Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya Mbowe na wenzake yaanza

Mbowepic Kesi ya Mbowe na wenzake yaanza

Mon, 10 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi leo Jumatatu Januari 10, 2022 inaendelea na usikilizwaji wa kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na wenzake watatu baada ya kesi hiyo kusimama kwa siku 21 kupisha sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya 2022.

Washtakiwa tayari wameshafikishwa katika ukumbi wa Mahakama hiyo.

Tayari mawakili wa pande zote mbili nao wameshafika katika Mahakama kwa ajili yakusikiliza uamuzi hukusiana na kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi.

SOMA: Kesi ya kina Mbowe kuanza kesho kwa uamuzi

Leo, Januari 10,  2022 Jaji Joachim Tiganga anayesikiliza kesi hiyo anarajia kutoa uamzi kuhusiana na kielelezo ambacho ni sare za Jeshi la Ulinzi wa Wananchi Tanzania , zilizopingwa na upande wa utetezi zisipokelewe  na mahakama kutokana na kukiuka matakwa ya kisheria.

Endelea kufuatilia Mwananchi ili kupata kile kinachojiri mahakamani hapo

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: