Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Luteni Urio akana kuwekwa kuzuizini hadi sasa

Mbowepic Data Luteni Urio akana kuwekwa kuzuizini hadi sasa

Tue, 1 Feb 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Shahidi muhimu wa Jamhuri katika kesi ya ugaidi inayomkabili mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na wenzake watatu leo Jumanne Februari 1, 2022 amekana kwamba yupo kizuizini na analetwa mahakamani hapo chini ya ulinzi.

Shahidi huo wa 12 Luteni Denis Urio anakuwa ni shahidi aliohojiwa kwa muda mrefu na wakili wa utetezi ukilinganisha na mashahidi wengine wa Jamhuri waliotangulia.

Luteni Urio ambaye anaelezwa kuwa mtu wa kwanza kutoa taarifa polisi kuhusu madai ya mipango ya kutekeleza ugaidi inayodaiwa kufadhiliwa na Mbowe amehojiwa kwa siku tatu mfululizo tangu Ijumaa iliyopita.

Leo Luteni Urio amekana kuwekwa kizuizini na kwamba mama yake mzazi aliwahi kwenda kumuona akiwa kuzuizini.

Soma mahojiano kati ya Wakili Kibatala na Shahidi Luteni Urio

Leo Februari Mosi, 2022 Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi , itaendelea na usikilizaji wa kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu, wanaotuhumiwa kwa makosa ya ugaidi.

Advertisement Wakili wa utetezi Peter Kibatala ataendelea kumuhoji shahidi wa 12 wa upande wa mashtaka Luteni Denis Urio, kuhusiana na ushahidi wake alioutoa mahakamani hapo wiki iliyopita dhidi ya washtakiwa hao.

Jaji Tiganga ameshaingia katika ukumbi wa mahakama kwa ajili ya kuendelea na kesi.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Robert Kidando ambaye ni kiongozi wa jopo la upande wa mashtaka anatambulisha column yake na kiongozi wa mawakili wa utetezi Peter Kibatala nae anafanya utambulisho.

Kidando: Shauri linakuja kwa ajili ya kuendelea na ushahidi kwa shahidi kuhojiwa na upande wa utetezi nasi tupo tayari

Jaji: Upande wa utetezi?

Kibatala: Nasi tupo tayari Mheshimiwa jaji

Kibatala: Shahidi habari za tangu Jana

Shahidi: Nzuri

Kibatala:Uliwahi kufahamishwa kuwa kuliwahi kufanyika kesi ndogo mbili ndani ya kesi kubwa ya msingi?

Shahidi: Sifahamu.

Kibatala: Adamu na Lingw'enya walisema wewe ulikuwa ni sehemu ya watu waliokamatwa, ni sahihi?

Soma zaidi: Kibatala amng’ang’ania Luteni Urio kesi ya kina Mbowe

Shahidi: Nasikia kutoka kwako.

Kibatala: Uliwahi kukutana na mawakili wa Serikali ikiwemo Mr Kidando kabla ya kuja kutoa ushahidi mahakamani hapa?

Shahidi: Kwa maelekezo niliambiwa nieenda kuripoti kwa DCI ndio nikaletwa hapa.

Kibatala: Kwa maelekezo yako hujasema kama uliwahi kukamatwa na maafisa wa Polisi hasa  Jumanne Malangahe na Goodluck?

Shahidi: Sasa nitasemaje wakati sijakamatwa?

Kibalata: Relax shahidi

Kibatala: Katika ushahidi wako hujawahi kusema kuwa hujawahi kutifikishwa kituo cha Polisi cha Tazara tarehe 8 au 9 ya mwezi wa Saba, mwaka 2020?

Shahidi: Sijawahi kufikishwa

Kibatala: Pia hujawahi kusema Kama ulifikishwa kituo cha Polisi Mbweni katika tarehe hiyo.

Shahidi: Sijawahi kufikishwa kituo chochote cha Polisi, narudia tena mimi sijawahi kufika kituo chochote cha Polisi Mbweni

Kibatala: Wewe una ugomvi na Adamoo na? Lingw'enya?

Shahadi: Sijawahi kuwa na ugomvi nao.

Shahidi: Narudia tena sijawahi kufikishwa kituo cha Polisi Mbweni, mbona unaniwekea maneno mdomoni?

Kibatala: Shahidi usikasirike

Kibataka: Unafahamu sababu ya mimi kukuuuliza maswali kuhusu wapi unasali na paroko wako ni nani?

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Sasa baada ya kukamatwa Adamo na Lingw'enya na kuteswa walipohojiwa walikutaja kuwa wewe ndio uliwaunganisha kwa Mbowe na wewe ulikamatwa ni sahihi?

Shahidi: Sijawahi kukamatwa

Kibatala: Katika ushahidi wako ulimtaja komando aitwaye Gabriel Mhina?

Shahidi: Sifahamu

Kibataka: Una ugomvi na watu niliyokutajia?

Shahidi: Sina ugomvi nao

Kibatala: Afande Kingai aliwahi kukuambia kuwa kuna komando wengine walikamatwa?

Shahidi: Hajawahi kuniambia

Kibatala: Ex- Komando Halid alimuuliza Bwire nani aliyekuunganisha katika kazi hii ya ulinzi? Akasema ni wewe ni sahihi?

Shahidi: Halid ni nani? Mimi simfahamu Halid na wala hapa katika ushahidi wangu sijamtaja

Kibatala: Huyo halidi pia, baada ya kukutafuta kwenye mtandao wa Facebook, ulimwambia utamuunganisha na kazi ya ulinzi migodini, ni sahihi?

Shahadi: Simfahamu Halidi wala sina Access huko migodini

Kibatala: Unamfahamu baba yako mdogo mzee John Urio?

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Unafahamu mke wako ndio aliyefanya juhudi za kuitoa gari yako Rav4 rangi ya silver pale kwenye parking na kwenda kuipark Kihonda ni Sahihi? Kwa sababu wewe mpaka sasa upo chini ya ulinzi, ni sahihi?

Shahidi: Sio sahihi? Gari haijawahi kuzuiliwa na hata nakuja hapa kutoa ushahidi gari nilipaki.

Kibatala:Tukitaka kuangalia upo kwenye active duties  kwenye Military Service tunatakiwa kuangalia nyaraka zipi?

Shahidi: Ni kuangalia identity card  na kuhakiki kwa mwajiri wake.

Kibatala:Ni kweli ili kudhibitisha kuwa wewe hujafukuzwa kazi unatakiwa kuangalia duties Roster?

Shahidi: Ni kweli

Kibatala: Kama tunafikiria kuiomba ahirisho kwa Mahakama kwa ajili ya kukupa nafasi ya kufuatilia nyaraka ya udhibitisho kuwa wewe upo kazini,  unaweza kufahamu mchakato huo utachukua siku ngapi? Ili upate nyaraka hiyo?

Shahidi: Sijui itachukua muda gani.

Kibatala: Ni sahihi mtoto wako mdogo Jackson wakati anazaliwa wewe ulikuwa mafichoni umefichwa?

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Pius Hilla ananyanyuka na kumueleza Jaji kuwa suala la mtoto, lisiwekwa kwenye rekodi kwa sababu hajalitolea ushahidi.

Jaji: Sawa

Shahidi: Hili swali nimeshakujibu wakili halafu wewe ni wakili msomi....Sasa sitaki uniulize tena? Sawa? Wewe ni wakili msomi? Alaah

Mahakama: Kichekoo hahaha hahaha hahaha

Kibatala: Shahidi hebu Relax basi

Shahidi: Mimi nimelax

Kibatala: Ni kweli shahidi hata mama yako mzazi ilibidi aje kukuona ukiwa kizuizini?

Shahidi: Narudia tena sijawahi kuwekwa kizuizini.

Kibatala: Ni kweli au sio kweli kwa kuwa upo kizuizini kwa sasa unasindikizwa na maofisa usalama wenye silaha?

Shahidi: Kwanza naomba uondoe neno kizuizi kwa sababu unanichafulia...mimi sijawahi kuletwa na maofisa usalama wenye silaha.

Shahidi: Mimi nakuja na mawakili wangu (wa upande wa mashtaka) ambao hunipitia hotelini na magari yao.

Kibatala: Kwa magari ya Serikali? Usinitajie namba zake kwa sababu ni masuala ya kiusalama.

Shahidi: Labda unipe task nikayakague

Kibataka: Hivi hizo dhana mbili zinaoana kweli?

Shahidi: Dhana zipi?

Soma zaidi:Luteni Urio: Sikuona umuhimu kurekodi mazungumzo yangu na Mbowe

Kibatala: Ulisema uliripoti kwa DCI ndio ukaletwa hapa mahakamani na leo umetueleza kuwa unapitiwa na mawakili wako kuletwa hapa mahakamani.

Shahidi: Hujanielewa ...siku ya kwanza nililipoti kwa DCI na baada ya hapo nikawa nachukuliwa na mawakili wa Serikali kuletwa mahakamani.

Kibatala: Shahidi Ndio utaratibu wako wa kila siku unapitiwa na mawakili wako?

Shahidi: Ndio wenyeji wangu.

Kibatala: Okay

Shahidi: Karibu

Kibatala: Unafahamu DCI, IGP na wengine wamehamia Dodoma?

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Sasa unafahamu kwa sababu ofisi mama ya DCI imehamia Dodoma?.

Shahidi: Siwezi kuzungumzia ofisi ya DCI

Kibataka: Shahidi unafahamu kitu kiitwacho Civico?

Shahidi Nafahamu.

Kibatala: Cimico ni Civic and Military Coordination?

Shahidi: Ndio,

Kibatala: Hii maana yake ni mahusiano ya kubadilishana taarifa kati ya taasisi za Jeshi na jamii.

Shahidi: Ni sahihi.

Kibatala: Unafahamu Presence Patrol?

Shahidi: Nafahamu.

Kibatala: Shahidi ni sahihi zimeshawahi kufanyika Presence Patrol hapa Tanzania inapofanyika uchaguzi au kunapotokea matukio tata?

Shahidi: Sifahamu.

Kibatala: Shahidi limetoka tishio la kuripua madaraja makubwa hapa nchini, ni kweli Jeshi letu haliwezi kufanya Presence Patrol?

Shahidi: Sijaelewa unaenda wapi.

Kibatala: Nisikilize swali langu.

Shahidi: Nimelielewa swali.

Kibatala: Shahidi nakuuliza spry ya sumu, je Uliwahi kuiongelea katika ushahidi wako?

Shahidi: Sijasema...halafu usinilishe maneno mdomo..vipi wewe rafiki yangu bwanaa...hebu relax

Kibatala: Una mfahamu Bwire.

Shahidi: Namfahamu.

Kibatala: Unafahamu jukumu la Bwire lilikuwa ni kwenda kumlinda Tundu Lissu?

Shahidi: Hata raisi mwenyewe halindwi na Komando.

Kibatala: Unafahamu Tundu Lissu Kama mgombea urais alitaka mlinzi Maalum kwa kuwa alishashambuliwa na risasi?

Shahidi: Kila mgombea anapewa mlinzi

Kibatala: Unafahamu mgombea urais anapewa walinzi wangapi?

Shahidi: Sifahamu.

Kibatala: Unafahamu Tundu Lissu alishambuliwa kwa risasi kwenye viwanja vya bunge ?

Shahidi: Sifahamu.

Kibatala: Unafahamu hadi leo Jeshi la Polisi halijakama mtu hata mmoja, alihusika na kumshambulia Lissu.

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Ni kosa mtu kujiimalisha kwa kuwa na walinzi wake?

Shahidi: Sio kosa

Kibatala: Unafahamu Ben Sanane alikuwa ni msaidizi binafsi wa Mbowe amepotea na hajajulika alipo hadi leo?

Shahidi: Sifahamu.

Kibatala: Kwa mujibu wa kanuni za Jeshi na miongozo ya jeshi,ofisa wa Jeshi anaruhusiwa kuwa na mahusiano na kiongozi wa chama cha upinzani? Ni kosa au sio kweli?

Shahidi: Si kosa kama ni mahusiano ya Kawaida lakini sio ya siasa.

Kibatala: Ulimfahamu ama hufahamu ...moja wapo ya majukumu ya Bwire na Lingw'enya  ni kumsindikiza Mbowe kwenye mikutano yake ya kisiasa  ikiwemo ule uliofanyika ukumbi wa kanisa Katoliki.

Shahidi: Sifahamu, nachojua walienda kutekeleza uhalifu.

Kibatala: Unafahamu Julai 26, 2020 Adamoo na Lingw'enya siku hiyo walipanda magari ya Chadema yenye nembo za M4C kwenda kwenye mikutano?

Shahidi: Walishawishiwa kuingia katika uhalifu na kukataa mawasiliano na mimi.

Kibatala: Kabla ya kukataa mawasiliano baina ya Adamoo na Lingw'enya, hukuwauliza?

Shahidi: Waliniambia wanataka kuajiliwa.

Soma zaidi: Shahidi muhimu kuhojiwa siku ya tatu kesi ya kina Mbowe

Kibatala: Big answer

Shahidi: Ndio ulikuwa unataka hilo.

Mahakama: Kicheko.

Kibatala: Shahidi ulipoongea na Mbowe alijicommit akisema anapanga kushiriki uchaguzi?

Shahidi: Alisema chama changu kimejipanga kuchukua dola

Shahidi: Alisema chama changu kimejipanga kuchukua dola kwa njia yoyote.

Kibatala: Unafahamu chama cha Chadema kilisimamisha wagombea katika ngazi zote?

Shahidi: Sifahamu.

Kibatala: Unafahamu alifanya kampeni?

Shahidi: Sikufuatilia sana.

Kibatala: Hata kama ulifuatilia kwa mbali ulijua?

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Unafahamu zile pesa ulizotumiwa na Mbowe zilikuwa ni za Mbowe au za chama?

Shahidi: Sifahamu.

Kibatala: Unafahamu jukumu la kutafuta walinzi ni jukumu lililoidhinishwa na chama?

Shahidi: Sifahamu.

Soma zaidi:Luteni Urio asoma mawasiliano yake na Mbowe mahakamani

Kibatala: Mtu alishtakiwa discharge ana mipaka ya kufanya kazi?

Shahidi: Ili mradi afuate sheria.

Kibatala: Unafahamu hata kina Diamond Platinum ana bordguard?

Shahidi: Sifahamu.

Kibatala: Shahidi naomba utusaidie kwanini ulichagua kukutana na Moses Lijenje eneo la Morogoro na sio sehemu nyingine?

Shahidi: Kwa sababu ndio center

Kibatala: Center ya Nini?

Shahidi:  kwa sababu ndio sehemu ya karibu.

Kibatala: Uliwahi kufahamu Mbowe alisafiri nje ya nchi?

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Unamfahamu Godless Lema?

Shahidi: Namsikia

Kibatala: Unafahamu Lema anaishi uhamishoni kwa sababu ya matishio ya maisha ya usalama wake?

Shahidi: Sijui Kama anaiishi uhamishoni kwa sababu ya matishio ya maisha yake.

Kibatala: Unafahamu Kama Tundu Lissu anaishi uhamishoni kwa sababu ya matishio ya usalama wa maisha yake?

Shahidi: Sijui kama ni uhamishoni au amekwenda kitalii.

Soma zaidi: Urio aeleza alivyomtafutia Mbowe makomandoo na kuahidiwa cheo

Kibatala: Unafahamu kama hawa vijana wasingekamatwa, Lissu asingeondoka hapa nchini?

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Unafahamu kama hawa vijana wasingekamatwa, Lema asingeondoka hapa nchini?

Shahidi: Sifahamu.

Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba kuishia hapa...yangu ni hayo tu.

Kibatala amemaliza kumhoji Luteni Urio na sasa upande wa mashtaka wanatakiwa kumfanyia re- examination ( mawakili wa Serikali kumuuliza shahidi  kwa ajili ya kupata ufafanuzi kuhusiana na ushahidi alioutoa wakati anahojiwa na mawakili wa upande wa utetezi).

Wakili Chavula: Hebu ifafanulie mahakama ni Kwanini ulimwambia Freeman Mbowe atumie wakala au msaidizi wake kutuma pesa bada ya kutumia namba yake ini salama zaidi

Shahidi: Nilimwambia atumie Wakala au msaidizi wake ili niweze kuwini Trust.

Wakili: Kuna swali uliulizwa kuhusu kukamatwa kwa kina Bwire ukasema hukushangaa ulivyosikia wamekamatwa.

Shahidi: Sikushangaa kwa sababu walinipa taarifa wakiwa wameshapanga.

Wakili:  Licha ya wewe kuwa na cheo na kumwambia Freeman Mbowe kuwa huna cheo hebu ifafanulie mahakama kwanini ulisema jibu hilo wewe ulikuwa mkweli.

Shahidi: Kwa mara ya kwanza ndio nakutana na Freeman Mbowe anataka kujua cheo changu nilimjibu hivyo kwa ajili ya usalama.

Wakili: Ulisikika uliieleza mahakama ukisema uliwaambia washtakiwa wakafanye kazi ya ulinzi na kuambatana nae katika kuchukua dola ulikuwa unamaanisha nini

Shahidi: Dhumuni kubwa la Mbowe kuwahitaji hao watu ilikuwa ni kwa ajili ya kukata miti, kuchoma vituo vya mafuta pamoja na kumdhuru viongozi.

Wakili Chavula:Mheshimiwa Jaji ni hayo tu.

Wakili Kidando: Mheshimiwa Jaji hatuna shahidi mwingine kwa leo tunaomba ahirisho la siku mbili Shahidi tuliyekuwa tunategemea hadi jana tulikuwa hatujampata alikuwa kasafiri.

Katika mazingira hayo hata kama tutakuwa hatujampata tutaendelea na Shahidi mwingine.

Ni hayo tu.

Wakili Kibatala: Bila kuwakosea wenzetu hatujaona sababu ya kuahirisha katika mashahidi kadhaa waliotajwa hata kibinadamu yenyewe tunaomba wenzetu kesho walete Shahidi kwa kuwa tumebrek mapema muda wa kumuandaa upo.

Wakili Kidando: Tumewasikia wenzetu kuita mashahidi hata kama ni wengi kiasi gani inacost kusubiri na wengine hawapo Dar es Salaam.

Jaji: Tujikite hiyo hoja ya siku mbili hao wamesema kwa nini iwe hadi Ijumaa.

Wakili Kidando:  Hadi tunaingia hapa mahakamani alikuwa hajasafiri ili tusipoteze resource ndio maana nikasema hadi Ijumaa tarehe 4.

Jaji: Tukitolea uwamuzi hoja iliyoletwa ya kuleta mashahidi hadi Ijumaa tarehe 4 tunajua kuleta Shahidi mahakamani ni jukumu la upande wa mashtaka.

Mahakama imeona kuja mahakamani kama hakuna shahidi haina maana hivyo ninaelekeza upande wa mashtaka kuleta Shahidi siku ya tarehe 4, 2022 na washtakiwa watabaki chini ya uangalizi wa Magereza.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz
Related Articles: