Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mawakili wa utetezi ‘wakomaa’ na mpelelezi kesi ya kina Mbowe

Mbowe Pic Data Mawakili wa utetezi ‘wakomaa’ na mpelelezi kesi ya kina Mbowe

Wed, 9 Feb 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Mawakili wa upande wa utetezi katika kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu, wameendeea kumhoji shahidi wa 13 wa upande wa Jamhuri kuhusu ushahidi alioutoa.

Leo Jumanne Februari 8, 2022 ni siku ya pili ambapo mawakili wa utetezi wanamhoji shahidi huyo wa upande wa mashtaka ambaye ni Mkaguzi wa Polisi, kutoka Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi, Mkoa wa Kipolisi Temeke, Tumaini Sostenes Swila.

Katika muendelezo huo, Leo asubuhi Swila alianza kuhojiwa na Wakili wa utetezi Fredrick Kihwelu na kufuatiwa na Wakili Peter Kibatala.

SOMA: Mawakili wa utetezi waanza kumhoji Mkaguzi wa Polisi kesi ya kina Mbowe

Hata hivyo, Wakili Kibatala hakumaliza maswali yake ya dodoso hivyo kuomba kuendelea kesho.

Shahidi huyo wa 13 wa upande wa mashtaka alianza kuhojiwa jana Wakili Nashoni Nkungu na Wakili John Mallya.

Jaji Joachim Tiganga anayesikiliza kesi hiyo katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi ameiahirisha mpaka kesho Jumatano.

Fuatilia hapa mahojiano hayo kati ya mawakili wa upande wa utetezi na shahidi wa 13 wa upande wa mashtaka…

Jaji Joachim Tiganga ameshaingia mahakamani na mawakili wa pande zote wamajitambulisha.

Sasa wakili wa utetezi Fredrick Kihwelu anaanza kumhojo shahidi

Wakili: Shahidi salama?

Shahidi: salama

Wakili: Sasa shahidi kwa mujibu wa maelezo yako simu 8 zilipelekwa kwaajili ya uchunguzi ni sahihi?

Shahidi: Sahihi.

Wakili: Hivi shahidi ukienda dukani kununua simu ndani ya simu kunakuwa na laini?

Shahidi: Hapana

Wakili: Kwa hiyo nitakuwa sahihi simu na liaini ni vitu viwili tofautuli?

Shahidi: Ni sahihi

Wakill: Shahidi hebu mwambie Mheshimiwa Jaji kama simu nane ambazo zimewasilishwa kama vielelezo line zake pia ziliwasilishwa kama vielelezo?

Shahidi: Ndio

Wakill: Hebu mkumbushe Mheshimiwa Jaji ni vielelezo namba ngapi?

Shahidi: Laini ziko ndani ya simu

Wakili: Tumekubaliana laini na simu ni vitu viwili tofauti hebu mkumbushe Jaji ni vielelezo namba ngapi?

Shahidi: Zilizowasilishwa ni simu na si laini

Wakili: Tukakubaliana simu inatambuliwa kwa IMEI number?

Shahidi: Ni sahihi

Wakili: Shahidi kwenye maelezo yako ulisema Januari 2020 ulipata uhamisho wa muda kwend amakao makuu Polisi Dar?

Shahidi: Ni sahihi

Wakili: Ni sahihi Augusti ulirudi kwenye kituo chako cha kazi?

Shahidi: Sahihi

Wakili: Umisho waonulikuwa wa muda gani?

Shahidi: Mwaka mmoja na miezi minane

Wakill: Umeleta uthibitisho mahakamani kuthibitisha kuwa ulipata uhamisho wa muda mfupi?

Shahidi: Sijaleta

Wakili: Unakubaliana na mimi uhamisho ni mchakato?

Shahidi: Ni utaratibu wa kazi

Wakili: Uliieleza mahamama kuwa ulipitia taratibu?

Shahidi: Ndio nilieleza

Wakili: Shahidi nitakuwa sahihi nikisema timing ya uhamisho wako ilikuwa ni ya kimkakati na ilihusu maandalizi ya shauri hili?

Shahidi: Si kweli

Wakili: Shahidi ulisema taarifa za matendo ya uhalifu zilipokewa na DCI Robert Boaz kwanza?

Shahidi: Ni Sahihi

Wakili: Ilihusu kuchoma masoko?

Shahidi: Ndio na matukio mengine

Wakili: Ilikuwa ni maandamano?

Shahidi: Ndio na matukio mengine

Wakili: Ilikuwa ni kuwadhuru viongozi?

Shahidi: Ndio na matukio mengine

Wakili: Katika orodha hiyo kuna ugaidi?

Shahidi: Ndio

Wakili: Ulieleza uongozi waliopanga kudhuriwa?

Shahidi: Ndio

Wakili: unaweza kumtaja?

Shahidi: Mmoja wapo ni Sabaya Ole Lengai

Wakili: Huyo ndio viongozi?

Shahidi: Ni mmoja wapo waliopanga kudhiriwa

Wakili: Mwingine ili wawe viongozi?

Shahidi: Mwingine simjui

Wasikilizaji wanasonya

Jaji: Tumeshakubaliana wengine ni wasikilizaji muacheni shahidi atoe majibu

Wakili: Hivi shahidi kuandamana ni kosa?

Shahidi: Ni kosa kama hawatafauata sheria?

Wakili: Kwani walishaanza kuandamana?

Shahidi: Bado walikuwa wanapanga?

Wakili: Ulijuaje kama hawatapata kibali?

Shahidi: Hilo siwezi kujibu

Wakili: Ni sahihi maelekezo ya kufungua jalada ulipewa na ACP Ramadhani Kingai?

Shahidi: Ni sahihi

Wakili: Kwa hiyo shahidi nitakuwa sahihi nikisema mtu mmoja anaweza akaamua upewe shtaka la namna gani?

Shahidi: Sio sahihi

Wakili: Wewe ulikuwa umeshapewa jukumu la kuwa msaidizi wake wa upelelezi wa kesi hii?

Shahidi: Ni sahihi kwa upande wa jalada la uchunguzi

Wakili: Kwani alikwambia fungua kesi fulani au mlijadiliana kuwa kwa kosa hili ni kesi fulani?

Shahidi: Alinielekeza

Wakili: Alikwambia au walijadiliana na nani mpaka kuamua hili ni kosa la ugaidi?

Shahidi: Hakuniambia

Wakili: Kwa hiyo ni sahihi Ramadhani Kingai ndio alifungua shtaka la ugaidi?

Shahidi: Hili siwezi kuliibia

Wakili: Kwa maelekezo ya Kingai ulipokea simu mbili walizokamatwa nazo watuhumiwa wawili kule Moshi?

Shahidi: Ni sahihi

Wakili: Mlikabidhiana simu hizo kwa hati ya makabidhiano?

Shahidi: Hapana

Wakili: Ndio maana hati ya makabidhiano haiko mahakamano hapa?

Shahidi: Ndio

Wakili: Kingai aliamuru ukabidhIwe simu za Half an Bwire?

Shahidi: Ndio

Wakili: Ni kweli simu za Luteni Urio mlikabidhiana kwa hati ya makabidhiano?

Shahidi: Ni sahihi

Wakili: Ni sahihi hiyo hati ya makabidhiano iko mahakamani?

Shahidi: Ni sahihi

Wakili: Ni sahihi kuwa hujawasilisha mahakamani hapa hati ya makabidhiano ya simu za Bwire?

Shahidi: Ni sahihi

Wakili: Kwa maelezo yako ulipokea ripoti ya uchunguzi kutka kwa inspekta Ndowo?

Shahidi: Ni sahihi

Wakili: Mlikabidhiana kwa hatib ya makabidhiano?

Shahidi: Nilisaini kitabu

Wakili: Unaweza kumkumbusha jaji umwkiwasilishamahakamani?

Shahidi: Sijakiwasilisha

Wakili: Pia ulipkkea simu nane kutoka kwa Inspeka Ndowo?

Shahidi: Ni sahihi

Wakili: Kwa maelezo yako Mheshimiwa Mbowe alikuwa akiwawezesha watuhumiwa kwa fedha na huduma Mbalimbali ni sahihi?

Shahidi: Ni sahihi

Wakili: Hizi huduma mbalimbali ni zipi?

Shahidi: Mheshimiwa Mbowe alikuwa anawasafirisha watuhumiwa, chakula na malazi huko Moshi

Wakili: Kwenye maeelezo yako umeeleza uchunguzi wa cyber unaonesha Mbowe alivyokuwa anawaelekeza nini cha kufanya, hiyo iko wapi?

Shahidi: Kwenye maelezo ya watuhumiwa

Wakili: Shahidi ni sahihi jina la Mheshimiwa Mbowe halikuandikwa kwenye nyaraka na kwamba angesitisha?

Shahidi: Ndio kwamba angeweza kusitisha na kutoa taarifa kwa msiri au kutumia njia nyingine hivyo ingekuwa vigumu Polisi kuelewa

Wakili: Kwani mtu akiamua kusitisha uhalifu ni kosa?

Shahidi: Inategemea

Wakili: Kwani Mbowe ni askari?

Shahidi: Hapana

Wakili: Ana mtoto polisi?

Shahidi: Kama nilivyosema kile kitabu cha Polisi kinasomwa na askari wengi hata wa mikoani, sasa katika hao hujui kuwa ni nani labda kuna ndugu yake hivyo amengeweza mwambia

Wakiii: Ni kawaida polisi kuficha jina la mtuhumiwa?

Shahidi: Ni kawaida

Wakili: Ni tukio lipi mnaficha taarifa?

Shahidi: Inategemea

Wakili: Ni katika mazingira gani?

Shahidi: Siwezi kutaja

Wakili: Kwani kuna tukio lipi lingine kubwa zaidi ya hili ambayo unaona huwezi kutuambia?

Shahidi: Yapo

Wakili: Basi mueleze Jaji usitueleze sisi.

Shahidi: Siwezi kusema.

Wakili: Shahidi tarehe 18/7/2020 wakati unakwenda kufungua jalada wakati jina la mtuhumiwa kimefichwa kwenye jalada hilo nani alikuwa mtuhumiwa?

Shahidi: Alikuwa ni Freeman Aikael Mbowe

Wakili: Kwa mujibu wa maelezo yako unasema mashahidi walifanya confession, kwa maana walikiri makosa, ni sahihi?

Jaji: Kwenye swali lako umesema mashahidi ni sahihi?

Wakili: Sorry, watuhumiwa, wa kwanza, wa pili na wa tatu?

Shahidi: Kwa mujibu wa maelezo yao

Wakili: Ulisema kwenye sampuli walikataa ni sahihi, sasa shahidi walikiri au walikataa?

Shahidi: Mshtakiwa wa kwanza alikataa lakini kwenye uchunguzi ulionekana ni mwandiko wake.

Wakili Kihwelu amemaliza kumhoji shahidi na sasa ni zamu ya Wakili Peter Kibatala.

Kibatala: Shahidi tumewahi kukutana na wewe kikazi au leo ndio mara ya kwanza?

Shahidi: Sikumbuki

Kibatala: Haukumbuki kuna sehemu yoyote tumeweza kukutana kuhusiana na uchukuaji wa vielele?

Shahidi: Sikumbuki

Wakill: Unafahamu kwa mwandiko wa mtu unaweza kunadilika kutokana na psychological factors?

Shahidi: Sifahamu

Wakili: Unafahamu kwamba mtu aliyefiwa na mama yake na anayetoka katika harusi ukimwambia aandike mianduko yake inatofautiana?

Shahidi: Sifahamu

Wakili: Still unasema umesomeal?

Shahidi: Ndio

Wakili: Unafahamu moja ya maandiko ya mtaalamu wa maandishi wakati wa kuchukua sampuli za miandiko lazima awepo shahidi huru?

Shahidi: Nafahamu lakini si lazima.

Wakili: Unafahamu kwamba wakati unapochukua sampuli za miandiko ni lazima utofautishe kati ya uppercase na lower case? (herufi kubwa na ndogo)

Shahidi: Nafahamu

Wakili: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji kama ulitofautisha? 

Shahidi: Sikumwambia

Wakili: Unafahamu taaluma ya umri wa maandishi?

Shahidi: Hayo Mambo unayoniuliza ni ya wachunguzi

Wakili: Unafahamu kwamba kujua hiyo michoro ilichorwa lini kwetu ni muhimu?

Shahidi: Sifahamu.

Wakili: Unafahamu kwamba hata kwako kujua hiyo michoro ilichorwa lini ni muhimu?

Shahidi: Kwangu si muhimu, muhimu kwangu ni kulinganisha maandishi

Wakili: Huoni kama suala la kujua ni lini akichora inahusiana na kesi yetu ya ugaidi?

Shahidi: Kwa hilo siwezi kulijibu

Wakili: Huwezi kulijibu kwa kuwa hutaki au hujui?

Shahidi: Rudia swali

Wakili: Hii ni kesi ya ugaidi na standard yake ni beyond reasonable doubts. Kama hiyo michoro ilichorwa baada ya tarehe 5/8/2020 hiyo michoro inakuwa na uhusiano na kesi hii?

Shahidi: Inakuwa haina umuhimu.

Wakili: Na bado unasema kwako haikuwa muhimu.

Wakili: Kama kidaftari Bwire angekuwa amechora tarehe 5/2/2020 hiyo ingekuwa ni muhimu kwako?

Shahidi: Kama angekuwa amechora kwa nia njema asingekataa

Wakili: Nilikusikia umisema kwamba DCI ndiye akiyepokea taarifa ya kwanza kutoka kwa Luteni Urio.

Shahidi: Ndio

Wakili: Na DCI ni bosi wako, bosi wa Kingai, Jumanne Malangahe, Mahita, mchunguzi wa silaha mchunguzi wa maandiko?

Shahidi: Ni sahihi

Wakili:  Na DCI ndiye akiyempa maelekezo Kingai?

Shahidi: Ndio

Wakili: DCI ana msaidizi?

Shahidi: Ndio

Wakili: Wakati huo msaidizi wake alikuwa nani?

Shahidi: Charles Kenyella?

Wakili: Unafahamu kwamba kama DCI angekuwa ana-comply taratibu alipaswa amweleze msaidizi wake? 

Shahidi: Sio sahihi

Wakili: RPC akikutuhumu anaruhusiwa kupeleleza?

Shahidi: Haruhusiwi lakini mwisho anashiriki katika maamuzi

Wakili: Kwa nini haruhusiwi ni ili kuzuia nini?

Shahidi: Ni utaratibu tu wa kazi

Wakili: Order iliyotoka kwa DCI unaweza kumbishia?

Shahidi: Inategemea

Wakili: Na Nini?

Shahidi: Na order yenyewe ni sahihi kwa utaratibu wa kazi

Wakili: wewe wakati unafungua jalada ni facts gani ambazo ulikuwa unazijua?

Shahidi: Uwepo wa taarifa za mtuhumiwa wa nne.

Wakili: Mpaka muda huo ulikuwa unaongea na Luten Urio ua bado?

Shahidi: Nilikuwa bado

Wakili: Kwa hiyo hukuwa na taarifa sahihi za kukuwezesha kufungua jalada?

Shahidi: Taarifa zilikuwepo kwa DCI

Wakili: Wewe ulikuwa umeshamhoji DCI Boaz maelezo yake il ujue kile akichosimuliwa na Boaz?

Shahidi: Hiyo ilikuwa ni taarifa tayari

Jaji: Swali ni kwamba wewe binafsi ulimuuliza DCI?

Shahidi: Hapana

Wakili: Unafahamu maana ya hearsay?

Shahidi: Nafahamu

Wakili: Ulikuwa hujamhojj DCi, Urio wala Kingai, kwa hiyo ulichofanyia kazi wewe ilikuwa ni hearsay?

Shahidi: Ni hearsay lakini haizuii

Wakili: Sijakuuliza kama inazuia au haizuii.

Wakili: Ni sahihi kwamba at the end of the day aliyekuwa anasimamia suala hili mpaka kina Mbowe wanafikishwa mahakamani ni huyohuyo Boaz?

Shahidi: Sahihi

Wakili: Na barua zote directly au indirectly zilikuwa zinatoka kwake?

Shahidi: Ndio

Wakili: Huoni kama alikuwa na maslahi binafsi maana yeye huyo ndo anapokea taarifa, anaunda timu ya upelelezi na mengine?

Shahidi: Hana maslahi binafsi

Wakili: Taarifa zilipokewa na nani?

Shahidi: DCI ambaye ndo anahusika na taarifa za nchi nzima

Wakili: Ni sahihi wakati unafungua faili la uchunguzi ulikuwa huna maelezo ya (DCI Boaz) mlalamikaji?

Shahidi: Ni kweli lakini si lazima

Wakili: Maelezo ya DCI ya tarehe 13/8/2020 na unafahamu kwa mujibu wa Sheri Ofisa wa polisia anayepokea taarifa kwa mdomo au kwa maandishi anaitoa mara moja?

Shahidi: Ni sahihi

Wakili: Ulichosema si lazima kuwepo maelezo ya mlalamimaji ni nini?

Shahidi: Kwamba taarifa iliyokuwa imeandikwa kwenye jalada tayari.

Shahidi: Unapopokea taarifa kwa raia Kama yeye ndiye mlalamikaji kwa ajili ya kufungua kesi na kama jina lake ndio linatakiwa kuonekana kwenye kesi ni lazima aandike kwanza maelezo, lakini kama unapokea taarifa tu na wewe ndio mlakamikaji (ofisa wa Polisi) hulazimiki kuandika maelezo kwanza

Wakili: Sheria gani ina-support decision hiyo?

Shahidi: Sikumbuki

Wakili: Nikikuombea PGO?

Shahidi: Sawa

Wakili anamuombea na kumpa shahidi PGO amtafutie kifungu kinachoeleza hivyo, lakini shahidia anapopekua baada ya muda anasema kuwa hajafanikuwa kukiona

Wakili: Sasa mimi nakuonyesha CPA (Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai) soma kifungu cha 10(3) alichotumia DCI kinasemaje?

Shahidi: Anasoma kifungu hicho

Wakili: Umekielewa?

Shahidi: Ndio

Wakili: Mueleze Mheshimiwa Jaji ni nini?

Shahidi: Kwamba ofisa polisi anayefanya upelelezi anapopokea taarifa kutoka kwa mtu yeyote lazima aandike maelezo

Wakili: Kwa hiyo ni sahihi kuwa ni lazima uwe na maelezo ya mlalamimaji kwanza kabla ya kufungua jalada?

Shahidi: Hapo ni sahihi

Wakili: Maelezo ya DCI yaliandikwa baada ya muda gani?

Shahidi: Kama miezi mitatu

Wakili: Maelezo ya Urio uliyaandika lini?

Shahidi: Tarehe 11/8/2020

Wakili: Ni baada ya muda gani tangu ulipofungua file?

Shahidi: Baada ya wiki mbili?

Wakili: Ni wiki mbili hizo?

Shahidi: Kama wiki tatu

Wakil: Bado unataka tuamini kuwa hii si ya kutunga?

Shahidi: Si kweli

Wakili: Maelezo ya mlalamikaji (DCI) yameandikwa karibu miezi mitatu na mtoa taarifa (Luten Urio) yaliandikwa wiki tatu baadaye, hii inaingia akilini? Siyo kama akina Adamoo na Ling'wenya wanavyodai kuwa naye alikamatwa baada ya kumtaja kuwa ndiye aliyewapeleka kwa Mbowe

Shahidi: Inaingia akilini, kuchelewa kuandika maelezo sio tatizo.

Shahidi: Unapopokea taarifa kwa raia Kama yeye ndiye mlalamikaji kwa ajili ya kufungua kesi na kama jina lake ndio linatakiwa kuonekana kwenye kesi ni lazima aandike kwanza maelezo, lakini kama unapokea taarifa tu na wewe ndio mlakamikaji (ofisa wa Polisi) hulazimiki kuandika maelezo kwanza

Wakili: Sheria gani ina-support decision hiyo?

Shahidi: Sikumbuki

Wakili: Nikikuombea PGO?

Shahidi: Sawa

Wakili anamuombea na kumpa shahidi PGO amtafutie kifungu kinachoeleza hivyo, lakini shahidia anapopekua baada ya muda anasema kuwa hajafanikuwa kukiona

Wakili: Sasa mimi nakuonyesha CPA (Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai) soma kifungu cha 10(3) alichotumia DCI kinasemaje?

Shahidi: Anasoma kifungu hicho

Wakili: Umekielewa?

Shahidi: Ndio

Wakili: Mueleze Mheshimiwa Jaji ni nini?

Shahidi: Kwamba ofisa polisi anayefanya upelelezi anapopokea taarifa kutoka kwa mtu yeyote lazima aandike maelezo

Wakili: Kwa hiyo ni sahihi kuwa ni lazima uwe na maelezo ya mlalamimaji kwanza kabla ya kufungua jalada?

Shahidi: Hapo ni sahihi

Wakili: Maelezo ya DCI yaliandikwa baada ya muda gani?

Shahidi: Kama miezi mitatu

Wakili: Maelezo ya Urio uliyaandika lini?

Shahidi: Tarehe 11/8/2020

Wakili: Ni baada ya muda gani tangu ulipofungua file?

Shahidi: Baada ya wiki mbili?

Wakili: Ni wiki mbili hizo?

Shahidi: Kama wiki tatu

Wakil: Bado unataka tuamini kuwa hii si ya kutunga?

Shahidi: Si kweli

Wakili: Maelezo ya mlalamikaji (DCI) yameandikwa karibu miezi mitatu na mtoa taarifa (Luten Urio) yaliandikwa wiki tatu baadaye, hii inaingia akilini? Siyo kama akina Adamoo na Ling'wenya wanavyodai kuwa naye alikamatwa baada ya kumtaja kuwa ndiye aliyewapeleka kwa Mbowe

Shahidi: Inaingia akilini, kuchelewa kuandika maelezo sio tatizo.

Wakili: Hiyo tarehe 14/7/2020 ya DCI kukutana na Urio uliitoa wapi?

Shahidi: Kama nilivyoeleza kwenye ushahidi wangu kuwa tarehe 14 /7/2020 DCI alipokea taarifa za uhalifu kutoka kwa Luteni Urio.

Wakili: Soma maelezo haya ya Kingai, ameitaja hiyo tarehe?

Shahidi: Hajataja

Wakili: Soma haya maelezobya mtoa taarifa Luteni Urio, ameitaja hiyo tarehe 14?

Shahidi: Hajaitaja

Wakili: Kwa nini tusiamini kuwa hiyo tarehe 14 mmeitunga baada ya sisi kumhoji Kingai?

Shahidi: Siyo kweli maana mimi ndio niliyefungua jalada la uchunguzi.

Wakili: Hilo jalada la uchunguzi liko hapa mahakamani?

Shahidi: Hapana

Wakili: Unafahamu shahi ni kwamba ushahidi tulionao hapa mahakamani watuhumiwa wa kwanza wenzake na Mbowe walipatikana tarehe 20/8/2020 na si 18/8/2020 unayosema?

Shahidi: Ndio nafahamu kulikuwa na mawasiliano.

Wakili: Tuambie mara ya kwanza aliongea na Lujenge au Bwire (watuhumiwa)

Shahidi: Sifahamu

Wakili: Umewahi kuona mawasiliano ya recruitment ya Lujenge na Bwire mpaka jana unatuambia kuwa  uchunguzi umekamilika jana?

Shahidi: Mawasiliano ninayozungumzia si ya simu.

Wakili: Ulisema kwamba hili faili hamkuweka jina la Mbowe kwa sababu ya kuogopa leakage?

Shahidi: Sahihi

Wakili: DCI alikuwa ameshaamua kuwa kuna tunuma za ugaidi?

Shahidi: Mi Sifahamu

Wakili: Aliyeamua hapa kuna tuhuma za ugaidi ni wewe au Kingai?

Shahidi: Siyo mimi, nimesema nilielekezwa na Afande Kingai

Wakili: Wewe kwa opinion yako ulijua lini kwamba hapa kuna tuhuma za ugaidi?

Shahidi: Baada ya kumhoji mtoa taarifa (Luteni Urio)

Wakili: Ulimwambia Jaji wewe na Kingai mlikaa ofisi gani wakati mnapeana maelekezo?

Shahidi: Sikumbuki

Wakili: Mimi nikisema hamkupeana maelekezo utaishia?

Shahidi: Nimesema kuwa sikumbuki

Wakili: Uamuzi kwamba msiweke jina la Mbowe kwenye file mliufanya pamoja?

Shahidi: Si kweli

Shahidi: Huu uamuzi ulifanyika lini?

Tarehe 18/7/2020

Wakili: Mpaka tarehe hiyo Urio alikuwa anafahamu kuwa Mbowe ni mtuhumiwa alikuwa anatahamu?

Shahidi: Alikuwa anafahamu

Wakili: Alikuwa anakaa wapi vile?

Shahidi: Morogoro?

Shahidi: Urio ni ofisa wa Polisi mwenye kiapo?

Shahidi: Hapana ila ni ofisa wa Jeshi

Wakili: Mlimuapisha Urio kuwa asitoe siri?

Shahidi: Sijasema mimi nilikutana na Urio

Wakili: Unafahamu Urio ali- interact na nani?

Shahidi: Sifahamu, maana kama mtu ameamua mwenyewe kutoa taarifa atawezaje kutoa siri?

Wakili: Hiyo ni supposition sasa. Unafahamu kuwa Urio tarehe 20/8/2020 akikutana na kina Bwire na akawaeleza habari za Mbowe kutaka kufanya ugaidi?

Shahidi: Hilo mimi sijui

Wakili: Sasa unaona kuna watu kama watano si ofisa wa polisi na Kingai ndiye aliunda timu ya upelelezi tena ya Arusha na akiwemo dereva Azizi, unaona bado kuna usiri hapo?

Shahidi: Ndio na ndio maana watuhumiwa walikamatwa na wako mahakamani

Wakili: Mbowe alikuwa ni mzembe kiasi hicho kwamba magaidi wake wamekamatwa na yeye yuko nje mwaka mzima asibadilishe mbinu?

Shahidi: Ndio maana nilisema lengo kuu ilikuwa kuzuia uhalifu.

Wakili: Unafahamu Lujange yuko wapi?

Shahidi: Sifahamu

Wakili: Unafahamu kuwa alikuwa anaendelea kuwasiliana na Mbowe?

Shahidi: Sifahamu.

Wakili: Shahidi, hebu nisaidie mimi sijaelewa lengo la Mbowe. Hivi kulipua na kuchoma ni sawa?

Shahidi: Ni maneno mawili tofauti

Wakili: Umesema alitaka kulipua vituo vya mafuta na kuchoma masoko

Shahidi: Ni sahihi

Wakili: DCI alisema kulipua vituo vya kuuzia mafuta na masoko, Kingai alisema kulipua vituo vya mafuta na masoko na Urio anasema kulipua vituo vya mafuta na kulipua masoko, wewe unasema kuchoma masoko, haya maeneo yana ulinganifu?

Shahidi: Ni terminology

Wakili: Ulimwambia Jaji ni terminology?

Shahidi: Sikumwambia

Wakili: Jumanne Malangahe katika maelezo yake anasema kuchoma masoko?

Shahidi: Hapana lakini haibadili maana.

Wakili Kidando anasimama na kutoa hoja: Mheshimiwa Jaji pamoja na kwamba tumechelewa kutoa hoja lakini tuna tatizo na kwenye ulinganisho wa maelezo ya mashahidi.

Mashahidi wengine ukiondoa CP Boaz wengine wote walishatoa ushahidi.

Kifungu 164(1) (c), tunaona sasa kinachoingia kwenye ushahidi kinaingia isivyoruhusiwa.

Kibatala: Kwanza objection haina merit. Lakini wao wameshachelewa hivyo kifungu cha 164 hakiipi mamlaka mahakama kuondoa ushahidi ulioingia kwenye rekodi.

Tatu, shahidi mwenyewe amesema source ya information yake ni hizo statement.

Halafu hii ni cross examination kama nauliza kitu ambacho si sahihi mahakama yenyewe itaona, lakini mimi nashambulia investigation conclusion. Kwa kuwa nilikuwa nimeshafika mbali kwa hiyo naomba niruhusiwe kuendelea.

Jaji: Wakati shahidi anaanza kuulizwa maswali alisema anaomba atumie statement yake na upande wa mashtaka mliridhia.

Kwa namna ambavyo ameulizwa ameulizwa kuwa alikuwa na access ya nyaraka hizo.

Ni kweli hizi nyaraka haziko kwenye kumbukumbu, lakini katika mazingira hayo maswali aliyoulizwa shahid na namna alivyoyajibu haioni kama yanaweza kuondolewa.

Hivyo wakili aendelee kumuuliza

Wakili: Anasoma sehemu ya maelezo yake kisha anauliza:

Unaona kwamba hakuna mahali pa kulipua masoko?

Shahidi: Ni kweli sikuandika lakini kwenye maelezo huwezi kuandika kila kitu

Wakili: Ulimwambia Jaji hivyo?

Shahidi: Hakuna

Wakili: Ni kweli kwamba kwenye maelezo yako hakuna mahali ambako umeeleza hiyo tarehe 14 (Julai 2020) kuna kitu cha kipelelezi ulichokifanya?

Shahidi: Ni kweli

Wakili: Mheshimiwa Jaji naona ni saa saba kasoro dakika tano, naomba ahirisho tutaendelea baada ya break.

Mahakama imahirishwa kwa dakika 45

Mahakama imerejea baada ya mapumziko ya dakika 45.

Mawakili wa pande zote wameshajitambulisha na wakili wa utetezi Peter Kibatala anamuomba Jaji kumkumbusha sehemu alipoishia.

Kibalata: Shahid nikiwa nimeshika maelezo hayo naomba usome haya maeneno.

Shahidi amepewa maelezo yake ya onyo na ameanza kuyasoma

Shahidi: Baada ya kufungua jalada, afande Boaz alinielekeza niwe mpelelezi wa kesi hiyo.

Kibatala: Tukitaka kuona kisheria wewe na Sajenti Nuru mlikabidhiana kielelezo namba 19/2020 tunatakiwa kuangalia kwenye register? Ni sahihi.

Shahidi: Ni sahihi.

Kibatala: Pengine hata terehe ya makabidhiano tunaweza kukiona huko?

Shahidi: Ni sahihi.

Kibatala: Zaidi ya ushahidi wa Luten Denis Urio, wewe kama mpelelezi, una ushahidi gani mwingine uliofanyika kazi hadi kupata conclusion hizi?

Shahidi: Ni miamala ya fedha za Mbowe alizokuwa anawatumia watuhumiwa, Justine Kaaya ambaye alikuwa anamtumia taarifa Mbowe za Lengai Ole Sabaya na kupitia taarifa hizo ndizo zilizopelekea watuhumiwa wawili kukamatwa huko Moshi Kilimanjaro.

Shahidi: Baada ya hapo ndio nikaandaa jalada.

Kibatala: Maelezo ya onyo ya Justine Kaaya yako wapi ili tuweze kulinganisha hicho unachosema katika maelezo yake ya awali na maelezo ya nyongeza aliyoyatoa Julai 30, 2021?

Shahidi: Hatukuyaleta kwa sababu hayana umuhimu.

Kibatala: Kama maelezo ya onyo ya Justine Kaaya mgeyaleta Mahakama kama kielelezo tungepata nafasi ya kuyalinganisha?

Wakili Kindando wa upande wa mashtaka amesimama na kueleza kuwa maelezo ya onyo ya Justine Kaaya hayawezi kuletwa mahakamani kwa sababu Kaaya sio mshtakiwa bali ni shahidi.

Kidando: Na yangeweza kuleta mahakamani kama Justine Kaaya angekuwa mshtakiwa, lakini hakuna Sheria inayotutaka tuyalete maelezo ya onyo ya Kaaya mahakamani hapa.

Jaji: Nimesikia hoja za pande mbili, ni kweli shahidi kwa kuwa hajashtakiwa hakuna namna yoyote yanaweza kuletwa kwa sababu shahidi hakushtakiwa.

Jaji: Hivyo mahakama inaona wakili anayemuuliza shahidi ni sawa na mahakama itakuja kuyapima wakati inatoa uamuzi.

Kibatala: Ni sahihi tukiangalia maelezo ya onyo ya Adam Kasekwa, tutaona amekiri kukaa kikao na Justine Kaaya, Ling'wenya, Bwire na Mbowe?  Tutakuta kwenye maelezo ya onyo ya Kasekwa?

Shahidi: Ndio.

Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba maelezo ya onyo ya mshtakiwa Adam Kasekwa.

Kibatala anapewa maelezo hayo na kumpatia shahidi ayasome maelezo ya Adam Kasekwa.

Kibatala: Hapo kwenye maelezo ya Kasekwa kuna jina la Justine Kaaya?

Shahidi: Hakuna.

Kibataka: Ili kujiridhisha na maelezo ya onyo ya Kasekwa kuwa alikiri maelezo yake, kwenye kikao cha tarehe 26/7/2020 tutaona Kaaya alikaa kikao na Adam Kasekwa?

Shahidi: Hakuna.

Kibatala: Shahidi katika ushahidi wako wewe unasema washtakiwa walikamatwa Rau Madukani walikuwa kutekeleza mpango au walikuwa katika mpango

Shahidi: Walikuwa wanajiandaa kwenda kutekeleza mpango huo.

Kibatala: Kama gari ya Landcruiser ilikuwa sio ya muhimu kwanini uliandikia maelezo?

Shahidi: Kimya.

Kibatala: Kama mtuhumiwa Moses Lujenje hamkumpata, je mliviarifu vyombo vya usalama kuhusiana na yeye kutopatikana na mnajua huko alipo ana silaha gani?

Shahidi: Hatukusema.

Kibatala: Ni sahihi hata Lengai Ole Sabaya hamkumwambia kama kuna watu wanataka kumdhuru?

Shahidi: Ni sahihi.

 Kibatala: Ni sahihi Mbowe aliwatuma vijana wake waende kumdhuru Lengai Ole Sabaya kwa sababu anamsumbua hivyo anatakiwa apewe displine ila wasimuue, tukiangalia kwenye maelezo ya Ling'wenya kuna sehemu tutaona hayo?

Kibatala: Moja wapo ya motivation ya Mbowe kuwatuma vijana waende kumdhuru Salaya ilikuwa ni kwamba Sabaya alikuwa anataka kuiba kura?

Shahidi: Ndio kwa mujibu wa maelezo yake.

Kibatala: Nikuombe maelezo ya Ling'wenya?

Shahidi: Sawa

Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba kielelezo, maelezo ya onyo ya mshtakiwa Mohamed Ling'wenya.

Shahidi anapewa na kuangalia, kisha anasema hakuna sehemu yenye maneno hayo.

Kibatala: Shahidi nakupa maeneo tena ya Adamo Kasekwa, utafuta sehemu iliyoandikwa ' Tulienda kwenye kikao siku ya tarehe 25/7/2020 usiku wa saa tano halafu tukarudi'.

Shahidi: Nimeyaona.

Kibatala: Haya tusomee

Shahidi anasoma maelezo hayo.

Kibatala: Sasa suala la kumpiga Sabaya na kumpuliizia dawa yenye sumu, shahidi ulichukua hatua zaidi kufanya upelelezi?

Shahidi: Kimya

Kibatala: Ni kweli huyu Sabaya alishapatikana na kesi inayohusiana na masuala ya kutumia nguvu dhidi ya wananchi?

Shahidi: Hilo siwezi kulizungumzia.

Kibatala: Hutaki? Au

Shahidi: Sikufuatilia hiyo kesi.

Kibatala: Hivi Mbowe alipoongea na Luteni Urio, aliomba Urio amtafutia watu wa namna gani? Walinzi au wahalifu?

Shahidi: Walinzi.

Kibatala: Sasa Mbowe alianzisha mchakato wa kupata walinzi au wahalifu?

Shahidi: Wahalifu

Mahakamani: hahahaha

Kibatala: Halafu yeye (Mbowe) aliletewa nani?

Shahidi: Wahalifu.

Kibatala: Maelezo ya Luteni Urio aliandika nani?

Shahidi: Mimi

Kibatala: Wewe kama mpelelezi, unafahamu Adamu na Kasekwa baada ya kupewa hela na Urio wao walienda Hai? Ni Sahihi?

Shahidi: Ni sahihi.

Kibatala: Sasa Luten Urio anasema maelezo yake ya onyo uliyoandika wewe anasema ulikosema kwani baada ya kuwapa hela yeye, Adam na Lingw'enya walienda Dar es Salaam na sio Hai, Nani ndio yupo sahihi?

Shahidi: Nilichoandika ndio sahihi.

Kibatala: Sasa swali langu ni kwamba kuna mgongano au hakuna mgongano, au nikupe maelezo ya onyo ya mshtakiwa Adam Kasekwa na Mohamed Ling'wenya, uyasome?

Shahidi: Nipe nisome.

Shahidi amepewa maelezo hayo anasoma.

Kibatala: Sasa umesoma maelezo yote, je uliyafanyia kazi kama mpelelezi?

Shahidi: Ndio niliyafanyia kazi.

Kibatala: Sasa mtoa taarifa wenu anasema, baada ya kuwapa hela walielekea Hai, Sasa hapo kuna mgongano au hakuna mgongano?

Shahidi: Hakuna mgongano.

Kibatala: Hakuna mgongano kweli? Halafu shahidi wewe ni mtu mzima?

Wakati Kibatala anaendelea kumhoji shahidi, Wakili Kidando na Abdallah Chavula wa upande wa mashtaka wamesimama na kueleza mahakama kuwa shahidi ameshajibu maswali, lakini Kibatala bado anamtaka shahidi kujibu.

Kidando: Tunaomba Wakili ajielekeze kuuliza maswali mengine kwa sababu swali hili tayari shahidi ameshalijibu.

Kibatala: Mheshimiwa Jaji naona kaka yangu Chavula amesimama naona pia muda umeenda, hivyo anataka kuahirisha.

Kibataka: Sasa Mheshimiwa Jaji naomba kuahirisha kesi hii kwa sababu pia muda umeenda halafu bado nina maswali.

Jaji: Nilikuambia uondoe neno mtu mzima.

Kibatala: Mheshimiwa Jaji nilishaliondoa.

Kidando: Pamoja na hilo tunaomba Mahakama impe maelekezo ili kesho tena asije kuanza na hilo.

Kibatala: Mheshimiwa Jaji nimeshaliondoa neno mtu mzima kwenye mataamshi yangu.

Jaji: Kwa hiyo kwa sababu ya kuliondoa neno mtu mzima ndio sababu ya kuomba kuahirisha kesi hii?

Kibatala: Hapana Mheshimiwa Jaji, ni muda pia umeisha saizi ni saa 11 jioni kasoro dakaki tatu, naomba ikikupendeza tuahirishe hadi kesho kwa sababu bado nina maswali ya kumuuliza shahidi.

Jaji:  upande wa mashtaka mnakubaliana na hoja ya kuahirisha keis hii?

Kidando: Hatuna pingamizi.

Jaji: Kama upande wa utetezi walivyoomba na kuungwa mkono na upande wa mashataka, Naahirisha kesi hii hadi kesho tarehe 9/2/2022 saa tatu asubuhi itakapoendelea kesi hii.

Jaji: Nasiistiza shahidi kesho uje mahakamani na washtakiwa mtakuwa chini ya usimamizi wa magereza.

Nawatakiwa jioni njema.

High Court!!!!

Chanzo: www.mwananchi.co.tz
Related Articles: