Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#KESIYAMBOWE: Kuendelea tena leo

Mbowe3 Washnda Ushahidi kesi ya kina Mbowe kuendelea leo

Mon, 17 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama Kuu leo itaendelea kusikiliza kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu baada ya kuahirishwa Ijumaa iliyopita.

Katika mwendelezo wa kesi hiyo, mahakama leo itapokea ushahidi kutoka kwa shahidi wa 10 wa upande wa mashtaka kati ya mashahidi 24 wanaotarajiwa kutoa kushahidi katika kesi hiyo.

Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Halfan Bwire Hassan, Adamu Hassan Kasekwa na Mohamed Abdillahi Ling’wenya.

Miongoni mwa mashahidi wa upande wa mashtaka wanaotarajiwa kutoa ushahidi wao ni pamoja na Luten Denis Leo Urio.

Urio ni ofisa JWTZ kutoka kikosi cha makomando, ambaye kwa mujibu wa upande wa mashaka, ndiye aliyeibua tuhuma zinazowakabili washtakiwa hao.

Wengine ni aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Kamishna wa Polis (CP) Robert Boaz, mke pamoja na mwenye nyumba wa mshtakiwa wa kwanza (Bwire), ofisa wa Polisi kitengo cha makosa ya mtandao, anayediwa kuchunguza mawasiliano ya Mbowe na washtakiwa wengine.

Wiki iliyopita shahidi wa tisa alikuwa ni mwanasheria wa kampuni ya huduma za mawasiliano ya simu za mkononi, Gladys Fimbari, ambaye pamoja na mambo mengine katika ushahidi wake alielezea miamala ya inayodaiwa kufanywa na washtakiwa hao kwa lengo la kufadhili vitendo hivyo.

Ushahidi mwingine kama huo ulitolewa na mwanasheria wa kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Mic Tanzania Ltd, maarufu kama Tigo, Fredy Kapala ambaye ni shahidi wa tano katika kesi hiyo aliyetoa ushahidi wake Novemba 2, 2021.

Kwa upande wa washtakiwa tayari wameshafikishwa mahakamani hapo, huku mawakili wa pande zote wameshafika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: