Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kibatala amng’ang’ania Luteni Urio kesi ya kina Mbowe

Mbowe Mpya Piccc Data Kibatala amng’ang’ania Luteni Urio kesi ya kina Mbowe

Mon, 31 Jan 2022 Chanzo: mwananchidigital

Kiongozi wa jopo la utetezi katika kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu, Wakili Peter Kibatala leo Jumatatu Januari 31,2022 ameendelea kumhoji shahidi wa 12 wa upande wa mashtaka ikiwa ni siku ya tatu mfululizo shahidi huyo kuhojiwa na upande wa utetezi huku mahojiano yakitarajiwa kuendelea kesho.

Shahidi huyo, Luteni Denis Urio wa upande wa mashtaka ameendelea kuhojiwa na Kibatala katika hatua ya udodosaji.

Mchuano baina ya Luteni Urio na mawakili wa utetezi ulianza Alhamisi, baada ya kumaliza kutoa ushahidi wake wa msingi aliouanza Jumatano ya wiki iliyopita huku akiongozwa na mwendesha mashtaka, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Abdallah Chavula katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.

Leo Jumatatu Kibatala aliendelea kumhoji Luteni Urio kuanzia asubuhi mpaka jioni Jaji Joachim Tiganga alipoahirisha kesi hiyo mpaka kesho Jumanne ambapo Kibatala ataendelea kumhoji shahidi huyo.

Kabla ya Jaji Tiganga kuahirisha kesi hiyo, Kibatala alitoa hoja ya kuomba kesi iahirishe mpaka kesho akidai kuwa bado ana maswali mengi, hoja ambayo iliunga mkono na upande wa mashtaka.

Ifuatayo ni mahojiano baina ya wakili wa utetezi Peter Kibatala na shahidi Luteni Urio

Jaji Joachim Tiganga ameingia mahakamani na kesi inatajwa na karani

Kiongozi wa jopo la Waendesha mashtaka Wakili wa Serikali Mwandamizi, Robert Kidando anafanya utambulisho.

Sasa kiongozi wa jopo la mawakili wa utetezi, Peter Kibatala anafanya utambulisho wa jopo lake.

Jaji Tiganga anawaita washtakiwa kwa kutaja namba zao kwenye kesi kuanzianza kwanza hadi wa nne na wote wanaitika.

Wakili Kidando: Shauri linakuja kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa na Shahidi wetu yupo.

Wakili Kibatala: Nasi Mheshimiwa Jaji tuko tayari

Sasa Wakili Kibatala anaanza kumhoji shahidi. Shahidi huyo, Luteni Denis Urio wa upande wa mashtaka.

Wakili: Mhe Urio good morning

Shahidi: Morning too

Wakili: Naendelea kukuuliza maswali. Ukiacha tukio hili umewaji kukutana na tikio longine kubwa la kigaidi kama hili?

Shahidi: Hebu rudia

Wakili: Ulishawahi kukutana na mtu mnayefahamiana akakwambia matukio mazoti kama haya au ni mara yako ya kwanza?

Shahidi: Ni sahihi

Wakili: Ulisama huna matatizo ya kumbukumbu?

Shahidi: Sahihi

Wakili: Sasa Shahidi inawezekana vipi ukasahau tarehe muhimu kama hizi za tarehe ya kukutana na Mbowe kukwambia masuala haya na tarehe ya kwenda kwa DCI na hasa Askari mkubwa kama wewe mwenye cheo cha Luteni?

Shahidi: Ni mara ya kwanza kupata taatifa kama hizo kwa Mheshimiwa Mbowe hivyo sikuamini mara moja lakini angekuwa na rekodi kama hizo ningejua.

Wakili: Vipi kukumbuka kwenda kwa DCI?

Shahidi: Sijakumbuka kwa sababu si duty yangu ya kufanya uchunguzi.

Wakili: Sawa, unaweza kusaidia kwa nini hata DCI katika maelezo yake hakumbuki?

Shahidi: Siwezo kumjibia DCI

Wakili: Unafahamau au hufahamu?

Shahidi: Sifahamu

Wakili: Je kwa nini hata ACP Kingao ambaye alikuwepo naye hafahamu?

Shahidi: Sijui kwa nini hajui

Wakili: Na kuhusu ofisa mwingine wa Polisi, Afande Swila naye hafahamu?

Shahidi: Sifahamu

Wakili: Wewe unaona hii hali ni ya kawaida?

Shahidi: Nilikwenda ofisi ya mtu sasa siwezi kumlazimisha kutake note.

Wakili: Unafahamu kwa nini maelezo yako yaliandikwa karibu mwezi mmoja baadaye badala ya kuwa ya kwanza?

Shahidi: Sifahamu

Wakili: Huoni kwamba ni busara maeelezo ya mtu muhimu kama wewe mtoa taarifa kuandikwa mapema?

Shahidi: Sielewi utaratibu wake yeye kama anaona inafaa

Wakili: DCI alikufafanulia kwa nini maelezo yako hayakuchukuliwa mapema?

Shahidi: Hawakunifafanulia

Wakili: Tarehe 11/8/2020 ndio ulikwenda kwa Inspekta Swila kuandika maelezo yako ya tukio zito la kupanga njama na makomandoo, Swila alikufafanulia?

Shahidi: Hakunifafanulia

Wakili: Tukiamini kwamba tuhuma zilitungwa kwanza ndipo wakatafutwa washtakiwa tunakuwa tunakosea?

Shahidi: Utakuwa unakosea.

Wakili: Katika kikao chenu wewe DCI na Kingao mliwahi jadili mbinu ya kumtuma Askari wa Polisi aende kwa Mbowe ajifanye ili kupata ushahidi kwa sababu wao wako trainees na wana vifaa?

Shahidi: Mimi sikuwahi kujadili

Wakili: Ni kweli kwamba katika ushahidi wako kuwa Mbowe alisema anataka kuchukua dola kwa namna yoyote na gharama yoyote kwenye uchaguz wa 2020

Shahidi: Ni kweli

Wakili: Na Bado unasisisitiza kwamba kwa hizo factor wewe hukuwa ni mwanajeshi kazini na wanaotakiwa Ni X Commandos bado jeshi halikujitaji kuchukua hatua?

Shahidi: Kwa sabau ni taarifa zilizotolewa kwenye uraia kwa hiyo bado zingerudi polisi maana ni taarifa ambazo hazikuwa sahihi.

Wakili: Unamfahamu aliyekuwa Luten Shimbo?

Shahidi: Namfahamu

Wakili: Kwamba Oktoba 13, 2010 Luten Shombo alisema kuwa uchaguzi unakuwa wa amani na kwamba Jeshi liko tayari kuchukua nchi kama kungetokea uvunjifu wa amani

Shahidi: Sikuwahi kusikia

Wakili: Kwa nini Hamkuona kwa taarifa hizo ambazo zinawahusisha makomandoo mngetuma makomandoo kuwa kama mamluki?

Shahidi: Kwanza Mbowe alikuwa hapokei simu na aliomba picha zao ili afanya research kama wako kazini.

Wakili: Kwa hiyo Freeman Mbowe ana mbinu za kufanya cross checking za Askari?

Shahidi: Ndio, kwa nini alitaka picha zao, kwa nini alitaka kujua umri wao

Wakili: Katika ushahidi wako ulisema Mbowe ana access na mtu mwingine jeshini?

Shahidi: Sikusema

Wakili: Kwa hiyo ni kweli kwamba kuna mambo ulikuwa huyafahamu hujui kama Mbowe alikuwa na plan A na B?

Shahidi: Ndio

Wakili: Unasema hukuwa na uhakika kama Mbowe alikuwa na plan A na B na Mbowe alikuwa na trust na wewe ulimhoji kama alikuwa na mtu mwingine ambaye alikuwa ameshamu-approach?

Shahidi: Sikumhoji

Wakili: Kwa assessment yako alikuwa anakuamini?

Shahidi: kuwa alikuwa ananiamini Mimi peke yangu?

Wakili: Na unasema alikuahidi cheo Kikubwa jeshini kama?

Shahidi: Kwa mawazo yake yeto, Mbowe hawezi kunipa cheo

Wakili: Baada ya kuachana na Mbowe mawazoni mwako ulikuwa umeshamkubalia au kumkatalia?

Shahidi: Kumkatalia

Wakili: Na kweli wakati anakwambia ulikuwa unamsikiliza tu na kwawmba ngoja amalize tu nakwenda kutoa taarifa?

Shahidi: Kuna hatua…

Wakili: Akili ya kawaida ya Luteni haikuweza kum-probe ili iujua huyu anapanga kulipua vituo vya mafuta au ni viongozi gani?

Shahidi: Kwa akili ya kawaida hata kama ni wewe ukishaanza kumdodosa anastuka.

Wakili: Utakubaliana na Mimi kwamba neno lako wewe dhidi ya neno la Mbowe na hakuna ushahidi wa sauti wala hamkutuma decoy?

Shahidi: Ndio maana tulituma hao vijana

Wakill: Hawa Ni washtakiwa kwani hawa ni mashshidi wenu?

Shahidi: Waliiingia kwenye uhalifu wenyewe

Shahidi: Unakumbuka lini uliongea na Ling'wenya?

Shahidi: Sikumbuki

Wakili: Ni kweli kwamba mzee Ling'wenya alikuwa aataka umwachia mwanaye kuhusu hiyo kazi kutokana na historia ya yale yaliyotokea jeshini?

Shahidi: Sifahamu

Wakili: Una ugomvi na mzee Ling'wenya mpaka akutungie hayo?

Shahidi: Sitahamu na wala sijawahi kumuona

Wakili: Unatajambua kuwa mzee Ling'wenya moyo wake unavuja damu kwa haya anayopitia kwa mwanaye uliyemuomba kuwa unamtafutia kazi ?

Shahidi: Sifahamu, kwani mwanaye aliambiwa kwamba akashiriki uhalifu?

Wakili: Alipokuuliza kuhusu mwanaye kukamatwa ulimpa ushirikiano gani?

Shahidi: Nilimwambia aongee na bosi wake.

Wakili: Ulimweleza mzee Ling'wenya ukweli kwamba Mbowe ana mipango ya ugaidi kwa hiyo tunataka kumtumia mwanao ili kupata ushahidi?

Shahidi: Sikumwambia

Wakili: Umeshawahi kusikia neno kumtoa mtu kafara?

Shahidi: Nafahamu

Wakili: Siku ya kwanza nilikuuliza maswali mengi kuhusu kwenda kanisani ukasema wewe ni Mkristo, Unamfahamu Daniel kwenye Biblia?

Shahidi: Namfahamu

Wakili: Unafahamu walichomfanyia?

Shahidi: Nafahamu walimtupa kwenywe tundu la Simba

Wakili: Unafahamu kwanza walimuingiza kwenye mtego kwa kumwambia atunge sheria, Mkristo mwenzangu huoni kuwa hicho ulichomfanyia mzee Ling'wenya kinafafana na hicho alichofanyowa Daniel?

Shahidi: Ni tofauti kabisa

Wakili: Na Mkristo mwenzangu moyo wako uko sawa tu?

Shahidi: Sawa kabisa

Wakili: Unafajamu mzee Ling'wenya ametumikia nchi hi bila doa?

Shahidi: Sifahamu

Wakili: Ni mazingira gani kiongozi anaweza kuondoka na kuwaacha askari wake

Shahidi. Huwezi kukaa sehemu moja na wafuasi wako wafuasi wanatakiwa kukaa mbele na kiongozi nyuma

Wakili. Unafahamu Adam Kasekwa aliachishwa kazi kwa kupata tatizo la kisaikolojia

Shahidi. Hana historia hiyo

Wakili. Kwenye maelezo mliyoleta mnasema ana historia hiyo

Shahidi. Kwani ameleta cheti cha daktari

Wakili. Ulifahamu sababu mahususi ya Ling'wenya kuachishwa kazi

Shahidi. Kwa utovu wa nidhamu

Wakili. Kwa kuwa uliwasiliana na Bwire unafahamu ni maeneo gani mahususi walitembelea kwaajili ya kumdhuru Sabaya

Shahidi. Bwire hakuniambia

Wakili: Unafahamu allegation ilikuwa ni kumdhuru Sabaya kwenye maeneo hayo

Shahidi: Aliieleza in breif lakini hakuniambia ni maeneo gani

Wakili. Nani aliyetumwa kumtafuta Mbowe ni nani

Shahidi. Ni mimi

Wakili. Mbowe aliomba polisi wamtafutie vijana

Shahidi: Hakuomba

Wakili: Ni kweli uliandika maneno hayo katika maelezo yako

Shahidi: Ni kweli

Wakili: Polis walikuwa na mawasiliano na Bwire

Shahidi; Hawakuwa nayo

Wakili: Nani alikuwa anaaminiwa na Bwire na Adamoo

Shahidi: Ni mimi

Wakili: Kuna msiri alikuwa anawapa wakina Kingai taarifa na kueleza walivyovaa ni wewe

Shahidi: Sio mimi

Wakili: Kingai aliwahi kukwambia kuna msiri wao mwingine zaidi yako

Shahidi: Hapana

Wakili: Kuna mtu mwingine alikuwa anawafahamu kadri waeleze walivyokuwa wamevaa

Shahidi: Sifahamu

Wakili: Unafahamu walichokuwa wanafanya pale Rau Madukani

Shahidi: Sifahamu

Wakili: Unafahamu Ling'wenya ana dada yake pale Rau madaukani walikuwa wameenda kumsalimia

Shahidi: Sifahamu

Wakili: Unafahamu Ling'wenya ana dada yake anaishi Sakina Arusha

Shahidi: Haikuwahi kuniambia

Wakili: Kati maelezo yako uliandika ulimpa Kingai namba za simu ili aweze kuwa fuatilia

Shahidi. Ni sahihi

Wakili. Wakati unaaongozwa na wakili uliongelea kuwa ulimpa Kingai namba za simu

Shahidi. Sikuongelea

Wakili. Ni muhimu au sio muhimu

Shahidi. Ni muhimu

Wakili. Unafahamu maana yake kuzungumzia suala la namba ya simu

Shahidi. Sifahamu

Wakili. Unafahamu nama ndugu walivyohangaika kuwatafuta ndugu zao kwenye vituo vya polisi na hospitali

Shahidi. Sifahamu

Wakili: 11/8/2020 uliandikishwa maelezo na kumkabidhi simu zako wakati Swilla anachukua simu yako alikuruhusu kutoa line

Shahidi. Ni sahihi

Wakili. Ulimwambia Jaji kuwa uliondoka na simu line yenye mawasiliano yako

Shahidi: Kulikuwa na line mbili

Wakili: Line ya Vodacom ulimwambia Jaji tarehe 12 uliirusha

Shahidi: Nilimwambia

Wakili: Hiyo nakala ya makabidhiano ya line ya voda ulikuja nayo

Shahidi: Sikujua kama itahitajika mahakamani

Wakili: Tukiomba tukague simu kama line ipo?

Shahidi. Vyovyote itakavyowezekana

Wakili. Mheshimiwa Jaji naomba kielelezo namba 34

Wakili Kibatala anampa Shahidi simu aiwashe ili wakague laini iliyopo.

Shahidi: Hakuna line hata moja

Wakili: Unajua maana ya kiapo chako

Shahidi: Nafahamu

Wakili: Unajua ukweli na uongo unapimwa kwa vitu vidogo vidogo kama hivi

Shahidi: Nafahamu

Wakili:Wakati unaamkabidhi Inspekta Swilla simu ilikuwa na line

Shahidi: Ndio ya Airtel

Wakili: Iko wapi

Shahidi: Sifahamu

Wakili: Ushahidi wako wa mdomo ulimkabidhi Swilla simu tatu utaungwa mkono na nini

Shahidi: Kwa sababu ziko hapa

Wakili: Unafahamu simu hizi tatu ni za muhimu kwa kuwa zilikuwa na mawasiliano flani

Shahidi: Nafahamu

Wakili: Ulimwambia Jaji simu mbili ulizozifuata uliziacha kwa nani

Shahidi: Nilimwambia

Wakili: Ulimwambia uliziacha chini ya uangalizi wa nani

Shahidi: Sikumwambia

Wakili: Unafahamu ni kwanini kataika maelezo ya Inspekta Swilla hazungumzii simu tatu

Shahidi: Sihitaji kufahamu

Wakili: Unafahamu Freeman Mbowe alikuwa na kaka mwenye cheo kikubwa jeshini na Rais Magufuli alihudhuria Msiba huo

Shahidi: Nilisikia

Wakili: Unataka tuamini Mbowe alimuacha kaka yake wa damu akakutafuta wewe

Shahidi: Alishastaafu

Wakili: Wewe na General nani anafahamu watu wengi zaidi

Shahidi: Yeye

Wakili: Unasema ulishangaa mara ya kwanza Mbowe kukupiga simu

Shahidi: Ndio

Shahidi: Unafahamu mtu kuwa na mawasiliano yako unaweza kulalamika

Shahidi: Mimi sio mtu wa muhimu

Wakili: Unafahamu mtu kukusumbua unaweza kulalamika

Shahidi: Sifahamu

Wakili: Ulitoa taarifa

Shahidi: Sikutoa taarifa

Wakili: Katika maelezo yako uliandika ulikuwa na ukaribu na Mbowe kwa kuwa ni kabila moja

Shahidi: Ni sahihi

Wakili: Nini kilikupa comfort hadi ukaendelea kuwasiliana naye

Shahidi: Mbowe ni Mbowe na Chama ni Chama

Wakili: Katika maelezo yako ulitenganisha

Shahidi: Sikutenganisha

Wakili: Unasema ulitumiwa 500,000 ukatoa 300 000 ukabakiwa na 200,000

Shahidi: Ni sahihi

Wakili: Unakumbuka ulichoandika katika maelezo yako

Shahidi: Nakumbuka

Wakili: Katika maelezo yako umesema ulipopokea ulizitoa zote

Shahidi. Hapana sikuzitoa

Wakili. Unakubaliana na mimi ulitoa 300000 na 200000 zikabaki kwenye simu

Shahidi. Ni sahihi

Wakili. Uliambiwa maana ya haya maelezo

Shahidi: Sikuambiwa

Wakili: Hakuna mahali uliposema hii hela zote ulizitoa mfukoni

Shahidi: Ni sahihi

Wakili: Utakubaliana na mimi ulichokisema na kilichaoandikwa vinatofautiana

Shahidi. Ni sahihi

Wakili: Ulimwambia Jaji 40000 ilienda wapi?

Shahidi: Sikumwambia

Wakili: Katika maelezo yao wanasema uliwapa Sh 87, 000 kila mtu?

Shahidi: Sikumpa mmoja mmoja hela

Shahidi: Kwahiyo katika haya maelezo na unacho sema wewe ni tofauti

Shahidi: Ni tofauti

Wakili: Unakubali au unakataaa jumla ni Sh174, 000

Shahidi: Amount hiyo siwezi kuifahamu

Wakili: Ushahidi huu na wako unatofautiana?

Shahidi: Unatofautiana

Wakili: Fedha ulizotumiwa na Mbowe ilikuwa kuwagharamia nauli zao za kuja Morogoro

Shahidi: Ni sahihi

Wakili: Naomba nikusumbue tena Shahidi nisaidie kuwasha kielelezo namba 34 uende kwenye meseji ambazo ulizisoma

Shahidi: Tayari

Wakili: Ni kweli ulisema Mbowe alikuambia umtafutie makomandoo wasiokuwa na kikomo

Shahidi: Hakuniambia idadi

Wakili: 20/7/2020 meseji inasema idadi ni watatu au wanne

Wakili: Hebu isome kwanza

Shahidi: Kaka wale mtu tatu au nne ni muhimu siku zimeisha

Wakili: Hapa anataja mtu tatu au nne

Shahidi: Ni sahihi

Wakili: 20/7/2020 saa 2:3 hii meseji nani alituma

Shahidi: Mimi nilituma kwenda kwa Freeman Mbowe

Wakili: Hii ilituma kwa namba gani

Shahidi: Mtandao wa Telegram

Wakili: Ili iweze kusajili mtandao wa telegram si lazima uwe na simcard

Wakili: Ulitumiwa namba gani msomee Jaji asikie

Shahdi: 1130138344

Wakili: Imeandikwa owner Denis Urio

Wakili wa Serikali Mwandamizi Pius Hilla. Sio nia yetu kusimama Wakili kamwambia asome Shahidi kasoma lakini wakati anataka kutoa ufafanuzi Wakili hataki.

Wakili Kibatala: Mheshimiwa Jaji hiyo namba wameileta wao hawakutoa ufafanuzi anataka kufanya submission watatakiwa wamuulize Shahidi kwenye re examination

Jaji: Kama nimemsikia vizuri Kibatala anamuuliza Sahahid kama anaifahamu hiyo namba kabla ya kujibu akawa anataka kutolea ufafanuzi lakini kwenye cross examination shahidi anatakiwa kujibu kile anachoulizwa.

Wakili Kibatala: Hiyo namba unafahamu

Shahidi: Sifahamu

Wakili: Kuna mtu alikuongoza kufafanua hiyo namba

Shahidi: Hakuna

Wakili: Unafahamu application inaitwa Freeman sms

Shahidi: Sifahamu

Wakili: Kuna mtu alikuongoza au kukuuliza kama unafahamu free sms

Shahidi: Hakuna

Wakili: Simu yetu bado ina chaji

Shahidi: Ndio

Wakili: Kuna sehemu yoyote Mbowe anakwambia kutumia simu sio salama

Shahidi: Yah mwisho

Wakili: Isome

Shahidi: Hello bro nimeshindwa kupokea simu kwa sababu ya......

Wakili: Kwahiyo unataka kusema imefanana na hiyo usitumie simu sio salama sana

Wakili: Linganisha meseji uliyomsomea Jaji na hii hapa zimefanana?

Shahidi: Zinafanana

Wakili: some Jaji

Shahidi: 729414989

Wakili: Inasemekana ni ya nani

Shahidi: Free

Wakili: Zinafanana na za kielelezo ulichosaoma awali

Shahidi: Zinatofauti kubwa

Wakili: Tafuta sms ya tarehe 20/7/ 2020 ya saa 2:14 isome

Shahidi: Naomba nitumie nauli niwamobilize nikutane nao Morogoro

Wakili: Nani alikuwa anaomba nauli

Shahidi: Mimi

Wakili: Baada ya wewe kuomba nauli Mbowe ndio akatuma

Shahidi: Ni sahihi

Wakili: Nitafutie meseji ambayo Mbowe anatoa wazo la kutuma hiyo 500,000

Shahidi: Hakuna

Wakili. Ni nani kwa mujibu wa meseji aliyetoa wazo la kutuma 500,000

Shahidi: Ni mimi

Wakili: Kwa mujibu wa kielelezo namba 34 hiyo meseji ulituma kwa kutumia namba gani

Shahidi: Haionekani

Shahidi: Tafauta meseji ya tarehe 20 /7/2020

Shahidi: Nimeiona

Wakili: Usiwe unatumia namba yako kutuma pesa tumia Wakala au wasaidizi wako, Ni nani alituma ujumbe huu?

Shahidi: Ni mimi kwenda kwa Freeman Mbowe

Wakili: Hao wasaidizi waliwahi kukutumia pesa kutumia namba zao

Wakili: Unamfahamu msaidizi wa Mbowe anaitwa Wile

Shahidi: Sifahamu

Wakili: Kwenye mazungumzo yenu kwenye miamala ya kifedha hajawahi kuzungumzia mtu anaitwa Wile

Shahidi: Nimewahi

Mahakama imerejea baada ya mapumziko ya muda mfupi kwaajili ya Wakili wa utetezi Peter Kibatala kuendelea kumuhoji shahidi wa 12, Luten Denis Urio.

Mawakili wa pande zote wako tayari kuendelea

Wakili Kibatala: Mheshimiwa Jaji Naomba kielelezo namba 34 na 36

Wakili: Shahidi washa simu

Shahidi: Tayari

Wakili: Meseji ya tarehe 22/7/2020 saa 3:19:30 Namba ya dereva wangu anaitwa Wille atatuma pesa na ndio atawapokea ni sahihi

Shahidi: Ni sahihi

Wakili: Tarehe hiyo namba iliyotuma pesa iliingia kwenye simu yako

Shahidi: Ni sahihi

Wakili: Ni wapi unasema Freeman Mbowe alikutumia hiyo namba

Shahidi: Alituma kwa njia ya kawaida

Wakili: Iko wapi

Shahidi: Sikumbuki

Wakili: Huyu Wille hujawahi kukutana naye

Shahidi: Sijawahii kukutana naye

Wakili: Huyu Mbowe alikwambia umtafutie watu au magaidi

Shahidi: Kwaaji ya kwenda kuambatana naye na kufanya nchi isitawalike

Wakili: Kwahiyo wewe ulikuwa unamtafutia Mbowe watu kwaajili ya kufanya uhalifu

Shahidi: Walinzi

Wakili. Waliwahi kukwambia wakina Kingai unatakiwa uwe mshtakiwa namba moja au mbili

Shahidi. Hawakuwahi kuniaamba

Wakili: 22/7/2020 saa 12:27 hiyo sms nani alituma

Sahahid: Mimi kwenda kwa Freeman Mbowe

Wakili: Wakina Bwire walikuwa wameshaindoka kwenda kwa Mbowe

Shahidi: Ni sahihi

Wakili: Kwa maelezo haya inamaana ulitoa zote kwa pamoja

Shahidi: Ni sahihi

Wakili: Ushahidi wako na maelezo ni sahihi vinatofautiana au vinapishana

Shahidi: Vinaoana tofauti iko kwenye tafsiri

Wakili: Ulikuwa unashauri Mbowe awe anakutumia fedha za ziada

Shahidi: Ni sahihi

Wakili: Kwahiyo ulikuwa unamuomba ukijua anamipango ya kigaidi

Shahidi: Ni sahihi

Wakili: Ulishawahi kusikia neno soulitationi

Shahidi: Sijawahi

Wakili. Fedha hizi ulikuwa unaomba baada ya kupokea 500,000

Shahidi: Ni sahihi

Wakili: Ulisema kila hatua ulikuwa unamfahamisha Kingai

Shahidi: Ni sahihi

Wakili: Unaweza kutuonyesha meseji yoyote uliyomtumia Kingai

Shahidi: Hakuna

Wakili: Na meseji yoyote unayotumiwa fedha

Shahidi: Hakuna

Wakili: Kuna meseji inasomeka Shkamoo Mkuu

Shahidi: Ni sahihi

Wakili. Kwahiyo ulikuwa unamsalimia mtu anayeenda kutekeleza vitendo vya kigaidi

Shahidi. Ndio nilikuwa sina ugomvi naye

Wakili: Unasema Halfani Bwire alikupigia akakwambia wenzake wako Moshi wanaenda kutekeleza vitendo vya Kigaidi

Shahidi: Hakunipigia mimi ndio nilimpigia

Wakili: Katika maelezo yako uliandika kuwa wako Moshi wanampango wakumshambulia Sabaya

Shahidi: Mimi nilimpigia

Wakili. Unataka tuamini ulichokiandika Bwire naye yuko Moshi

Shahidi: Tumuulize

Wakili: Na katika maelezo yako uliandika Bwire yuko Dar es Salaam

Shahidi: Sikuandika

Wakili: Katika maelezo yako umeandika tukakutana tena na Freeman Mbowe limeingizwa kimakosa kwa sababu umesaini na kudthibitisha kuyasoma?

Shahidi: Sahihi

Wakili. Unasema kabla ya kukutana naye alikuwa anakutumia na ujumbe na kukutakia heri?

Sahahidi: Ni sahihi

Wakili: Mtu anayekutumia ujumbe na kukutakia heri ni mzalendo au sio mzalendo

Shahidi: Ni mzalendo

Wakili: Nani alikutafuta ni Freeman Mbowe au wewe ulimtafuta

Shahidi: Yeye ndio alinitafuta

Wakili: Kupitia nini

Shahidi: Simu na kupitia Whatsup call na namba nyingine

Wakili: Hizo namba ulizifikisha kwa DCI

Shahidi: Sikuzifikisha

Wakili: Nani aliandika maelezo yake kuwa nilimtafuta na kumwambia kuwa tunaweza kuonana.

Kuna sehemu umeandika kuwa ulimtafuta baada ya kukuita micdcall

Shahidi: Hamna

Wakili: Unaona kuna mfanano hapo au kuna tofauti

Shahidi: Kuna tofauti

Wakili: Kuna mahali ulipoandika kuwa baada ya kumpiga. DCI ulijutambulisha kama Ofisa wa jeshi

Shahidi: Nilijitambulisha

Wakili: Mheshimiwa Jaji kwa Ruhusa yako naomba wenzangu wanipe nyaraka halisi ya maelezo

Wakili: Maelezo ni ya kwako

Shahidi: Ni sahihi

Wakili: Nitafutie hiyo sehemu tafadhali

Shahidi: Hakuna

Wakili: Maelezo yako na ushahidi wako vinafana

Shahidi: Vinatofautiana

Wakili: Unakumbuka ulichojibu kwa wakili Mallya kuhusu kutumiana meseji

Wakili Kidando: Mheshimiwa Jaji naomba Shahidi asome maelezo yake kwanza

Wakili Kibatala: Mheshimiwa Jaji nyaraka hii inasomwa baada ya kuingia

Jaji: Utaratibu unasema nyaraka kwanza isomwe

Wakili Kibatala: Haya Shahidi soma maelezo yako.

Wakili: Ngerengere na Kihonda pana umbali gani

Shahidi: Kilomita 50 au 60

Wakil: Ulishamwambi Mheshimiwa Jaji unaishi Kihonda

Shahidi: Familia yangu iko kule

Wakil: Ulishawahi kusema hapa mahakamani kama kuwa unaishi Kihonda

Shahidi: Hapana

Wakili: Una matatizo na hayo maelezo

Shahidi: Hapana

Wakili: Unataka Jaji atende haki kabisa

Shahidi: Ndio

Wakili. Kuna tatizo tukiyatoa

Shahidi: Hakuna tatizo

Wakili. Mheshimiwa Jaji kama Shahidi alivyoomba

Jaji: Upande wa mashtaka mnasemaje

Wakili Kidando: Hatuna pingamizi Mheshimiwa

Jaji. Mahakama imepokea maelezo haya kama kielelezo namba nne cha upande wa utetezi.

Wakili: Shahidi simu bado ina chaji?

Shahidi: Ngoja niwashe

Wakili: Kuna meseji inasema kuwafanyia vetting ilikuwa vetting ya nini?

Shahidi: Kwa kuwa wanaenda kufanya kazi ya ugaidi ni muhimu kufanya vetting na wakiona vitendo vya kihalifu waniambie

Wakili: Hii meseji ulikuwa unajitumia mwenyewe au?

Shahidi: Nilikuwa natumia Freeman Mbowe

Wakili: Kuna kitu kingine cha ziada ulitaka kuwafanyia wakina Adamoo hadi ukaomba hela ya ziada kwa Mbowe.

Shahidi: Kwa kuwa hela ya awali ilishakuwa comshumd

Wakili: Ulikuwa unawafanyia orientation magaidi.

Shahidi: Ndio kwa fedha za Mbowe

Wakili: 22/7/2020 ulituma meseji inasema lakini wewe usitumie namba yako nani alituma

Shahidi: Mimi kwenda kwa Freeman Mbowe

Wakili: Kwa nini ulimtumia

Shahidi: Ili kuongeza Trust

Wakili: Nauli pamoja na hela za kula ni 2000, 000 nani alituma hiyo meseji

Shahidi: Mimi kwenda kwa Mbowe

Wakili: Hapa mlikuwa mnakubaliana nini kuhusu mishahara

Shahidi: Kwa hiyo kazi wanayoenda kuifanya

Wakili: Ni kazi gani hiyo

Shahidi: Ya uhalifu

Wakili: Kuna meseji inasema kuhusu utawala utawala ni nini

Shahidi: Chakula

Jaji: Nimepata taarifa kuna mafundi wanahitaji kufananya matengenezo tujitahidi angalau saa kumi na nusu tumalize.

Wakili Kibatala: Basi ngoja nisukumesukume hadi hapo kisha ntatoa hoja ya kuahirisha.

Wakili Piusi Hilla. Mheshimiwa Jaji tunaomba Wakili afanye cross kuna maeneo naona anarudia

Jaji. Ni vizuri unapouliza maswali ukatoa eneo hilo moja badala ya kurudia rudia.

Wakili Kibatala: Kama kuna sehemu anaona nimerudi au kama kuna swali basi aseme.

Wakili: Unaweza kufanya mlipuko bila kuwa na vya kulipiulia

Shahidi: Huwezi

Wakili: Katika ushahidi wako kuna sehemu ulisema bunduki aina ya luger ni mahusi kwaajili ya makomandoo kufanya ugaidi

Shahidi: Sijasema

Wakili. Baada ya Julai 24, 2020 uliwahi kuwasiliana tena na Mbowe

Shahidi: Nilikuwa nikimpigia hapokei nikamtumia meseji

Wakili: Ulikuwa unawasilia naye kwa meseji

Shahidi: Telegram

Wakili: Ulimuonyesha Jaji meseji ulizokuwa ukifanya juhudi za kumtafuta Mbowe

Sahahid: Sikufanya

Wakili: Tunakubaliana kilichoandikwa hapo ni simu yako na sio simu zako

Shahidi: Ni sahihi

Wakili: Uliongozwa na wakili wa Serikali kuonyesha rekodi zako za simu ulizokuwa unawasiliana na Bwire

Shahidi: Hapana

Wakili: Inspekta Swilla alikwambia na yeye ni mpelelezi kwenye shauri hili

Wakili: Sifahamu

Shahidi: Ni sahihi hukuwahi kusema kama uliandika maelezo ya ziada

Shahidi: Ndio

Wakili: Kambi ya makomandoo ipo Ngerengere au Kizuka

Shahidi: Kizuka

Wakili: Ulimwambia Jaji kuwa Kambi iko Kizuka na sio Ngerengere

Shahaidi: Ngerengere ni tarafa

Wakili Kibatala: Unakuambuka nilikwambia nini kuhusu namba DCI

Shahidi: Nakumbuka

Wakili: Ulisemaje

Shahidi: Nimeacha hotelini kwangu kwenye diary

Wakili: Ijumaa tulivyoachana hapa hadi leo na hujaja nayao

Shahidi: Nilisubiri nipewe maelekezo na mahakama

Wakili: Na wakili Mallya alikuuliza kuhusu Order nayo iko wapi

Shahidi: Hotelini kwangu

Wakili: Kwahiyo na leo nikihitaji haipo.

Wakili: Kipindi kinachohusiana na shauri hili ni kuanzia Juni 2020 hadi Agosti 2020

Shahidi: Ni sahihi

Wakili: Mbowe alikuwa anawasiliana na wewe kwa Telegram ili kuficha mawasiliano yenu

Shahidi: Ni sahihi

Wakili: Kabla ya tarehe hizo tukiangalia hatutakuta mahali mlikuwa mnawasiliana kwa telegram kabla ya tarehe hizo

Shahidi: Tulikuwa tunawasiliana kwa whatsup

Wakili. Ulimwambia Mheshimiwa Jaji wakati unamkabidhi Inspekta Swilla simu ulimuona akibandika kikaratasi

Shahidi: Sikumwambia

Wakili: Kazi ya kuzuia uhalifu ni yako au polisi

Shahidi: Polisi

Wakili: Chakula alichokula Adamoo na wenzake nani alilipia

Shahidi: Kililipiwa na pesa za Freeman Mbowe

Wakili: Ulisema katika fedha ulizowapa wakina Adamoo walitoa kiasi flani kwaajili ya chakula

Shahid: Sikusema

Wakili: Unafahamu hakuna simu ya Mbowe hata moja iliyokamatwa

Shahidi: Sifahamu

Wakili: Wewe ulikuwa una mamlaka yoyote ya kiupelelezi zaidi ya kutoa taarifa?

Shahidi: Sina mamla ya kiupelelezi zaidi ya kuto taarifa

Wakili Kibatala: Mheshimiwa Jaji bado nina maswali kwa shahidi na kupitia ombi letu naomba tuahirishe kesi hadi kesho Februari Mosi, 2020 kwaajili ya kuendelea na Cross Examination.

Wakili Kidando: Hatuna pingamizi Mheshimiwa iIa tunaomba Shahidi kesho ajielekeze kwenye maeneo ambayo hayajaulizwa.

Jaji: Naahirisha kesi hii hadi kesho Februari Mosi 2022 kwaajili ya shahidi wa 12 kuendelea kuhojiwa na upande wa utetezi.

Shahidi unakumbushwa kuja kuendelea kutoa ushahidi wako washtakiwa mtaendelea kuwa chini ya uangalizi wa Magereza.

Chanzo: mwananchidigital
Related Articles: