Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imeahirisha kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na wenzake watatu.
Jaji Joachim Tiganga anayesikiliza ameahirisha kesi hiyo mpaka kesho Jumanne Januari 11, 2021 saa tatu asubuhi baada ya shahidi wake wa nane, Mkuu wa Upelelezi wa Polisi Wilaya (OC-CID) Arumeru, Mrakibu wa Polisi (SP), Jumanne Malangahe kumaliza ushahidi na upande wa utetezi kuanza kumhoji shahidi huyo.
Wakati mawakili hao wakiendelea na kumhoji shahidi, Wakili wa utetezi Peter Kibatala aliiomba mahakama iahirishe kesi hiyo mpaka kesho akidai kuwa bado ana maswali mengi lakini muda umepita, hoja ambayo iliridhiwa na pande zote na kumfanya Jaji Tiganga kuahirisha kesi hiyo.
Mapema asubuhi kesi hiyo ambaypo ilisimama kwa siku 21 kupisha mapumziko ya sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya 2022 ilianza kwa Jaji kutoa uamuzi mdogo wa pingamizi lililokuwa limewekwa na upande wa utetezi.
Akitoa uamuzi huo mdogo, Jaji Tiganga aliridhia Mahakama kutokupokea sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kama moja ya kielelezo ambapo upande wa utetezi ulidai kuwa kielelezo hicho kipo kinyume na sheria.
Baada ya uamuzi huo, Mahakama iliendelea na usikilizaji wa ushahidi wa shahidi wa nane wa upande wa mashtaka ambaye ni Mkuu wa Upelelezi wa Polisi Wilaya (OC-CID) Arumeru, Mrakibu wa Polisi (SP), Jumanne Malangahe.
Hapa ni mwanzo mwisho wa muenendo wa kesi hiyo ilivyoendelea leo
Jaji Joachim Tiganga ameshaingia mahakamani kwa ajili ya kusoma uamuzi
Mawakili wa pande zote wameanza kujitambulisha.
Jaji Tiganga anawaita majina washtakiwa mmoja baada ya mwingine
Wakili wa Serikali Mwandamizi, Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji shauri linakuja kwa ajili ya kupokea uamuzi na kuendelea na ushahidi
Jaji: Upande wa utetezi?
Kibataka: Mheshimiwa Jaji nasisi tupo tayari kupokea uamuzi na kuendelea na kesi
Jaji: Nilitoa maelekezo hapa mahakamani, mtu yoyote anayeingia amwe amevaa maski (barakoa) kwanini wengine hawajavaa??
Jaji: Nina excuse ya wakili mmoja ambaye havai ...sasa wengine je?
Wakili Mallya: Mimi nina tatizo kidogo lakini nimechukua tahadhari zote za kujikinga na Uviko-19.
Baada ya Maelezo hayo, mmoja wa wafuasi wa Chadema alitoka nje na kwenda kuvaa barakoa kisha kuingia ndani huku watu wengine waliokuwepo ndani ya mahakama waliokuwa wameshusha barakoa zao chini ya pua, wakizipandisha barakoa zao juu ya pua
Jaji Tiganga ameanza kusoma uamuzi wa kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi.
Jaji Tiganga: Upande wa utetezi wao walianza na hoja moja kuwa kielelezo hicho namba 14 (Hati ya ukamataji mali) kilichezewa hivyo wanaomba ihesabike kuwa kisipokelewe na mahakama kwa sababu hajikidhi vigezo.
Jaji Tiganga: Kwa upande wa mashtaka wao walijibu hoja za upande wa utetezi kwa kueleza kuwa upande wa utetezi wametafsiri vibaya tafsiri ya sheria na kusema suala la utunzaji wa vielelezo linafahamika na upande wa mashtaka haulazimishwi kutoa vielelezo vyote.
Jaji Tiganga: Upande wa mashtaka wakaendelea kuomba korti ipokee kielelezo hicho kwa sababu kimekidhi vigezo.
Jaji: Upande wa mashtaka uliendelea kueleza kuwa shahidi wa nane wa upande wa mashtaka SP Jumanne Malangahe aliandika maelezo namna alivyomtambua shahidi na namna alivyowasilisha vielelezo hivyo kwa mtunza vielelezo aitwaye Sajenti Johnstone.
Hivyo upande wa mashtaka waliomba mahakama ipokee kielelezo hicho kwa sababu hakikuchezewa na kilifuata mnyororo wa utunzaji.
Upande wa mashtaka waliendelea kuiomba mahakama ipokee kielelezo hicho baada ya kupitia mnyororo wa utunzaji wa kielelezo.
Jaji: Pia upande wa mashtaka walieleza kuwa shahidi wa nane SP Jumanne Malangahe ndio aliyevikamata vielelezo hivyo na ndio yeye aliyevitoa mahakamani baada ya kuvitoa kwa mtunza vielelezo.
Jaji: Upande wa utetezi wakiwasilisha nyongeza yao ya kuwapinga vielelezo hivyo walieleza kuwa shahidi alitakiwa aviandike vielelezo hivyo katika notebook yake ili kuepuka vielelezo visichezewa.
Jaji: Hoja kuhusu Competent iliyotolewa na upande wa utetezi kuhusu kielelezo hicho kwamba hakukuwa na uthibitisho uliotolewa kama kweli sare hizo ninmali ya JWTZ
Jaji- Wakili Mallya alidai kuwa vielelezo hivyo ni vya kijeshi na nilitakiwa kutolewa kwa majina ya kijeshi.
Mallya alidai mfano kuna kielelezo shahidi alikita kuwa ni koti la mvua au ponjoo wakati kwa lugha ya kijeshi linatambulika kama sleeping bag.
Jaji: Wakili Mallya aliendelea kueleza kuwa kwa mazingira hayo shahidi huyo SP Jumanne Malangahe hana uelewa wa kutosha kuhusiana na vielelezo vyenyewe, hivyo wanaomba vielelezo hivyo visipokelewe.
Mallya aliendelea kueleza kuwa shahidi wa nane huyo hajaithibitishia wala hakuleta ushahidi wake mahakakani kama ni mtaalamu wa utambuzi wa vifaa vya kijeshi
Jaji: Kwa upande wa mashtaka kupitia wakili Kidando akijibu hoja ya wakili Mallya alidai kuwa shahidi alitambua vielelezo hivyo kwa alama alizoweka mwenyewe na kwamba sio lazima shahidi kuwa mtambuzi bali anatakiwa kuwa na ufahamu wa vifaa vya kijeshi.
Jaji: Hivyo upande wa mashtaka walidai maelezo aliyotoa Mallya kuwa vielelezo hivyo vimetolewa kwa majina tofauti havina mashiko kwa sababu Mallya yeye sio shahidi katika kesi hii, hivyo wanaomba Mahakama ipokee kielelezo hicho kwa sababu shahidi alitambua vielelezo hivyo kupitia alama alizoweka wakati wa ukamataji.
Jaji: kourti baada ya kupitia hoja za pande zote mbili zilizowasilishwa na Mallya, inatupilia mbali pingamizi hili.
Jaji: Kifungu pia cha 22(3) d cha Sheria ya Uhujumu Uchumi inasema pia kuwa ni lazima kutoa risiti but pia PGO ya 226 (2,5) na yenyewe inasema kuhusiana na utolewaji wa risiti
Na mwisho Guidelines ya Mahakama Chapter 05 Paragraph ya 5 (f) inasema kuwa inatakiwa kutolewa risiti ya mali zilizokuwa zinakamatwa
Hakuna sehemu inayosema kuwa pale mahala ambapo risiti haijatolewa basi seizure Certificate itumie kama mbadala wa risiti
Kwa upande wa utetezi walikataa mwaliko huo kwa kuomba mahakama ikatae mwaliko huo kwamba risiti na seizure Certificate ni nyaraka mbili tofauti
Katika eneo hilo Mahakama inamaoni kuwa swala la risiti Mahakama imewekwa wazi na ni muhimu itumike
Suala la Certificate of Seizure (hati ya ukamataji) kutumika badala ya Risiti kuna Maamuzi ya mahakama ya Rufani ya ANDREA AGUSTINO na wenzake ikiwa imeamliwa huko Tanga katika Rufani ya Jinai.
Mahakama ilipo itwa Kuona Kuwa Risiti Itumike Mbadala wa Certificate of Seizure ilisema Kuwa
Basi ni wazi kuwa Mahakamani ya Rufani ilishaona kuwa jambo hili no vitu viwili tofauti na Mahakama inaona kuwa kutokutolewa kwa risiti Ni mambo mawili tofauti.
Baada ya kuwa tumeona kutokutolewa kwa risiti kuna athari, Mahakama ya Rufani Iliyoketi Iringa na Ilikuwa aime Quote with Approval katika Kesi ya PATRICK JEREMIAH Vs JAMHURI 34 / 2016
Kwa sababu hiyo Mahakama hii Inaona Kuwa Kushindwa Kutoa Kwa risiti ni Fatal na Jambo hili lina athiri Admissibility.
Kutokana na malekezo hayo ya Kisheria yakiyoelezwa katika PGO hiyo ni wazi kuwa alama iliyiwekwa siyo alama ambayo PGO 229 imeitambua na kuelekeza
Hata kama alama hiyo ingekuwa imevumiliwa basi kama ingekuwa alama hiyo iliwekwa mbele ya mashahidi hao basi ingevumilia
Hivyo, katika utaratibu huo Mahakama ina maoni kwamba alama hiyo iliyowekwa imekiuka PGO 229 kwa maana hiyo inaathiri afya ya kielelezo hicho na kuathiri Competence
Na nikitafuta matakwa ya Adminsibility kuwa Polisi ofisa alitakiwa kutoa risiti ya ku -acknowledge kukamata vielelezo hivyo
Hata hivyo jatika koja hiyo upande wa utetezi wanasema kuwa mtu yoyote ambaye anafanya upekuzi lazima atoe risiti baada ya upekuzi kama ambavyo Sheria inalekeza
Wanasema kuwa shahidi wa nane wa upande wa mashtaak hajasema kuwa ametoa risiti wala hajatoa nakala yoyote mahakamani kama alitoa risiti
Kwa namna hiyo wakialika sheria kwa kutokutoa risiti.
Katika majibu yake Wakili Kidando anasema kwa kufanya upekuzi na kukamata mali, Shahidi namba nane alitoa hati ya ukamataji mali ( Seizure Certificate).
Pia upende wa mashtaka wakasema kuwa kwa kutolewa Seizure Certificate ambayo ina content sawa na risiti wakaomba Mahakama wa one kuwa Seizure Certificate ionekane kama risiti
Upande huo wa mashtaka waliendelea kwa kuomba Mahakama Izingatie Sehemu ya Pili katika sehemu A ya CPA, 2 (a) D Mahakama Ione kuwa Kuwepo Kwa Seizure Certificate ni sawa na Kutolewa Risiti
Hivyo, nakubaliana na upande wa utetezi kama ambavyo wameieleza Mahakama kuwa panapokuwa umefanyika upekuzi katika nyumba, box au eneo ofisa ambaye amekamatwa mali anatakiwa kutoa risiti juu ya mali alizokamata na nukuu Kifungu cha 38 (3) ya CPA
Kifungu Kingine kinachohusika kutolewa na risiti ni kifungu cha 35(3) ya Sheria ya Polisi na Polisi Wasaidizi Sura ya 322
Uamuzi wa Jaji Tiganga: Katika hali ya kawaida Mahakama ilitakiwa kuishia hapa, lakini kuna mwaliko wa Kibatala kuwa Mahakama izingatie kuwa unatafuta nini kila inapokuwa Sheria inakiukwa lakini wanapewa nafasi upande wa mashtaka
Nimeona hakuna cha ku reconcile katika maamuzi ambayo nimeshayatoa, maamuzi yote niliyo yatoa ni maamuzi halali hivyo Mahakama inaona hoja hiyo halikuwa na mashiko na naitupilia mbali
Mahakama inaona hoja zote zilizoletwa na upande wa utetezi hayakuwa na mashiko isipokuwa mapingamizi mawili ya Lebelling na kutokutoa risiti
Na kwa mapingamizi haya Mahakama inaona yana merit na sababu nilizotoa mahakamani nakataaa vielelezo hivyo na ninatoa amri.
Jaji Tiganga baada ya kutoa uamuzi huo, Mawakili wa pande zote mbili wanakubaliana na uamuzi Jaji kwa kusimama na kumuinamia.
Jaji: Haya upande wa mashtaka tuanendela na ushahidi.
Baada ya Jaji kutoa uwamuzi shahidi wa nane anaendelea na ushahidi.
Jaji: Shahidi tunakukumbusha uko chini ya kiapo na utaendelea kutoa ushahidi wako.
Wakili Kidando anamuongoza Shahidi kuendelea na ushahidi.
Shahidi Jumanne Malangai Tarehe 24/2020 nikiwa Arusha nilifika eneo moja nililoliona kwenye mchoro linaitwa kilombero na kubaini ni soko lililoko katikati ya Jiji upande wa magharibi limepakana na gereza la kisongo, kutokea hapo umbali mfupi upande wa kulia kuna hilo soko la kilombero.
Nilipo endelea na upelelezi kesho yake tarehe 25, alikamatwa mtuhumiwa Elia Kaaya ambaye baadae aliachiwa baada ya upelelezi kukamailika
Justin Kaaya aliachiwa baada ya ushahidi kuonyesha alikuwa hausiki
Tuliendelea kufuatilia taarifa za watuhumiwa wengine ambapo tarehe 10/9 alikamatwa mtuhumiwa mwingine ambapo naebaliachiwa baadaa ya upelelezi kukamillika.
Mshtakiwa huyu kwa taarifa tulizopata alikuwa Miongoni mwa watuhumiwa waliokuwa washiriki kufanya uhalifu.
Tulifika mkoani Tabora na kukamata mtuhumiwa mwingine Gabriel Mhina tarehe 19/9/2020 nae alikuwa ni askari wa JWTZ Kikosi cha 92 KJ nae aliachiwa baada ya ushahidi kutokamilika
Kuna mtuhumiwa mwingine tulimkamata Mwanza tarehe 19 wakati tukiwa tunamfuatilia mtuhumiwa mwingine Malima ambaye nae aliwahi kuwa JWATZ Kikosi cha 92 KJ
Asubuhi nlitembelea eneo lingine Mwanza mjini ambapo kuna mkutano ya barabara kuelekea mabatini upande wa kushoto kuelekea benki ya BOT kuna kituo cha mafuta kinachoitwa Puma Energy
Tulimkamata Malima eneo la mjini linaloitwa pasians na baadae aliachiwa baada ya kuhojiwa na kuonekana hakuna ushahidi wa kumpeleka mahakamani
Baada ya hapo upelelezi uliendelea na tarehe 22/11 aliketwa mtuhumiwa wa nne Freeman Mbowe ili niweze kumuhoji
Baada ya mtuhumiwa kuletwa mbele yangu na kujitambulisha nilimuonya kuhusiana na tuhuma za kula njama za kutenda ugaidi na baada ya kumuonya alikubali kuandika maelezo yake mbele ya Wakili wake alimtambulisha Fred Khiwelo.
Wakili Kibatala: Haya yote anayoeleza shahidi yako kwenye rekodi sioni kama yana tija
Shahidi: Baada ya kumuhoji Mbowe alisema hawezi kutoa maelezo hadi pale atakapofika mahakamani.
Jina la Alfani Bwire nililiandika kutokana na matamshi yake mwenyewe
Mheshimiwa Jaji ni hayo tu.
Wakili Kibatala: Kutokana na yale mazoea yetu tuliyojiwekea kupumzika saa saba ningeshauri tupumzike dakika 45 ili tukirudi tuweze kuendelea
Wakili Kidando: Mheshimiwa hatuna pingamizi
Jaji. Tunabreak kwa dakika 45 tutarudi hapa saa saba na nusu.
…………………………………………………..
Mahakama imerejea kwaajili ya upande wa utetezi kumuhoji Shahidi.
Wakili Nashon Nkungu: Unasema ulihusika kuwakamata mshtakiwa wa pili na watatu
Shahidi: Ni sahihi
Wakili: Baada ya kuwakamata mlienda nao central Polisi
Shahid. Ndio
Wakili. Mlikuwa na afande Mahita
Shahdi: Ndio
Wakili: Mlifika kituoni
Shahid: Ndio
Wakili: Mwambie Jaji kama ni muhimu kumuandikisha mtuhumiwa kwenye detention register
Shahidi: Ndio
Wakili: Kwahiyo unaweza kumfikisha mtuhumiwa kituoni na usimwandikishe
Shahidi: Mtuhumiwa anaandikishwa pale anapofikishwa kituoni
Wakili: Unafahamu kwamba ni kinyume na PGO inapinga askari kutegemea kumbukumbu zake kwenye kesi za jinai
Shahidi: Hiyo ni nyongeza
Wakili: Muda nni vitu vya makadirio au ni muda sahihi
Shahidi: Ni Muda sahihi
Wakili: Mida mliyokuwa mna andika ni sahihi na sio makadirio
Shahdi: Ni Muda sahihi
Wakili: Ulisema mlifika Rau madukani saa saba mlifika na dakika ngapi?
Shahidi. Nachojua tulifika saa saba sio kila nachofanya ntaangalia dakika.
Wakili: Baada ya kufika pale mahita aliambiwa akaangalie kama mtuhumiwa wa pili na Watatu wako pale
Shahidi: Ni sahihi
Wakili: Ilikuwa saa ngapi
Shahii: Sio kila unachofanya unakadiria muda
Wakili: Nikisema alirudi baada ya nusu saa
Shahidi: We ndio utakuwa umesema hivyo
Wakili: Mazoezi yote sita yalifanyaika kwa muda gani
Shahidi: Ndani ya saa moja
Wakili: Baada ya kufanyika mambo yote mlienda kuwapekuea
Shahid: Ndio
Wakili: Hebu mwambie Jaji hii immrandikwajr
Shahidi: P12
Wakili: Na hii nyingine unaweza kutambua
Shahidi: Imeandikwa P11
Wakili. Kwenye vielelezo hivi angalia upekuzi ulifanyika muda gani
Shahidi: Saa saba mchana.
Wakili: Upekuzi ulifanyika kabla hamjafika?
Shahidi: Ulifanyika saa saba mchana
Wakili. Ni sahihi zaidi ya mara moja mlienda na watuhumiwa Moshi central
Shahidi: Kweli
Wakili: Ni sahihi kwamba mlitembea na watuhumiwa na kuwarudisha polisi, huoni kama mngepata nguvu kama mngetoa detention register
Sahahid: Muhimu ni ushahidi nilioutoa hapa
Wakili: Unajua umuhimu wa detention register
Sahahid: Ndio
Wakili: Bila kuwepo kwa nyaraka hizi mtu anaweza kuwa na uhakika watuhumiwa walifikishwa polisi
Shahidi: Sio lazima mtu aliyefikisha ndio anaweza kusema
Wakili: Kwahiyo hata muda wa uwakika kuletwa Dar haupo
Shahidi: Upo
Wakili: Kwahiyo hata nyaraka hiyo hujaileta hapa mahakamani
Shahidi: Sijaileta
Wakili: Mkiwa moshi watauahumiwa walilala wapa
Shahidi: Sijui kama walilala kwa kuwa kituo cha polisi
Wakili: Kama kweli mlisafiri kitu kingine cha kuonyesha ni polisi logbook
Shahidi: Polisi logbook hainihusu mimi sio dereva
Wakili: Mlisafiri na gari binafsi au ya Polisi
Shahidi: Ya Polisi
Wakili: Kila safari unajua lazima iwe autorised
Shahidi: Nafahamu
Wakili: Unafahamu unapoanza kusafiri station ofiser anatakiwa kurekodi muda na namba ya gari
Shahidi: Inategemea
Wakili: Unafahamu gari ya Polisi inapotoka nje ya mkoa unahitaji ruhusa ya IGP
Shahidi: Sio kweli
Wakili: Unafahamu gari inapopata hitilafu inatakaiwa kuripotiwa kituo cha karibu
Shahidi: Sio kweli
Wakili: Unafahamu fomu ya Polisi EMI
Shahidi: Sifahamu
Wakili: Unajua gari ya Polisi inataikiwa kuwa na logbook
Shahidi: Nafahamu
Wakili: Ni sahihi hujatoa logbook hapa mahakamani
Shahaidi: Sijato
Wakili: Na kwenye ushahid wako hujataja namba za gari
Shahidi: Sijataja
Wakili: Tarehe 9 wewe na Mahita mliwapeleka watauahumiwa Mbweni
Shahidi: Sio kweli
Wakili: Unakumbuka nmba za gari mliotumia
Shahidi: Sikumbuki
Wakili: Ili kuonyesha mlienda Mbweni una logbook
Shahidi: Mimi sio dereva
Wakili: Kuna kauli mbili za mashahidi wawili ni sahihi wewe na Mahita mlikuwa kwenye gari moja
Shahidi: Ni sahihi
Wakili: Mlikuwa mnawauliza maswali mbalimbali.
Shahidi: Vitu gani hebu fafanua
Wakili: Mahita alihoji alipo mtuhumiwa Lijenje
Shahidi: Hilo liliulizwa
Waikili: We na Mahita nani muongo
Shahidi: Hakuna muongo
Wakili: Unajua watuhumiwa wanakataa hamkuzunguka kutafuta mtumiwa mwingine
Shahidi: Kwenye ushahidi wangu nimeeleza
Wakili: Mlienda hadi Aish hotel
Shahidi: Tulienda
Wakili: Mlikuwa na hati ya upekuzi
Shahidi: Hatukwenda kupekua tulienda kutafuta mtuhumiwa
Wakili: Uliiingia kwenye hiyo hoteli
Shahidi: Alienda Kiongozi wetu
Wakili: Kama mlikuwa mnamtafuta mtuhumiwa mlienda tu na kuondoka
Shahidi: Hiyo ni kazi inayohitaji utaalamu sio kama unavyotaka wewe
Wakili: Ulisema sababu za kutokuandika maelezo ni kwakuwa mlikuwa a mnamtafuta Lijenje
Shahidi: Pamoja na shauri lilipokuwa limefunguliwa Dar es salaam
Wakili: Wakati huo mlikuwa mnamfahamu mtuhumiwa wa nne Freeman Mbowe ni mtuhumiwa
Shahidi: Tulikuwa tunafahamuu
Wakili: Wengine waliweza kuandika bila Mbowe kukamatwa
Shahidi: Ni sahihi
Wakili: Ni sahihi Mbowe ulimuhoji saa sita usiku
Shahidi: Ndio
Wakili: PGO inaeleza kila hatu zichukuliwe kwenye ushahidi utakaohusu finger print
Shahidi: Ni sahihi
Wakili: Ni sahihi hapa mahakamani hujaleta ushahidi unaohusu finger print
Shahidi: Ndio haikuwa na sababu
Wakili: Unafahamu madawa ya kulevya yakikamatwa yanatakiwa kumkabidhiwa kituo cha karibu
Shahidi: Inategemea na mazingira
Wakili: Unafahamu mtuhumiwa akikiri anatakiwa kupelekwa kwa mlinzi wa amani
Shahidi: Inategemea na mtuhumiwa mwenyewe
Wakili: Unafahamu mtu huyo wa tatu anaongeza nguvu mahakamani
Shahidi: Nafahamu
Wakili: Kwahiyo hukuona umuhimu wa mlinzi wa amani
Shahidi: Kama nilivyosema inategemea na uhitaji wa mtuhumiwa
Wakili: Mahita si unamfahamu
Shahidi. Nafahamu
Wakili: Ulimtaja ni mmoja mlieenda naye nyumbani kwa Bwire
Shahidi: Ndio
Wakili: Kwenye ushahidi wako mlimkamata Bwire na simu mbili
Shahidi: Ni sahihi
Wakili: mmezitoa hapa mahakamani
Shahidi: Hapana
Wakili: Mnazihusisha na tuhuma hizi za ugaidi
Shahidi: Bado ziko kwenye utaratibu
Wakili Nkungu amemaliza sasa ni zamu ya Wakili John Mallya.
Wakili Mallya: Unajua mamlaka inayotoa leseni ya kufanya biashara ya mafuta
Shahidi: Sifahamu
Wakili. Inaitwa EWURA
Wakili: Hata kama hujui EWURA wanatoa leseni lakini wale wanaofanya biasahara wanaopata wapi leseni
Shahidi. Sifahamu
Wakili: Umekuja na barua kutoka EWURA angalau Jaji ajue Mwanza Pasians pana kutuo cha Puma Energy
Shahidi: Mimi sijasema kama pana kutuo cha mafuta
Wakili: Mwambie Jaji kama wewe unatoa leseni
Shahidi: Sitoi leseni
Wakili: Twende kwenye siko hapo ulipozungumzia pana soko
Shahidi: Lipo
Wakili: Unasjili masoko
Shahidi: Hapana
Wakili: Umewahi kufanya kazi ofisi ya DIC kabla ya kwenda Arusha
Shahidi: Ndio
Wakili: Ulikuwa kitengo gani
Shahidi: Kitengo cha upelelezi
Wakili: Umewahi kushiriki operesheni mbalimbali
Shahidi: Ndio lakini siwezi kuzitaja
Wakili: Ushiriki wako kwenye kesi ya Tito Magoti
Shahidi: Siwezi kulizuungumzia hapa
Wakili: Unajua Freeman Mbowe ni kiongoz wa upinzani
Shahidi: Ndio
Wakili: Amekuwa akipingana na Sera za Serikali
Shahidi: Siwez kulizuungumzia
Wakili: Umesema wewe ni msukuma unajua na Boazi naye ni Msukuma
Shahidi: Sifahamu
Wakili: Na kwenye kesi ya Kabendera ulihusiakaje
Shahidi: Sifahamu
Wakili: Umesema mnashirikiana na serikali za mita unajua mtuhumiwa wa nne aliwahi kuambiwa anauza madawa ya kulevya na kina Makonda
Shahidi: Sifahamu
Wakili: Umewahi kusikia kuhusu kupotea kwa Beni saa nane
Shahidi: Nilisikia kwenye vyombo vya habari
Wakili: Mlimpeleka wapi Beni
Shahidi: Sifahamu
Wakili: Mbowe alivyokamtwa aliletwa kwako
Shahidi: Ndio
Wakili: Vitu vya Mbowe zikiwemo simu ziko wapi
Shahidi: Sifahamu….
Wakili: Watuhumiwa wanadaiwa kufanya vikao vya ugaidi Dar hebu nionyeshe kwenye maelezo yako wapi wamekiri
Shahidi: Anasoma maelezo
Wakili: Kujadiliana kuhusu malipo ni vikao vya ugaidi
Shahidi: Ndio
Wakili: Unajua sheria inakataza mtu kuwa na mlinzi binafsi
Shahidi: Ndio
Wakili: Ukiwa kwenye ofisi ya DCI 2017 Kiongozi mwenzake Tundu Lissu alivamiwa na risasi
Shahidi: Nafahamu
Wakili: Na unafahamu watu wanaoweza kutumia silaha kama hizo ni watu wenye mafanzo
Shahidi: Hata wahalifu wanaweza
Wakili: Sasa mtu kama Mbowe hutaki ajilinde
Shahidi: Ni kazi ya Polisi
Wakili: Wakati Lissu anavamiwa polisi walikuwa likizo?
Shahidi: Lilikuwepo
Wakili: Sasa kuna ubaya gani
Mbowe kujilinda
Shahidi: Hakuna ubaya
Wakili: Bastola uliyosema ulikama kwa Adamoo inamilikiwa na Kingai na wewe ndio uliweka
Shahidi: Sio kweli
Wakili: Bastola hiyo inamilikiwa na Kingai na aliinunua 2014 pale Moshi ndio maana Msajili hakuleta rekodi zake hapa
Shahidi: Siwezi kuliongelea
Wakili: Ulishawahi kutoa maelezo yoyote kuhusiana na jina Adamoo
Shahidi: Sijaelezea
Wakili: Mheshimiwa ni hayo tu
Wakili Dickson Matata anaanza kumuhoji Shahidi.
Wakili Matata: Ling'wenya alienda kwa Mbowe kufanya nini?
Shahidi: Alisema alipigiwa simu na Denisi Urio kwaajili ya VIP Protection
Wakili: Ni kosa au sio kosa kufanya VIP Protection
Shahidi: Sio vibaya kama itafanyika hivyo
Wakili: Na huyu mtu alitumiwa nauli
Shahidi: Ndio
Wakili: Ni kosa mtu kutumia fedha ya nauli na kula njiani
Shahidi: Sio kosa kama itakuwa imetumika hivyo
Wakili: Naomba nikuulize kuna sehemu yoyote imetajaa vituo vya mafuta au sheli
Shahidi: Hivijatajwa
Wakili: Naomba nionyeshe ni wapi pameandikwa wataweka sehemu gani magogo
Shahidi: Hakuna
Wakili: Ni sehemu gani specific wamesema watafanya maandaman
Shahidi: Hakuna
Wakili: Ni kosa kufanya maandamano kwa mujibu wa sheria
Shahidi: Inategemea yanafanyikaje
Wakili Matata: Ni kifungu gani kinasema mtuhumiwa kupelekwa kwa mlinzi wa amani hadi atake
Shahidi. Sikumbuki ila ni kwa uelewa wangu
Mheshimiwa ni hayo tu
Sasa ni zamu ya Wakili Peter Kibatala.
Wakili Kibatala: Kupitia kesi hii unajua Watanzania wanapima utendaji kazi wa Jeshi la Polisi
Shahidi: Mimi natimiza majukumu yangu
Wakili: Unafahamu unatakiwa kuwa na adabu mbele ya mahakama
Wakili: Mheshimiwa Jaji tarehe 14/12 uje na udhibitisho tarehe 15 Desemba ulifanya au hukufanya
Shahidi: Sikufanya
Wakili: Sasa unataka tukuelewe kuwa una adabu mbele ya washtakiwa na mahakama
Shahidi: Ni nayo adabu
Wakili: Ulinyosha mkono ukasema kuna swali hujaulizwa
Shahidi: Sikunyoshaa
Wakili: Kwahiyo tuseseme umeizoea sana mahakama
Shahidi: Hapana
Wakili: Mwaka 2020 ulikuwa na cheo cha ASP
Shahaidi: Ndio
Wakili: Ni lini ulipandishwa
Shahidi: Mwaka jana mwezi sita
Wakili: Kupandisha cheo ilikuwa tayari umeshiri kwenye masuala ya upelelezi kwenye kesi hii
Shahidi: Ndio
Wakili: Kipindi kile alikuwa na cheo gani
Shahidi: ASP
Wakili: Na alikuwa nani
Shahidi: Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Arusha
Wakili: Na sasa hivi
Shahidi: RPC
Wakili: Mahita sasa hivi ni nani
Shahidi: Inspekta
Wakili: Alipanda au ameshuka
Shahidi: Amepanda
Wakili: Na Goodluck
Shahidi: Yuko chuo anasoma
Wakili: Kukamatwa kwa Bwire dereva wa daladala unamfahamu
Shahidi: Siwafahamu
Wakili: Hukuchukua taarifa zozote
Shahidi: Hapana
Wakili: Sasa huoni utatupa ugumu kujitetea
Shahidi: Kwenye ushahidi wangu nimeeleza
Wakili: Tutakuaminije wakati uliambiwa ulete vyeti hujaleta.
Shahidi: Mshtakiwa alikamatwa ndio maana yuko chini ya ulinzi
Wakili: Hata details za trafiki aliyeelekeza daladala
Shahidi: Haikuwa na umuhimu
Wakili: Ni sahihi ulipohojiwa ulimzungumzia simu za Bwire wakati zinachukuliwa ulikuwepo
Shahidi: Nilishuhudia
Wakili: Wakati mnazichukua kulikuwa na shahidi huru yoyote
Shahidi: Hapana
Wakili: PGO inasemaje kuhusu shahidi huru yoyote
Shahidi: Kuwepo na shahidi huru
Wakili: We ndio una panga shahid gani anakuja
Shahid: Mimi sikuhusika na hizo simu
Wakili: Kwa ufahamu wako washtakiwa walioachiwa walikaa ndani muda gani
Shahidi: Muda mrefu karibia mwaka mmoja
Wakili: Kwanini mliwaachia
Shahidi: Upelelezi ulikamilika
Wakili: Polisi wamejipangaje kuwa fidia
Shahidi: Siwezi kulizungumzia
Wakili: Kuna mmoja hadi leo amepata tatizo la kiakili
Shahidi. Sifahamu
Wakili: Unajua hawa vijana walitumikia hii nchi kwa jasho na damu
Shahidi: Walikuwa ni wahalifu
Wakili: Kwanini mliwaachia
Shahidi: Ushahidi haukutosheleza
Wakili: Kwanini mahakama isione wewe una maslahi
Shahidi: Sina maslahi
Wakili: Ulisema matendo haya ya kigaidi yalikuwa yafanyike nchi nzima
Sahahid: Ni sahihi
Wakili: Kwahiyo wahanga wangekuwa pamoja na raia wa kigeni
Sahahid: Inawezekana
Wakili: Mlitoa taarifa kwa Ubalozi wowote
Shahidi: Hapana
Wakili: Unajua mapambano ya ugaidi ni ya Kimataifa na kuna mkataba mbalimbali tumesaini
Shahidi: Ndio
Wakili: Mwambie Jaji kama ulimzungumzia jitihada zozote mlizofanya na Interpol
Shahidi: Suala hilo sikulizungumzi
Wakili. Ulimwambia Jaji Soko la Kilombero liko moja tu
Shahidi: Sikumwambia
Wakili: Sheli ni nini
Shahidi: Watatu wamezoea kutumia jina hilo
Wakili: Wakati wanatoka Morogoro kwenda Moshi walikuwa wanafahamu kuwa wanaenda kufanaya vitendo vya kigaidi
Shahidi: Walikuwa wa nafahamu
Wakili: Kati ya Mbowe na Urio nani alikuwa anawafahamu
Shahidi: Aliyekuwa anafadhili
Wakili: Mbowe na Urio nani alikuwa Morogoro
Shahidi: Urio
Wakili: Nani aliyewatongoza
Shahidi. Urio
Wakili. Urio ni mtoto mdogo
Shahidi: Mtu mzima
Wakili: Urio yuko hapa kizimbani
Shahidi: Hayupo
Wakili: Mheshimiwa Jaji kama wenzangu watakubali naomba niahirishe tuendelee tena kesho kwa kuwa nina maswali mengi.
Wakili Kidando: Hatuna pingamizi na tulishakubaliana naomba tuahirishe shauri hili hadi kesho.
Jaji: Kufuatia maombi yaliyoletwa na upande wa utetezi na kuridhwa na upande wa mashtaka naahirisha shauri hili hadi kesho saa tatu asubuhi ambapo upande wa utetezi wataendelea kumuhoji shahidi, shahidi unaonywa kuwa kufika kwaajili ya kuendelea kutoa ushahidi na washtakiwa mtaendelea kuwa chini ya uangalizi wa magereza.