Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mawawakili wa utetezi waanza kumhoji Mkaguzi wa Polisi kesi ya kina Mbowe

Mbowepic Data Mawawakili wa utetezi waanza kumhoji Mkaguzi wa Polisi kesi ya kina Mbowe

Mon, 7 Feb 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

hahidi wa 13 wa upande wa Jamhuri katika kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu, amemaliza kutoa ushahidi wake leo Jumatatu Februari 7, 2022 huku upande wa utetezi ukianza kumhoji maswali ya dodoso kuhusu ushahidi alioutoa.

Shahidi huyo ambaye ni Mkaguzi wa Polisi, kutoka Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi, Mkoa wa Kipolisi Temeke, Tumaini Sostenes Swila alianza kutoa ushahidi wake Ijumaa iliyopita katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.

Baada ya kumaliza kutoa ushahidi wake leo, mawakili wa upande wa utetezi walianza kumhoji maswali.

Wakili wa utetezi Nashoni Nkungu anayemtetea mshtakiwa wa kwanza katika kesi hiyo, Halfan Bwire Hassan ndiye aliyeanza kumhoji shahidi akifuatiwa na Wakili John Mallya anayemtetea mshtakiwa wa pili Adam Kasekwa.

Baada ya Wakili Mallya kumaliza kumhoji shahidi, Wakili Fredrick Kihwelu anayemtetea mshtakiwa wa tatu Mohamed Ling'wenya, alitoa hoja ya kuomba kesi hiyo iahirishwe mpaka kesho kutokana na muda wa kazi kuisha.

Baada ya Kihwelu kutoa hoja hiyo, Jaji Joachim Tiganga anayesikiliza kesi hiyo aliuhoji upande wa mashtaka ambapo waliridhia hoja hiyo.

Jaji Tiganga ameahirisha kesi hiyo mpaka kesho Jumanne ambapo mawakili upande wa utetezi utaendelea kumhojo shahidi huyo namba 13 wa upande wa mashtaka.

Fuatilia hapa kilichojiri mahakamani leo…

Tayari Jaji Tiganga ameshaingia katika ukumbi wa Mahakama.

Jaji: Shahidi bado upo chini ya kiapo.

Shahidi huyo anaongozwa na wakili wa Serikali Mwandamizi. Robert Kidando.

Shahidi: Machi 30, 2021 nilipokea taarifa ya uchunguzi wa maandishi kutoka Kitengo cha uchunguzi wa maabara sayansi ya uchunguzi wa maandishi.

Shahidi: Julai 10, 2021 nilipokea ripoti ya simu 8 kutoka inspector Innocent Ndowo kutoka Kitengo cha uchunguzi na Makosa ya Mtandao katika maabara ya Uchunguzi na Sayansi.

Ripoti hiyo nilivichukua kwa kusaini kitabu cha makabidhiano kilichopo katika Kitengo cha uchunguzi wa Makosa ya Mtandao.

Pia niliweza kukapokea simu 8.

Baada ya kupokea simu hizo nilienda kuzihifadhi katika Kituo Kikuu Cha Polisi Dar es Salaam ambapo nilimkabidhi Koplo Charles ambaye ni mtunza vielelezo katoka kituo hicho cha polisi.

Ripoti hiyo baada ya kuisoma niliihifadhi ndani ya jalada la kesi na kulifungia ndani ya kabati.

Katika ripoti hiyo iliweza kunionyesha mambo yafuatayo;

Niliweza kugundua kulikuwa na mawasiliano kati ya Luten Denis Urio na mtuhumiwa Freeman Aikaeli Mbowe, ambayo yalifanyika kwa njia ya Telegram.

Pia kufuatia maelezo ya shahidi Luten Urio ambayo alieleza kuwa alitumiwa fedha jumla ya Sh699, 000.

Ilionyesha 20/7/2020 namba 0719 933386 ambayo ni namba ya Mbowe ilituma kiasi cha Sh 500,000 kwenda kwa namba ya Luteni Urio ambayo n 0787 5552 00

Pia 22/7/2020 ilionyesha kuwa shahidi Luten Urio kupitia namba yake 0787 555200 ilipokea Sh 199,000 kutoka namba ya wakala.

Baada ya kupokea taarifa hizo niliendelea kuandika maelezo ya mashahidi mbalimbali na aliahirisha kuwa ni kweli Mbowe alituma fedha hizo kiasi cha Sh 699,000.

Baada ya upelelezi kukamilika na washtakiwa kufikishwa mahakamani, ilibainika kuwa watuhumiwa watatu ambao ni Kaaya, Gabriel Mhina na Halid, hawana kesi na hivyo kuachiwa.

Na 27/72021 watuhumiwa hao watatu waliachiwa kwa kuondolewa mashtaka dhidi yao.

18/7/2021 niliandika jalada hilo kwenda kwa DCI nilimjulisha kuwa upelelezi wa shauri hilo umekamilika na Kuna ushahidi dhidi ya Mbowe na walimkamata na kumuunganisha na wengine.

Jalada hilo nililifungua kituo Kikuu Cha Polisi Dar es Salaam (Central) lenye kumbukumbu namba CD/ IR/ 2027/2020 lenye kosa la kula njama ya kutaka kufanya vitendo vya kigaidi.

Kidando:Ulipewa maelezo kuwa katika jalada ulilofungua ulielekezwa usiandike jina la Freeman Mbowe ili kuepusha uvujaji wa taarifa, tueleze hapa ulikuwa inamanisha nini?

 Shahidi: Nilikuwa na manisha kuwa angeweza kusitisha kumzuia mtoa taarifa na badala yake angebadilisha njia nyingie ya kufanya uhalifu ambayo ingepekekea Jeshi la Polisi kushindwa kubaini mahali, tarehe na uhalifu huo ungefanyika na hivyo ingepelekea Jeshi la Polisi kushindwa kuzuia uhalifu huo.

Kidando: Ni hatua gani zilizochukuliwa baada vya kuandika barua kwa DCI?

Siku iliyofuatia nilipokea tena jalada kutoka ofisi ya DCI Camillus Wambua alinitaka nilitunze jalada hilo na afanye jitihada za kumkamata Mbowe.

Mnamo 22/7/2021 nilipokea karatasi ya maelezo ya mtuhumiwa Freeman Aikaeli Mbowe kutoka SP Jumanne Malangahe.

Kimsingi karatasi hiyo ilikuwa inaonyesha kuwa Mbowe amekataa kutoa maelezo yake polisi.

Kidando: Ulimfahamu Mbowe alikatwaje? Baada ya kupitia hiyo karatasi?

Shahidi: Nilifahamu Mbowe alikuwa amekamatwa huko Mwanza na kusafirisha kuletwa Dar es Salaam.

Kidando: Kumekuwa na taarifa kuwa washtakiwa hao wamefikishwa mahakamani je ukiwaona utawajua?

Shahidi: Ndio

Kidando: Wataja kwa majina.

Shahidi anawataja kwa majina mshtakiwa wa kwanza kutoka kulia kwangu ni Halfan Bwire Hassan, akifuatiwa na Adam Kasekwa, Mohamed Ling'wenya na Freeman Mbowe.

Kidando: Mheshimiwa Jaji, Shahidi wetu ameweza kuwatambua watuhumiwa.

Shahidi: Mbowe alifikishwa mahakamani 26/7/2021.

Kidando: Kwanini Mbowe alifikishwa mahakamani 26/7/2021 wakati wengine walifikishwa 19/8/2020

Shahidi: Sababu ya Mbowe kufikishwa mahakamni tofauti na wengine ni kwa sababu nilikuwa nasubiri ripoti ya upelelezi.

Sababu inayoonyesha washtakiwa hao wamekula njama ni kwamba mshtakiwa wa kwanza hadi wa nne walikula njama za kutenda vitendo vya ugaidi ni kutokana na maelezo yao.

Sababu ya Pili ni kupitia ushahidi wa Luten Denis Urio, Askari walioandika maelezo ya watuhumiwa na Askari waliowakamata.

Pia fedha Sh699, 000 iliyotumwa kwa Luten Urio huku wakifahamu kuwa fedha hiyo wanaenda kufanyia vitendo vya kigaidi.

Na fedha hiyo ilionyesha mshtakiwa wa pili (Adam Kasekwa) mshtakiwa wa tatu (Mohamed Ling'wenya) mshtakiwa mwingine ambaye hajakamatwa waliweza kufika eneo la utekelezaji wa uhalifu ambalo ni Moshi.

Kidando: Vipi kuhusiana na mshtakiwa wa kwanza (Bwire) kuhusiana na pesa hiyo?

Shahidi: Bwire naye alishapokea fedha kutoka kwa Luten Urio kwa ajili ya utekelezaji

Kidando: Mheshimi ni hayo tu kwa leo.

Upande wa mashtaka umemaliza kutoa ushahidi na sasa hivi upande wa utetezi wanaanza kumhoji shahidi.

Wakili wa utetezi Nashoni Nkungu anayemtetea mshtakiwa wa kwanza katika kesi hiyo, Halfan Bwire Hassan anaanza kumhoji shahidi

Nkungu: Shahidi habari yako.

Shahidi: Nzuri

Wakili: Umepona?

Shahidi: Naendelea na kutumia dawa.

Wakili: Ni sahihi shahidi ulikuwa serious kama kosa lenyewe lipo?

Shahidi: Ni sahihi.

Wakili: Ni sheria gani ilikuwa inawaongoza?

Shahidi: Sheria ya ugaidi na CPA ndio vilikuwa vinatuongoza.

Wakili: Nani alikuwa anatoa uamuzi wa haya makosa ya ugaidi na vitendo vya kigaidi?

Shahidi: Ramadhani Kingai

Wakili: Na wewe una taaluma ya kujua  makosa ya ugaidi.

Shahidi: Ndio

Wakili: Uliipatia wapii?

Shahidi: Botswana.

Wakili: Ni kweli Justine Kaaya ulimuandika maelezo yake?

Shahidi: Hapana

Wakili: Ni sahihi huyo Justine Kaaya kuwa alitumiwa fedha na Mbowe?

Shahidi: Ni sahihi.

Wakili: Huyu Kaaya moja ya maelezo yake ni kwamba alitumia hela Sh 200,000 kwenye line yake ya Voda?

Shahidi: Ni sahihi

Wakili: Na Halfan Bwire alitumia hela na Freeman Mbowe?

Shahidi: Walitumiwa wote lakini kwa malengo tofauti.

Wakili: Hayo malengo ya pesa aliyotumiwa Kaaya wewe umeyaonena wapi?

Shahidi: Kutokana katika maelezo yake.

Wakili: Na malengo ya Bwire ya kutumiwa pesa wewe umeyaonea wapi?

Shahidi: Katika maelezo yake.

Wakili: Huyu Kaaya tunayemzungimza hapa hukuwa umeona malengo yake hadi unamleta hapa?

Shahidi: Rudia swali.

Wakili: Ulikuwa hujagundua lengo lake hadi unamleta mahakamani?

Shahidi: Sahihi.

Wakili: Alifikishwa mahakamani lini?

Shahudi: Septemba 2020.

Wakili: Ndio ukaja kumuachia zaidi mwaka mmoja?

Shahidi: Ni sahihi.

Wakili: Na ukaja kugundua kuwa Kaaya hahusiki baada ya upelelezi kukamilika?

Shahidi: Ndio maana alitolewa.

Wakili: Ni sahihi Kaaya alishiriki kikao cha ugaidi?

Shahidi: Ni sahihi Kaaya alikuwa anashiriki kikao cha ugaidi lakini alikuwa hajui lengo la kikao kile.

Wakili: Kwa hiyo ni sahihi Mbowe alikuwa anashiriki kikao cha ugaidi?

Shahidi: Ni sahihi Mbowe alikuwa anashiriki kikao cha ugaidi.

Mahakama: Hahahahaa

Wakili: Sahihi ni sahihi au sahihi kuwa wewe ndio uli-lebal simu ya Halfan Bwire?

Shahidi: Wewe haukuwa makini kunisikiliza, Mimi Sikusema hivyo.

Wakili: Wewe ulisemaje? Hebu tukumbushe

Shahidi: Mimi siku label simu ya Bwire, bali niliweka label kwenye simu za Luten Denis Urio.

Wakili: Ni sahihi ulipokea bastola A 5340 ikiwa na risasi.

Shahidi: Alipokea hiyo bastola ikiwa na risasi moja na vichwa kutoka Koplo Hafidhi.

Wakili: Hii Aina ya design ya kulebal wewe unaitoa wapi? Ipo kwenye Sheria? Au unabuni tu.

Shahidi: Ipo kwenye Sheria

Wakili: Ni Sheria gani

Sahihi: Sheria ya PGO.

Wakili: Sasa msomee Jaji katika kitabu hiki kuwa mlikabidhiana au hamkukabidhiana vielelezo kuanzia kielelezo cha kwanza hadi cha nane (simu 8), Unafahamu vielelezo hivyo lazima viwe na namba?

Shahidi: Ni sahihi vielelezo lazima viwe na namba.

Wakili: Ni sahihi Kaaya Justine alikuwa kuwa Msaidizi wa katibu wa CCM Wilaya ya Arumeru?

Shahidi: Ni sahihi

Wakili: Pamoja na kupokea hela za kufadhili vitendo vya ugaidi bado aliachiwa huru?

Shahidi: Ni sahihi aliachiwa kwa kuwa hakuwa na hatia na hakujua lengo la Mbowe.

Wakili: Ni sahihi katika maelezo yako uliyoandika 6/8/2020.

Shahidi: Ni sahihi

Wakili: Ni sahihi wewe na wapelelelezi wenzio, hamkuona Mbowe alifanya vikao vya kigaidi Moshi wala Dar es Salaam?

Shahidi: Hatujawahi kuona

Wakili: Hakuna ushahidi wa video au CCTV Camera inayoonyesha Mbowe akipanga ugaidi?

Shahidi: Hakuna

Wakili: Na kuna sauti yoyote uliyorekodi kuhusiana na Mbowe kupanga ugaidi?

Shahidi: Hakuna.

Wakiki: Shahidi wewe unafahamu simu inaweza kurekodi sauti au video

Shahidi: Nafahamu.

Wakili: Unafahamu Jeshi la Polisi linaweza kutumia simu kurekodi sauti au video.

Shahidi: Jeshi halitumi hivyo.

Wakili: Shahidi hivi nikumbushe cheo chako.

Shahidi: Mkaguzi wa Polisi.

Wakili: Shahidi hebu muonyeshe Jaji kama kuna sms zozote wewe kama mpelelezi ulizipitia zinaonyesha kuwa watuhumiwa walipanga vitendo vya kigaidi.

Shahidi: Ipo sms inayoonyesha washtakiwa walipanga kikao cha kufanya ugaidi huko Moshi.

Wakili: Nikikupa kielelezo, utanionyesha hiyo sms ya kupanga kufanya vitendo vya kigaidi?

Shahidi: Ndio

Wakili: Mheshimiwa Jaji naomba kielelezo P6

Shahidi anapewa kielelezo hicho ili aweze kuonyesha hiyo sms.

Shahidi: Nimeiona ni sms ya 22/7/2020, muda wa saa 7:49 mchana inaeleza hivi ' watakuwa na safari ya kwenda Hai leo usiku au kesho asubuhi'

Maelezo haya yanawahusu washtakiwa wanne.

Wakili: Watu hao wakakutana kwenye sms? Au wapi?

Shahidi: Walikutana Hai Moshi katika Hoteli ya Aishi.

Wakili: Dhumuni la safari walishatoa katika maelezo

Shahidi: Kwenye maelezo yao.

Wakili: Una maanisha utazipata?

Shahidi: Yeah tukiunganisha doti.

Mahakama: Hahahaha

Wakili: Ni sahihi mlikuwa mmemuweka Luteni Urio kuwa msiri wenu?

Shahidi: Ni sahihi

Wakili: Ni kweli mlimwambia kila kinachoendelea anawapa taarifa?

Shahidi: Ni sahihi

Wakili: Baada ya Urio kuwapa taarifa, Ni kweli hamkuweza kufunga safari kwenda Moshi katika Aishi Hotel?

Shahidi: Ni kweli.

Wakili: Unafahamu ile Aishi Hotel ina CCTV camera?

Shahidi: Sifahamu.

Wakili: Hufahamu kwa sababu hujawahi kufika?

Shahidi: Ni sahihi

Wakili: Si sahihi hujawahi kutembelea hoteli hiyo?

Shahidi: Ni sahihi

Wakili: Sasa kama hujawahi kutembelea hoteli ya Aishi, Ni sahihi umewafikisha mahakamani watuhumiwa bila kwenda kufanya uchunguzi?

Shahidi: Suala la upelelezi ni kubwa na tukigawanyika kufanya upelelezi.

Wakili: Kwenye ushahidi wako uliwahi kusema wewe ulishawahia kuwa forensic bureau

Wakili: Vielelezo hivyo ulivileta lini na ulimpa nani?

Sahidi: Nilimpa afande Nzowo.

Wakili: Umekuja kuachana na vielelezo hivyo mwaka huu, ni sahihi?

Shahidi: Sina kumbukumbu

Wakili: Shahidi wewe umesema umeondoka pale Polisi Chang'ombe, Agosti 2020, na hukusema vile vielelezo ulikuwa unavitunza ulimkabidhi nani wakati unaondoka?

Shahidi: Nilisema nimevikabidhi Central Polisi.

Wakili: Ulikaa na vielelezo hivyo hata bado kufanyiwa examination, Ni sahihi?

Shahidi: Kama ulikuwa umelala niambie nikukumbushe sawa? Mimi Sijasema hivyo .. Mimi nilipokea vielelezo kuanzia 7 na 8 mwezi wa Nane.

Wakili: Ni sahihi baada ya kuvipokea vielelezo hivyo ulikaa navyo ofisini kwako au ulienda navyo Central.

Shahidi: Nilikuwa navyo Central kwa ajili ya uchunguzi na hainizuii mimi kukaa navyo vielelezo hivyo kwa ajili ya kuvifanyia uchunguzi kabla ya kuvipeleka kwa mtunza vielelezo.

Wakili: Hukusema kama DCI alikupa jukumu la kukaa na vielelezo hivyo na sio Mkuu wa Forensic Bureau.

Shahidi: Kwa uelewa wako wewe.

Wakili: Ulitoa uthibitisho hapa Mahakamani kuwa DCI alikupa muongozo wa kubaki na vielelezo licha ya kuwa hauruhisiwi.

Shahidi: Sikueleza hayo.

Waliki: Kwa ufahamu wako mtu anayemtafutia watu wa kwenda kumfanyia uhalifu sio kosa?

Shahidi: Inategemea.

Wakili: Huyu Urio alikuwa Askari Polisi?

Shahidi: Hakuwa askari Polisi.

Wakili: Mlimpa ulinzi wa kisheria?

Shahidi: Sio mimi niliyepokea taarifa kutoka kwa Denis Urio.

Wakili: Ni sahihi hamkumpa kifaa chochote cha kurekodia?

Shahadi: Sikuwahi kuonana na Denis Urio.

Waliki: Nina imani yangu ulisikiliza ushahidi hapa mahakamani.

Shahidi: Wa nani?

Wakili: Luten Denis Urio.

Shahidi: Wapi?

Wakili: Hapa Mahakamani.

Ushahidi:  Sijawahi kuhusikia

Wakili: Muda gani Halfan Bwire, Adam Kasekwa na Mohamed Ling'wenya walipata kujua kuwa kitu wanachokifanya ni ugaidi?

Shahidi: Wanajua wenyewe watuhumiwa.

Waliki: Unakubaliana na mimi kuwa Luteni Denis Urio kuwa yeye ndio aliunda kundi la kuongoza ugaidi baada ya kupewa fedha na Mbowe.

Shahidi: Sio kweli.

Wakili: Wewe unafahamu sheria ya kumficha jina la mtu?

Shahidi: Hakuna

Wakili: Lakini shahidi unafahamu faili linatakiwa liweje na namba yake zinatakiwa ziweje, si unafahamu?

Shahidi: Namfahamu.

Wakili: Wewe ni mtaalamu wa ramani?

Shahidi: Ninaweza kutafsiri.

Wakili: Kwa hiyo hata Mimi nikichora hapa unaweza kutafsiri?

Shahidi: Huo mchoro wako haufanani na mchoro uliopo kwenye kielelezo.

Wakili: Ni sahihi katika kidaftari chake hakukuwa na majina ya mkoa wowote?

Shahidi: Ni sahihi hakuna majina ya mikoa kwenye michoro, isipokuwa ilionyesha mishale inaelekezwa kwenye vituo vya mafuta vilivyopo Dar .

Wakili Nkungu: Mheshimiwa Jaji ni hayo tu kwa upande wangu.

Wakili Mallya: Mheshimiwa Jaji nina maswali machache lakini naona muda wa health break umefika.

Jaji: Sawa basi naahirisha kesi hii kwa muda wa dakika 45, hivyo naahirisha kesi hadi saa 7: 45 mchana.

Mahakama imerejea na Jaji ameshaingia katika ukumbi wa mahakama

Mawakili wa pande zote wanajitambulisha

Kwa sasa wakili wa utetezi John Mallya anayemtetea mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo Adam Kasekwa ndio anaanza kumuuliza Shahidi maswali kutokana na ushahidi alioutoa

Wakili Mallya: Shahidi kuna namba ya kesi uliyoifungulia jalada yenye kumbukumbu namba CD/IR/2097/2020 umesoma hapa je ipo sahihi au ina makosa?

Shahidi: Ipo sahihi

Wakili: Kwa hiyo shahidi hakuna namba nyingine inayozungumzia hii kesi namba?

Shahidi: Ni sahihi.

Wakili: Haya shahidi kabla ya kuja wewe kutoa ushahidi, kuna wengine walikuja kutoa ushahidi hapa na wakaeleza na unaona kuna picha inakosekana hapa ni sahihi?   Tazama (anamuonyesha nyaraka shahidi)

Shahidi: Ni sahihi

Mallya: Wakati unajaza hiyo nyaraka ni wewe ulikuwa wapi?

Shahidi: Nilikuwa Dar es Salaam ofisi ya DCI.

Wakili: Ni sahihi uko tayari kuvunja Sheria kwa sababu ya utaratibu uliopewa?

Shahidi: Sitakubali kuvunja utaratibu.

Wakili: Kwenye fomu ya Urio uliokabidhiwa ilikuwa na sahihi au laa?

Shahidi: Kama inavyojieleza....Amesaini Urio

Waliki: Mheshimiwa Jaji naomba nipatiwe maelezo ya bwana Denis Urio.

Karani anatafuta nyaraka hiyo na kumpatia Mallya.

Mallya: Unaweza kumueleza Mheshimiwa Jaji na ukamueleza same picha ya signature ya Urio ikoje? Labda ina duara au

Shahidi: Picha ipi?

Wakili: Unaweza kueleza labda ina herufi kubwa au ndogo.

Shahidi: Hivi ni swali la kuniuliza hilo? Haa!  yeye ndio anaweza kujua

Mahakaman: Hahaha

Mallya: Sasa kwa ruhusa ya Jaji naomba unyanyuke uende kumuonyesha nyaraka hizi mbili saini ya bwana Urio, muonyeshe hii na hii

Shahidi ananyanyuka kizimbani hadi kwa Jaji na kumuonyesha saini za Urio zilizopo katika nyaraka mbili tofauti (Maelezo ya Urio na hati ya kukabidhi simu).

Mallya: Kwa taarifa ulizopata unajua Bwire alikamatwa wapi?

Shahidi: Maeneo ya Chang'ombe.

Mallya: Unajua simu ya Bwire ilijaziwa wapi? Licha ya kuwa wewe hukujaza hiyo fomu.

Shahidi: Sijui walijazia wapi

Mallya: Lakini Kingai na Afande Goodluck walikuambia uwasubiri Central ili wakukabidhi simu za Bwire, sasa ni sahihi simu hizo zilijaziwa Central?

Shahidi: Sifahamu

Mallya: Msomee Mheshimiwa Jaji hapa, shahidi anapewa nyaraka na kusoma

Shahidi: Station, Central Dar es Salaam, ndipo jalada la kesi hii limefunguliwa

Mallya: Ishia hapo hapo tu Central Polisi. mimi sitaki ufafanuzi.

Mallya: Wewe ni Shahidi wa namna gani? Umejipanga au?

Shahidi: Nilijipanga.

Mallya: Kama ulijipanga ungekuwa na fomu ya kujaza kielelezo kutoka kwa Urio na wala usingemwambia Urio arudi tena kesho yake kwa ajili ya kukabidhi simu nyingine aina ya Samsung.

Mallya: Kumtukana Rais ni moja ya matishio ya usalama wa nchi?

Shahidi: Sifahamu.

Mallya: Ugaidi ni tishio la usalama wa nchi?

Shahidi: Ndio.

Mallya: Mlalamikaji katika kesi hii alikuwa ni nani?

Shahadi: Robert Boaz aliyekuwa DCI na ACP Kingai

Shahidi: Na DCI ndio aliyetuma watu wa kufanya upelelezi.

Mallya: Ni lini ulimweleza DCI kuwa upelelezi dhidi ya Mbowe umekamilika?

Shahidi: 18/7/2021 ndio nilimwandikia DCI kuwa upelelezi dhidi ya Mbowe umekamilika na kilichobaki ni kumkamata na kumpekeka mahakamani.

Mallya:  Unasema ulimwandikia DCI kuwa 18/7/2021 na 30/7/2021 uliandika maelezo ya Justine Kaaya ni sahihi?

Shahidi: Hapana maelezo ya Kaaya ni ushahidi wa ziada

Mallya: Shahidi wewe unakaa Dar es Salaam

Shahidi: Sahihi

Mallya:  Ni sahihi unafahamu 18/1/2022 Soko la Karume liliungua moto?

Shahidi: Nilisikia.

Mallya: Sasa wakati masoko ya Karume na kule Moshi yanaungua moto, Mbowe na wenzake walikuwa wapi?

Shahidi: Ndani

Mallya: Wapi?

Shahidi: Walikuwa gerezani.

Mallya: Sasa hamuoni kama ni laana ya Mbowe kwa kuwa mlikuwa mmemsingizia kuchoma moto?

Shahidi: Sio kweli, ni uongo.

Shahidi: Taarifa tulizokuwa nazo ni Mbowe kulipua vituo vya mafuta, kukata miti na kuweka barabarani.

Mallya: Unafahamu ripoti ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ilisema nini kuhusiana na kuungua moto kwa soko la Karume?

Shahidi: Sifahamu.

Mallya: Ni sahihi unafahamu Justine Kaaya alikuwa anaendelea kuwasiliana na Mbowe, hata baada ya hawa washtakiwa (Bwire, Ling'wenya na Kasekwa) kukamatwa?

Shahidi: Sio sahihi

Mallya: Mimi naiachia Mahakama.

Mallya: Ni sahihi ulipewa simu na wakati unakabidhiwa  simu wewe ulikuwa eneo gani.

Shahidi: Ndio na nilikuwa kituo Kikuu cha Dar es Salaam.

Mallya: Wakati unakabidhiwa simu uliambiwa IMEI ya simu imefutwa wewe ulifanya utaratibu wa kupata IMEI zake na ulikuwa na nani?

Shahidi: Nilikuwa na DC Goodluck

Mallya: Ling'wenya mwenyewe alikuwepo

Shahidi: Hakuwepo

Mallya: Ester Ndunguru alikuwepo?

Shahidi: Hakuwepo

Mallya: Unasema ulibonyeza namba fulani fulani hadi ukapata hiyo IMEI, ni sahihi?

Shahidi: Ni sahihi

Mallya: Unafahamu Mbowe alikamatwa na kuchukuliwa vitu nyake ikiwemo simu na kompyuta?

Shahidi: Nafahamu alikamatwa na viti kama simu zaidi ya moja na laptop.

Mallya: Simu aina gani?

Shahidi: zaidi ya moja.

Mallya: Na kompyuta ngapi na aina gani?

Shahidi: Sijui aina ila ni zaidi ya moja.

Mallya: Mimi naweza kukuambia japo sikuwepo huko ni laptop mbili aina ya Apple.

Mallya: Kwa hiyo mlivipelekwa maabara ya uchunguzini

Shahidi: Ndio

Mallya: Ni sahihi kuwa hukuongozwa kusema kuwa simu na laptop za Mbowe ulizipeleka kwenye maabara ya uchunguzi?

Shahidi: Ni sahihi.

Mallya: Na mpaka leo bado hujapata ripoti ya uchuguzi vifaa hivyo?

Shahidi: Leo asubuhi ndio nimejulisha kuwa matokeo ya uchuguzi vifaa hivyo ndio umekamilika.

Shahidi: Japo bado sijapewa ripoti.

Mallya: Tuende eneo lingine, Line ya Airtel ya Luteni Urio iko wapi?

Shahidi: Ipo kwenye simu yake.

Mallya: Urio alipokuja kutoa ushahidi alisema line yake haioni na hata alivyoiwasha haikuwaka, una uhakika ipo kwenye simu?

Shahidi: Ipo kwenye simu yake.

Mallya: Shahidi wewe ni mzoefu ni sahihi dawa za kulevya ni hatari

Shahidi: Ni sahihi

Mallya: Ni sahihi hawa vijana wangekuwa wanatumia ingekuwa ni rahisi wao kutekeleza vitendo hivyo, kwa hiyo wanakesi mbili

Shahidi: Kesi ya dawa za kulevya ipo na hapa wapo wameshtakiwa kwa vitendo vya ugaidi.

Shahidi: Kesi wanayotuhumiwa nayo ni ya kweli.

Mallya: Hivi Makao makuu ya Jeshi la Polisi ni Dodoma au mmesha hama Dar?

Shahidi: Dodoma

Mallya: Hivi Ni sahihi, Polisi wa Central wanalalamikiwa kutoa Siri za wateja wao?

Shahidi: Si sahihi.

Mallya: Kwanini jalada la kesi lilifunguliwa Dar es salaam na sio sehemu nyingine.

Shahidi: Ni kwa sababu taarifa za kesi ndio zilipokuwa.

Mallya: Ikitokea katika mkoa fulani kuna uhalifu unataka kutokea, kuna askari anaweza kutumwa kwenda kuzuia huo uhalifu ?

Shahidi: Inategemea na mazingira.

Mallya: Ni tarehe gani kati ya 14 na 18/7/2020 ndio ulifungua jalada la kesi kwa madai ya kutoa fedha kwa ajili ya kufadhili vitendo vya kigaidi?

Shahidi: 22/7/2020 Mbowe ndio ali- organized suala la kufanya vitendo vya kigaidi kwa kutoa fedha.

Shahidi: Na hata katika maelezo ya onyo, alisema mimi na chama changu tunedhamiria kuchukua dola.

Mallya: Kwa hiyo ulifungua kesi kupitia hiyo kauli, je hao wanachama wake unawafahamu? Kuna Lissu, Mnyika na Lema

Shahidi: Mimi Sifahamu.

Mallya: Ni sahihi chama cha CCM kimeundwa kwa sababu ya kushika dola?

Shahidi:  Ni chama chochote cha kisiasa kipo kwa ajili lengo la kuchukua dola.

Mallya: Chadema mwama 2020 kilishiriki katika uchaguzi au hakikushiriki.

Shahidi: Kilishiriki

Mallya: Kwenye hati ya mashtaka ametajwa Lengai Ole Sabaya, alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, uliwahi kumtafuta ukamhoji? Kwa kuwa yeye ndio alikuwa muathirika wa matendo hayo

Shahidi: Sijawahi kumtafuta.

Mallya:  Sasa Lissu aliyepigiwa risasi na IGP Sirro alisema upelelezi wa Lissu haujakamilika kwa sababu Lissu hakuhojiwa, hauoni kama ni kuna upendeleo wa upande mmoja? Huyu ambaye hata hajaguswa (Ole Sabaya) yeye upelelezi wake umekamilika lakini Lissu ambaye alipigwa risasi akavunjika vunjika upelelezi wake bado haujakamilika?

Shahidi: Umekamilika kwa sababu Mbowe alipanga kula njama ya vitendo vya kigaidi kwa kuchoma masoko, kulipua vituo vya mafuta na kukata miti na kuweka miti barabarani.

Mallya: Haya ulitembelea vituo vya mafuta, sasa ulishindwa hata kupewa risiti ili kuonyesha kuwa ulienda katika vituo hivyo.

Shahidi: Sikuona haja ya kuchukua risiti.

Mallya:  Haya twende kwenye masoko...unafahamu vyama vya ushirika?

Mallya: Hata ulitembelea masoko ulishindwa kupewa hata risiti?

Shahidi: Sikuona.

Mallya: Nikisema nyie ndio mliogoza vitendo vya ugaidi nitakuwa sahihi?

Shahidi: Sio kweli.

Mallya: Unafahamu

Mallya: Niambie hao watu wengine alishiriki nao katika vikao vya kupanga ugaidi aliwatoa wapi?

Shahidi: Alitafutiwa na Luteni Denis Urio ili wafanye taarifa.

Mallya: Kwa hiyo wakati wanakaa vikao walikuwa tayari wanafanya ugaidi au?

Shahidi: Walikuwa tayari wamesha shawishiwa kufanya vitendo vya ugaidi.

Mallya: Kwani vikao hivyo walikaa wapi?

Shahidi: Moshi hoteli ya Aishi.

Mallya: Kwa hiyo walianza vitendo vya ugaidi tarehe 25 /7/2020 Pap? Ndio wali-turn kuwa magaidi?

Shahidi: Ni sahihi

Mallya: Wakati Mbowe anawatumia pesa, watuhumiwa walikuwa magaidi au sio magaidi?

Shahidi: Hawakuwa magaidi.

Mallya: Wakati Mbowe anawatumia pesa siku ile ya 20/7/2020 pesa zile zilikuwa chafu au safi?

Shahidi: Iikuwa ni pesa chafu.

Mallya: Kama siku hiyo ile pesa ingetumwa na Mbowe, halafu wale vijana wangeikataa ile pesa kwa kutoa taarifa, je Ile pesa ingekuwa safi au chafu?

Shahidi: Ingekuwa bado ni chafu.

Mallya: Kwa hiyo Mbowe angekuwa amekaa na nani kwenye hicho kikao cha ugaidi?

Shahidi: Angekuwa amekaa na washtakiwa watatu.

Mallya: Wewe ndio ulimwambia Mheshimiwa Rais kuwa kwenye kesi hii kuwa kuna watu tayari wameshafungwa? Ni sahihi.

Shahidi: Sijawahi kumwambia Mheshimiwa Rais.

Shahidi:  Na wala sijawahi kusikia hicho kitu.

Mallya: Shahidi unatuhuma kuwa wewe ndio uliyempiga Halfan Bwire katika kituo ha Polisi Chang'ombe kwa kusema kuwa 'mshusheni chini ni nimshughulikie'

Shahidi: Sijawahi kumpiga wala kutoa kauli hiyo.

Mallya: Katika ushahidi wako shahidi, ulisema ulimwambia Urio atoe laini zake kwa sababu ule ujumbe wa mawasiliano ya Telegram, huwa unabakia kwenye simu hata kama utatoa line? Ni sahihi.

Shahidi: Usahihi ni kwamba ujumbe uliopo kwenye Telegramu huwa ubaki kwenye simu hata baada ya mtu atatoa line ya simu.

Mallya: Katika ushahidi wako shahidi, ulisema ulimwambia Urio atoe laini zake kwa sababu ule ujumbe wa mawasiliano ya Telegram, huwa unabakia kwenye simu hata kama utatoa line? Ni sahihi.

Shahidi: Usahihi ni kwamba ujumbe uliopo kwenye Telegramu huwa ubaki kwenye simu hata baada ya mtu atatoa line ya simu.

Mallya: Hiyo line uliyomwambia aitoe ilikuwa ni line gani?

Shahidi: Ilikuwa ni Vodacom.

Mallya: Unaweza kutuambia ni kwanini Luteni Urio wakati anatoa ushahidi alifungua simu moja na simu nyingine hazikuwaka anadai kuwa huenda hazina chaji, sasa wewe ukiwa kama mpelelezi unafikiri kwanini simu zingine hazikufunguka?

Shahidi: Sifahamu.

Mallya: Nisahihi katika faili lako la upelelezi ulikuwa na zaidi ya hawa watuhumiwa wanne?  Ni sahihi

Shahidi: Ni sahihi.

Mallya: Kwani jumla ya watuhumiwa waliokuwa katika kesi hii ni wangapi

Shahidi:  Walikuwa saba.

Mallya: Mheshimiwa Jaji ni hayo tu.

Wakili Fredrick Kihwelu: Mheshimiwa Jaji zimebaki dakika tatu kufikia saa 11 jioni.

Kihwelu: Naomba ahirisho la kesi hii hadi kesho kwa sababu muda umeenda.

Jaji: Upande wa mashtaka mnasemaje?

Kidando: Hatuna pingamizi.

Jaji: Basi kupitia ombi lililowasilishwa na wakili wa utetezi Fredrick Kihwelu, naahirisha kesi hii hadi kesho, Februari 8, 2022 saa 3: 00 asubuhi.

Jaji: Shahidi utaendelea kuwa chini ya kiapo na washtakiwa wataendelea kuwa chini ya usimamizi wa magereza hadi kesho.

Jaji: Niwatakie jioni njema.

Court!!!

Chanzo: www.mwananchi.co.tz
Related Articles: