Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia Aikataa kesi ya Mbowe - Video

Samia Dw Rais Samia akihojiwa na DW

Fri, 18 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KWA mara nyingine tena, Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amewataka watu wanaokosoa hatua ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kufunguliwa mashtaka ya ugaidi, kuiachia mahakama iamue kama ana kosa au hana kosa.

Ni baada ya mtangazaji wa D.W Swahili, Sudi Mnette, kumuomba atoe ufafanuzi juu ya kauli yake aliyowahi kuitoa dhidi ya kesi ya uhujumu uchumi, namba 16/2021, inayomkabili Mbowe na wenzake katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, jijini Dar es Salaam.

“Nitatolea ufafanuzi kauli ngapi? Watu wanasema kila kauli kuhusu Rais, utazitolea zote ufaanuzi? Anayesema mwache aseme na nilisema mapema kwamba, mimi naruhsu freedom of speech (uhuru wa kuongea), sababu watu wakisema napata kujua wanayoyasema na mimi najua ya kuyarekebisha jinsi ninavyoendesha Serikali yangu,” amesema Rais Samia.

Rais Samia amesema “kwa hiyo kama wamesema, kila wanalosema nitalitolea ufafanuzi? Acha waseme tuiachie mahakama, kesi iko mahakamani mahakama itaamua ana kosa au hana kosa. Sisi hatuwezi kusema chochote.”

Agosti 2021, akihojiwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC Swahili), Rais Samia aliwataka wanaopiga kelele kuhusu kesi hiyo, waiachie mahakama kwani ndiyo itakayoamua kama ana hatia au hana hatia.

Katika kesi hiyo yenye mashtaka sita ya ugaidi, mbali na Mbowe, washtakiwa wengine ni waliokuwa makomando wa Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Halfan Bwire Hassan, Adam Kasekwa na Mohammed Abdillah Ling’wenya.

Kesi hiyo inasikilizwa mfululizo mbele ya Jaji Joachim Tiganga, ambapo kesho Ijumaa, mahakama hiyo inatarajia kutoa uamuzi mdogo kama wana kesi ya kujibu au hawana, baada ya upande wa mashtaka kufunga ushahidi.

Rais Samia Suluhu Hassan, akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Ujerumani (D.W Swahili), ameizungumzia kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake, akisema “acha waseme tuiachie mahakama itaamua ana kosa au hana kosa, sisi hatuwezi kusema chochote.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: