Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Karani aliyetoweka na Sh 600,000 za Sensa akamatwa akitaka kutapeli tena

Karani Matei Karani aliyetoweka na Sh 600,000 za Sensa akamatwa akitaka kutapeli tena

Thu, 25 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia Karani wa Sensa Kata ya Ilomba Jijini Mbeya LUtengano Mwakibambo kwa tuhuma za kutofika kwenye kituo cha kazi alichopangiwa kwa kusingizia kuwa anaumwa.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, SACP Ulrich Matei amesema mtuhumiwa baada ya kulipwa Tsh. 600,000 kama malipo ya awali alitoweka lakini Agosti 21, 2022 baada ya kusikia malipo ya awamu ya pili yanatolewa alirudi tena kwa ajili ya kusaini fedha hizo na ndipo akakamatwa na sasa anaendelea kuhojiwa ambapo upelelezi ukikamilika hatua nyingine za kisheria zitafuata.

"Kuna mtu ambaye alilipwa pesa zake akatakiwa aende kituoni kwake kuhesabu sense, lakini hakwenda. Tumemkamata na yupo lokapu sentro kwa sababu amelipwa pesa za serikali na kazi ile hajaifanya, hatuwezi kukubali, huyo tunamzuia," amesema Kamanda Matei.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: