum.

“Kutokana na mazingira na shughuli za wakazi wa visiwa vya Ukerewe ambao wengi ni wavuvi, uamuzi wa Serikali wa kutangaza Agosti 23 kuwa siku ya mapumziko itawezesha wengi kushiriki. Nawasihi wavuvi na wafanyabishara wote walioko visiwani washiriki sensa,” alisema Manumbu

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: