Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC aahidi kulinda siri za wanaume wa kimasai katika sensa

Dccc Pic Data DC aahidi kulinda siri za wanaume wa kimasai katika sensa

Tue, 23 Aug 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Frank Mwaisumbe amewataka wanaume wa jamii ya Kimasai kutoa taarifa sahihi za idadi ya wake na watoto wao katika sensa huku akiwaahidi maelezo hayo yatakuwa na usiri mkubwa.

Mwaisumbe ameyasema hayo jana Agosti 22 kwenye mkutano wa hadhara wa wananchi wa kata za Esilalei wilayani humo wakati akihamasisha utolewaji wa taarifa sahihi za idadi ya wanakaya katika zoezi la uhesabuji watu ‘sensa’ linalotarajiwa kuanza Agosti 23 kote nchini.

Mwaisumbe amesema kuwa anajua wanaume wa jamii ya kimasai wana desturi ya kuwa na wake wengi na watoto ambao wengine hawafahamiki na familia zao za karibu hivyo kuwataka kutoa taarifa kamili katika zoezi la sensa akiwahakikishia usiri mkubwa wa taarifa zao.

“Taarifa zitakazokuja kuchukuliwa zitakuwa za siri kwa matumizi ya serikali pekee kwa hiyo msiwe na wasiwasi ndugu zangu.

“Wanaume hakikisheni hamtaniangusha, kama una watoto au kuna mke mwingine mahali hakikisha unamsema na tutatunza siri, msifiche fiche mambo mkidhani zitavuja mahali naomba sana isitokee,” amesema Mwaisumbe.

Amewataka viongozi wa ngazi za vijijini na vitongoji kuhakikisha wananchi wenu wana taarifa hizi za sensa na wahamasishe ushirikiano, kwani wasipofanya hivyo wataangusha watendaji wa juu.

Advertisement Naye mwenyekiti wa Baraza la Madiwani halmashauri ya Monduli, Isack Joseph Capriano amesema taarifa sahihi za idadi ya wananchi itawasaidia kutekeleza kwa urahisi miradi ya maendeleo kwa wakati kuzingatia mahitaji halisi.

“Ndugu zangu hakikisheni hamfichi idadi ya wana kaya ili kutusaidia sote kupata bajeti nzuri kutoka serikali kuu ikiwemo hata mikopo kwa makundi mbali mbali ya vijana, wanawake na walemavu,” amesema.

Kwa upande wake katibu wa CCM wilaya ya Monduli, Rukia Mbasha aliwataka wananchi hao kuepuka uzushi na uchonganishi za imani potofu juu ya zoezi hilo hasa kwa watu tegemezi.

“Mtu asikudanganye kumficha ndugu yako aliyelala kwako siku hiyo ambae ni mlemavu au tegemezi kwa aina yoyote, kwani kufanya hivyo kutapunguza hata bajeti zao zinazowastahili, serikali ikidhani wamepungua kumbe mmewaficha,” amesema Mbasha.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz
Related Articles: