Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dodoma yazindua Sensa kwa kufyatua baruti, kukata keki

Moto Fataki Dodoma yazindua Sensa kwa kufyatua baruti, kukata keki

Tue, 23 Aug 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule ameongoza shughuli ya kuzindua Sensa ya Watu na Makazi leo Jumanne, Agosti 23,2022 mkoani hapa kwa kulipua baruti na kukata keki.

Na mara baada ya kukata keki na kufyatua baruti iliyofanyika Wilaya ya Mpwapwa, viongozi mbalimbali alioambatana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, wakala keki kisha uwanja mzima ukatulia kusikiliza ujumbe wa Mkuu huyo wa Mkoa.

Aidha Senyamule ametumia fursa hiyo kuwaasa mamia ya waliojitokeza kwenye eneo hilo ambapo pia umelala Mwenge wa Uhuru kutoa ushirikiano kwa makarani wa Sensa.

Aidha makarani hao wa Sensa walionekana wakiwa wameshikilia Vishikwambi vyao huku wakiwa wamevaa makoti mng'ao (Reflctor) wakiwa tayari kwa kazi hiyo ya Sensa lililoanza Saa 6 usiku wa Agosti 23, 2022.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz
Related Articles: