Viongozi wa utawala wa kijeshi wa Niger wanasema hawawezi kukubali ziara ya ngazi ya juu ya kidiplomasia kwa sababu kutakuwa na hatari za kusalama kwa viongozi.
Wajumbe kutoka kundi la kikanda la Ecowas, Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa walikuwa wanatarajiwa kuwasili leo. Lakini viongozi wa mapinduzi waliiambia Ecowas kwamba vikwazo na tishio la uvamizi kutoka kwa jumuiya hiyo vilizua hasira ya umma, hivyo ujumbe haungeweza kukaribishwa kwa utulivu na usalama.
Waliongeza kuwa mipaka ya ardhi na anga ya Niger imefungwa. Ripoti kutoka mji mkuu wa Niamey zinasema watu wengi wameyapokea mapinduzi hayo kama pumzi ya hewa safi, ingawa Rais aliyepinduliwa, Mohamed Bazoum, alichaguliwa kidemokrasia.
Washington imeonya kuwa kuna hatari mamluki wa Wagner wa Urusi watachukua fursa ya mapinduzi ya Niger.